Msaada: Huyu ni nyoka wa aina gani?

Msaada: Huyu ni nyoka wa aina gani?

[emoji16][emoji16][emoji16] we acha uongo
Sio uongo ni kweli hana sumu huyo
Screenshot_20240403_223026_Google~2.png
 
Da'Vinci Sijapenda!!!!! Umenifanya nimetupa simu moyo unaenda mbioo
Bahati nzuri nipo kitandani simu haijaanguka chini....
Acha masihara tabia zingine upuuzi mtupu!
Ulisema hutofungua picha Nini kilikufanya uzifungue?
 
Kama ni Morogoro basi atakuwa ni BROWN HOUSE SNAKE ambao wanapenda sana kukaa kwenye makazi ya watu wakila panya, mijusi. Ni nyoka wasio na sumu na ni completely harmless to humans.View attachment 2953250 wanapatikana kwa wingi sana Morogoro mjini.
Nadhani nimekusaidia mkuu
nashukuru sana mkuu, kumbe nimeua nyoka asie na madhara
 
Peace,

Wakuu jirani yangu amekua ananiambia hua anamwoma nyoka mkubwa nyakati za jioni akikatiza katika uzio wake. (Uzio unaotutenganisha) awali nilidhani ananitania maana manawake huwa waoga waoga tu akiona kijiti anaweza kusema nyoka au pia utani na masikhara

Lakini kwa umri wake sio mtu wa utani (mama mtu mzima) aliponiambia mara ya pili na ya tatu nikaanza kua makini. Sasa leo jioni hii upande wa pili na kule anakoniambia nimekutana na huyu nyoka nikamuua.

Nilipomuita aje kumtazama akasema nyoka anayemuonaga ni kama huyu kwa muonekano ila mkubwa zaidi, akasema ni kama mara 3 kwa unene na urefu hana uhakika maana hua hamuoni mwanzo mpaka mwisho wake.

Wakuu hapa naona sasa nahitaji kukaa mguu sawa maana ni kama kuna kambi ya hawa viumbe maeneo haya tuna share oxygen pamoja. Huyu niliyemuua anaweza kuwa mtoto wa huyo anaeonekana. Hapa kutakua na kiota.

Wakati najipanga kuwakabili hawa wajomba naomba aliye na ufahamu wa aina za nyoka anifahamishe huyu ni aina gani ya nyoka na tabia zake na je natakiwa kukabiliana nao katika mtindo upi.

(Najua utaratibu wa kuwataarifu mamlaka ya maliasiri lakini wote tunaifahamu nchi yetu kama ghorofa la Kishimba lilipoungua wakataarifiwa jeshi la zima moto sio tu walikuja siku iliyofuata yani walifika baada ya masaa 32 ila pia walikuja na gari halina maji, unaweza ukapata picha kuwategemea mamlaka za serikali ilivyo riskView attachment 2953224

Update: Nimelazimika kuihamisha familia (mke, watowo watatu na dada wa kazi) hapa nitabaki mwenyewe mpaka vita na hawa viumbe itakapofika tamati, maana kuna kila dalili huu mziki utakua bab kubwa. Hapa kutakua na kiota
jiandae ukoo wa huyo nyoka unakuja kwenye maomboleze ya mwenzao
 
Huyo atakuwa Black mamba wale wanajikunjaga wanaruka umbali mrefu kama sikosei ila pia huwa wanakimbiza adui yaani kumuua kama ni wale wakubwa inahitaji akili kubwa
umejuaje ni black mamba na ili hali hujaangalia ndani ha mdomo wake ??
 
huyo ni nyoka wa kawaida mara nyingi hupendelea kuishi karibu na makazi ya watu wanakula panya na wadudu wengine wakati mwingine mabaki ya chakula Hawana sumu kali akikung'ata unaweka hata sarafu ya 50 kwenye jeraha na unapona mapema tu
Na ni ngumu sana mpaka akuvamie labda umkanyage
Tunawaita home snake ni mweusi lakini ana kama ukijivu kwa mbali kwenye ngozi yake
Mkuu rudisha familia hao nyoka ni sehemu ya familia ungekuwa Arusha ningekupa mchongo wa kuwauza kwa jamaa mmoja hapa town..
 
Nyoka hana shida kama hujamchokoza
Nyoka hahitaji kuchokozwa ili akuzuru, nyoka ameumbwa kuzuru, so ukimuona maeneo ya makaazi muwahi, umuue ukimkuta porini mdiyo umuache
 
Morogoro Kuna nyoka wengi Sana,tunapishanaga na vifaranga Hadi ndani,ni shida.uwatafute maliasili wakwambie dawa ya kuwavuta ili uwaone na kuwaua wote ni hatari
 
Tofauti ya mzungu na mswahili iko hapo. Mswahili akiona nyoka anauwa. Mzungu akiona nyoka anamkamata na kumpeleka mahala pake
 
Fuga paka na bata pia kwenye Nyumba yako nyoka na paka na Bata ni vitu viwili tofauti paka wapo active sana asa akigundua ilo eneo lina nyoka kila siku atakua anafanya kazi ya kuwinda nyoka usisahau kuchoma tairi la Gari oil mwaga chumvi ya mawe kwenye mashimo yote yanayozunguka nyumba
 
Back
Top Bottom