Msaada: Je, unaweza kupata nakala ya taarifa zako ulizojaza NIDA?

Msaada: Je, unaweza kupata nakala ya taarifa zako ulizojaza NIDA?

Mh! ulijaziwa hizo taarifa mpaka usizijue..? unahabari haohao nida ukiomba namba yako wanakuuliza hizo taarifa ili wahakiki kama ni wewe sasa inakuwaje tena wewe ukazitafute hizo taarifa ikiwa wao wenyewe walizipatia kwako!!!!!
 
Mh! ulijaziwa hizo taarifa mpaka usizijue..? unahabari haohao nida ukiomba namba yako wanakuuliza hizo taarifa ili wahakiki kama ni wewe sasa inakuwaje tena wewe ukazotafute hizo taarifa ikiwa wao wenyewe walizipatia kwako!!!!!
Sehemu niliyojiandikisha nilikua mgeni, sijui ule mtaa unaitwaje na nilienda mara moja tu

Pia namba za cm nilizokua natumia wakati huo sizikumbuki tena
 
Tumia app ya mixx by Yas utaweza ona kata ya makazi ya kudumu na kata ulipoandikishwa hiyo Nida
 
Sehemu niliyojiandikisha nilikua mgeni, sijui ule mtaa unaitwaje na nilienda mara moja tu

Pia namba za cm nilizokua natumia wakati huo sizikumbuki tena
Hapo chachaa. Ukipata kuulizwa km jina la mama au shule uliosoma kdg itakuwa afadhali. Lkn hayo mambo ya kata inakuwa mtihani hasa km sehemu uloandikisha ulikuwa mgeni. Halafu vijana wa siku hizi kila kitu hamkumbuki. Nyie kila jambo mnachkulia easy tu
 
Sehemu niliyojiandikisha nilikua mgeni, sijui ule mtaa unaitwaje na nilienda mara moja tu

Pia namba za cm nilizokua natumia wakati huo sizikumbuki tena
Utapata ugumu maana wewe ndo unatakiwa kutoa hizo taarifa ili wazipate kwenye system
 
Nenda wilayani ofisi za nida wana info zako hakikisha una supporting documents cheti cha kuzaliwa, vitambulisho vingine kama voter's, bima , vyeti vya shule nk

NB mkono mtupu........
Msiwasingizie sio kila mtoa huduma hiyo anahitaji pesa, kuna watu wanahudumia vizuri kabisaaa na anakwambia ni kazi yangu kukuhudumieni wananchi
 
Sehemu niliyojiandikisha nilikua mgeni, sijui ule mtaa unaitwaje na nilienda mara moja tu

Pia namba za cm nilizokua natumia wakati huo sizikumbuki tena
kama namba yako ya nida unayo nitakuelekeza kuangalia kata yako!
namba nane za awali zinahusu taarifa zako za mwezi mwaka na tarehe ya kuzaliwa, namba tano zinazofuata zinahusu kata yako so kama huijui ziandike hizo namba Google itakuonyesha ni kata ipi!.

andika hivi mfano: "33219 Tanzania postcode location"
kisha search itakuletea ni kata gani huo mfano niliokuonyesha hiyo ni kata ya kawekamo ipo mwanza wilaya ya ilemela.
 
Back
Top Bottom