Msaada: Huyu ni nyoka wa aina gani?

Msaada: Huyu ni nyoka wa aina gani?

Mleta mada toa location yako kwanza maana tusije tukatoa ushauri wa mkazi wa Tabora kumbe wewe mkazi wa Dar upo hapo Tegeta.

Location muhimu.
 
Huyo ni koboko ila ni Bado mtoto sasa hapo baba na mama yake itakuwa wanamtafuta mtoto jipange mkuu

Kama ni black mamba ni bora umeiondoa familia kwa maana sumu yake sio poa, akikugonga huponi.

Pole na hongera kwa kufanikiwa kumdhibiti. Nadhani anaweza akawa black mamba/koboko.

Njia ambayo nimewahi kuitumia kudhibiti nyoka ni kumwaga mafuta machafu kuzunguka nyumba yote na baadhi ya maeneo ambayo unahisi wanaweza kuwepo.
Huyo sio black mamba au Koboko kwa jina lililozoeleka kwasababu Morogoro ipo kwenye ukanda wa tropical savannah ambao ina receive bimodal rainfalls and two peak of high rainfalls ambapo Koboko hapendi kuishi kwenye maeneo ya ukanda kama huo. Blackambas wanapendelea kuishi kwenye ukanda wa savannah yenye rock hills yasioyokaliwa na binadamu.
Huyo ni brown house snake na Hana shida hata kidogo kwa binadamu, ni uoga wa watanzania na kutokuwa na elimu ya hawa viumbe so wamuonapo nyoka yoyote tu wanajua wapo kwenye hatari. Kuna zaidi ya species 3000 ya nyoka duniani lakini ni 200 tu wenye uwezo wa kumdhuru binadamu.
 
Nipo naangalia kipindi cha snake in city hapa hapa jamaa hao anawapapasa na mkono kama anachezea fimbo!

Ana hatari huyu!!!
Yule jamaa na mkewe wana kitu cha ziada, na halafu wanawarudisha porini... Wakifa wanawazika kabisa... Ujasiri walionao si mdogo
 
Huyo sio black mamba au Koboko kwa jina lililozoeleka kwasababu Morogoro ipo kwenye ukanda wa tropical savannah ambao ina receive bimodal rainfalls and two peak of high rainfalls ambapo Koboko hapendi kuishi kwenye maeneo ya ukanda kama huo. Blackambas wanapendelea kuishi kwenye ukanda wa savannah yenye rock hills yasioyokaliwa na binadamu.
Huyo ni brown house snake na Hana shida hata kidogo kwa binadamu, ni uoga wa watanzania na kutokuwa na elimu ya hawa viumbe so wamuonapo nyoka yoyote tu wanajua wapo kwenye hatari. Kuna zaidi ya species 3000 ya nyoka duniani lakini ni 200 tu wenye uwezo wa kumdhuru binadamu.
Aisee, ila nyoka ni kiumbe kinatisha aisee sijui kwa nini.

Halafu wanafanana, sasa kuliko kujipa matumaini hatokua na sumu ni bora kuua tu, tatizo unaweza mkanyaga bahati mbaya akakudhuru.
 
Naon watu wengi wameweka attention kwa huyo aliyetumwa..

ishu ni HUYO mkubwa ambaye hajulikani urefu wake huyo ndio tatizo kubwa.

Mtoa mada unachotakiwa kufanya ni kulala usiku huu wa leo.

Kesho anzq OPERATION maalum ukishirikiana na majirani.

Fanya searching procedures ambazo utakuw na checklist yako maalum.

Hakikisha unaanza na kwako na kwa jirani zako pia at least nyumba 3 ktk mzunguko wa nyuzi 360°, means nyumba 12 zinatakiwa ziwe ktk operation maalum.

Swala la Nyoka sio la kupuuzia, hawana maana hao. The way unavyochelewa ndio wanazidi kupazoea hapo kwako.

Kingine jitahidi usafi na hakikisha una mifugo kama BATA na Mbwa.
 
Aisee, ila nyoka ni kiumbe kinatisha aisee sijui kwa nini.

Halafu wanafanana, sasa kuliko kujipa matumaini hatokua na sumu ni bora kuua tu, tatizo unaweza mkanyaga bahati mbaya akakudhuru.
Kila nyoka ana sifa zake za kipekee na mazingira wanayopendelea kuishi. Ina hitaji umakini wa hali ya juu kuweza kuwatambua na kujua mpaka aina ya sumu wanayotoa ili incase ikitokea ukang'atwa ujue unapaswa kuchukua hatua gani.
 
