1. Mafuta. Itakua ngumu kujudge kwasababu haujawa specific kwenye mwaka, na engine size. Pia kuna model hapo zinatumia petrol na zingine diesel. Ila Mazda ya diesel 2.2 L itakua inakunywa wese kiduchu.
2. Uimara. Zote nzuri kwasababu za Japan. Wajapan wanajitahidi sana. Ila Toyota hana mpinzani, kisha Mitsubishi na Mazda wanapokezana. Ila still kuna factors nyingi mfano model year, matumizi ya owner akietangulia na service history.
3. Speed ya nini? Ukitaka speed chukua performance cars kama Audi, BM na Benz.
4. Vipuri. Zote unapata. Kariakoo wana spare hadi za Tesla.
5. Ukisasa. Nunua latest. Utaenjoy. Ila uyo bwana outlander outdated kama jina lake.
6. Muonekano ipo subjective. Kama demu tu. Mwingine anapenda shepu la Zuchu mwingine Sanchoka.
7. Izo gari zote bei ni 25 to 30M.