Msaada: Huyu ni nyoka wa aina gani?

Kumbe naweza kumfuga kwa ajili ya panya kama paka
 
umejuaje ni black mamba na ili hali hujaangalia ndani ha mdomo wake ??
Unamuona tu kwa rangi yake ya juu..japo wapo wachache mnooo wanafanana na Black mamba...watu tumeishi mazingira ya nyoka
 
Watumie hiyo picha wale wa South Africa wa kipindi National Geographic Channel kinaitwa snake in the city kama sijakosea...ila watasikitika sana kuona umemuua maana wao huwa hawauii.
 
Kumbe naweza kumfuga kwa ajili ya panya kama paka
Yes inawezekana kabisa na akakua mkubwa kama 3m cha msingi asiwe anatoka tu nje maana watu wakimuona wataanza kukuhusisha na imani zingine au wakakuulia mifugo wako pendwa😀
 
Watumie hiyo picha wale wa South Africa wa kipindi National Geographic Channel kinaitwa snake in the city kama sijakosea...ila watasikitika sana kuona umemuua maana wao huwa hawauii.
Yeah yule jamaa na mke wake watapandwa na jazba na kujiuliza ni jamii gani hii haijali haki za kuishi kwa wanyama wengine?😀
 
Sio kweli kuna nyoka wengi sana wana rangi hiyo na sio black mamba
Black mamba anaweza kujulikana kwa rangi nyeusi ilyokolea ndani ya mdomo wake pale anapofoka au akisimama wima kwa 3/4 ya mwili wake vinginevyo ni rahisi kumchanganya na aina nyingine ya nyoka kwa rangi yake.
 
Huyu nyoka hana shida kama hujamchokoza huonekana majira ya mchana pekee, nimepishana nao katika harakati za kilimo huko Kimashuku, kwa jina simjui.
 
Huyu nyoka hana shida kama hujamchokoza huonekana majira ya mchana pekee, nimepishana nao katika harakati za kilimo huko Kimashuku, kwa jina simjui.
Anaitwa brown house snake mkuu. She is completely harmless to humans
 
Yes inawezekana kabisa na akakua mkubwa kama 3m cha msingi asiwe anatoka tu nje maana watu wakimuona wataanza kukuhusisha na imani zingine au wakakuulia mifugo wako pendwa😀
Nyumbani wageni hawatakanyaga 🤣
 
Nyumbani wageni hawatakanyaga 🤣
Wakija unamwambja nyoka wako, ingia chini ya uvungu na usitoke🤣
Kimbembe wageni wanakula mezani alafu akajitokeza na kumpandia mmoja wapo mguuni maana kwa asili nyoka wanavutiwa na harufu nzuri nzuri kama za vyakula especially harufu ya wali. Sipati picha huyo mgeni atakavyoibwaga hiyo dinning table na vyakula vyote chini kwa kihoro🤣🤣🙌
 
Kuna dawa inauzwa katika maduka ya pembejeo za kilimo ni ya nyoka na wadudu unapulizia tu hiyo kwisha kazi
 
Daah wee jamaa nyama nyeupe io proten pure, uyoo mama nyokaa ukimuuaa wahi kumweka kwenye fridge Afu nifwate pm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…