Huyo anaweza kuwa kifutu au Cobra, ni aina ya nyoka wanaosimamisha kichwa na kuvimbisha shingo kama afanyavyo chura anapochokozwa. Mmemponda kiasi cha kutotambulika kirahisi....Utadhani Israel anavyowaponda wapalestina bila huruma? 😳
 
Tungeona kichwa ingekuwa rahisi, mwagia mafuta ya taa na oil chafu mara kwa mara watahama tu hapo.
 
Peace,

Wakuu jirani yangu amekua ananiambia hua anamwoma nyoka mkubwa nyakati za jioni akikatiza katika uzio wake. (Uzio unaotutenganisha) awali nilidhani ananitania maana manawake huwa waoga waoga tu akiona kijiti anaweza kusema nyoka au pia utani na masikhara

Lakini kwa umri wake sio mtu wa utani (mama mtu mzima) aliponiambia mara ya pili na ya tatu nikaanza kua makini. Sasa leo jioni hii upande wa pili na kule anakoniambia nimekutana na huyu nyoka nikamuua.

Nilipomuita aje kumtazama akasema nyoka anayemuonaga ni kama huyu kwa muonekano ila mkubwa zaidi, akasema ni kama mara 3 kwa unene na urefu hana uhakika maana hua hamuoni mwanzo mpaka mwisho wake.

Wakuu hapa naona sasa nahitaji kukaa mguu sawa maana ni kama kuna kambi ya hawa viumbe maeneo haya tuna share oxygen pamoja. Huyu niliyemuua anaweza kuwa mtoto wa huyo anaeonekana. Hapa kutakua na kiota.

Wakati najipanga kuwakabili hawa wajomba naomba aliye na ufahamu wa aina za nyoka anifahamishe huyu ni aina gani ya nyoka na tabia zake na je natakiwa kukabiliana nao katika mtindo upi.

(Najua utaratibu wa kuwataarifu mamlaka ya maliasiri lakini wote tunaifahamu nchi yetu kama ghorofa la Kishimba lilipoungua wakataarifiwa jeshi la zima moto sio tu walikuja siku iliyofuata yani walifika baada ya masaa 32 ila pia walikuja na gari halina maji, unaweza ukapata picha kuwategemea mamlaka za serikali ilivyo riskView attachment 2953224

Update: Nimelazimika kuihamisha familia (mke, watowo watatu na dada wa kazi) hapa nitabaki mwenyewe mpaka vita na hawa viumbe itakapofika tamati, maana kuna kila dalili huu mziki utakua bab kubwa. Hapa kutakua na kiota
Mkuu wala usihamishe familia. Just fanya hivi...

Tafuta wale siafu wanaong'ata sana wale. kisha wapandikize uani kwako. wataenea sana na hakika hautaona wala kusikia tena habari ya nyoka hapo kwako.

Nilisumbuliwa sana na majoka hapa kwangu na nilichokifanya ni kuwaleta hao wadudu. Nimewahi kushuhudia wakimalizana kibingwa na sir snake. wanampangusa haswaa wanamuacha skeleton kama samaki vile
 
Mimi NYoka ninayemuogopa kuachana na hao ma sijui mambas ni kifutu(puff adder) kwa sababu zifuatazo
(1) utulivu,ni NYoka mpole hapendi kushambulia watu hivyo akishiba kama reptile wengine hupendelea kuota jua kusaidia mfumo wa chakula,

Sasa hapa anakaa kwenye njia ambayo watu hupita Ili kuchomwa na jua vizuri na anajikunja vizuri na kufanana na mazingira kiasi Cha ndege na nguchiro kumuona na binadamu pia
(2) usipomuona ukamkanyaga vizuri lazima ata panick na kukung'ata na kukuachia cytotoxic venom ambayo usipowahishwa hospital haraka unaweza kukosa mguu

Black mamba na cobras tumewazoea wakituona wanasepa kwa Kasi ya ajabu unless mfungiane mahali
 
Nyoka hana shida kama hujamchokoza
Hivi hua huogopi kabisa hawa viumbe ww😳😳😯
 
Back
Top Bottom