Msaada: Jirani yangu ni mbabe na msumbufu

Pole jaribu pitia upya karatasi yako ya kuuziwa hilo eneo urefu na upana wake, Kama uko sahihi ni haki yako songa mbele kudai haki yako ila mwisho wa siku usiache nia yako njema ya kuacha barabara kwa majirani zako
 
Usicheke na waswahili watakupanda kichwani.

Nipe tenda hiyo nimuwekee ngozi za chui uwani halafu namletea kipira, huyo mtaonana baada ya miaka 30 kama atatoka jela salama
 
Pole jaribu pitia upya karatasi yako ya kuuziwa hilo eneo urefu na upana wake, Kama uko sahihi ni haki yako songa mbele kudai haki yako ila mwisho wa siku usiache nia yako njema ya kuacha barabara kwa majirani zako
Wewe huwajui waswahili, hawa ni wa kuwavalia sura ya kazi, jirani mwema atajionesha kwa matendo yake na jirani mshenzi muoneshe wewe ni mshenzi kuliko yeye.
 
🤣🤣🤣🤣🤣 weeee wapo unanijaza upepo wew nijichanganye kwenye kumi na nane za jirani akishindwa huku ataenda kule
Nakwambia hamna lolote, dar hakuna mganga wote ni wachumia tumbo.
 
Hati au Ile karatasi ya mauziano si inaonesha ukubwa wa kiwanja chako? tumia hiyo kutatua huo mgogoro kwa kuonesha karatasi moja wapo. ikishindikana wapeleke kwenye mabaraza ya aridhi
 
 
Kwa maelezo yako mimi nahisi wewe ndie tatizo.

1. Kama wewe ulitoa njia kwenye eneo lako mashahidi walikuwa kina nani?

2. Kama eneo ni lako why usiwape documents zako za umiliki kama ushahidi ?

3. Kama wewe ndie ulietoa njia, why wenyekiti na viongozi wa mtaa wasiwe upande wako ?

4. Majirani wote kwa nini hawakutetei wewe ?
 
Ukifunga barabara ambayo imeishapitika zaidi ya miaka mitatu litakuwa kosa na itakula kwako.
ushauri wangu ni kwamba,kama aliyekuuzia bado yupo hai mtumie.maana atakuwa anajua mipaka ya eneo alilokuuzia.Itakusaidia kumnyamazisha huyo jirani yako.
Pili,kama kwenye barua uliyonunulia inaonyesha ukubwa wa kiwanja chako,waambie hao viongozi mkafanye vipimo ili ukweli uwe dhahili.
 
mie nafkir ungekuja na picha ya ukuta ulivyo njia na panapowagombanisha na iman ungepata msada zaid wa mawazo kwa wadau hapa ila kwa maelezo tu aijtoshelez mfno ujataja sehem usika pia pengne ote mnavunja shelia sehem aistahil ujenz ila pole kwa changamoto
 
Kaka 😂😂😂😂
 
Wewe huwajui waswahili, hawa ni wa kuwavalia sura ya kazi, jirani mwema atajionesha kwa matendo yake na jirani mshenzi muoneshe wewe ni mshenzi kuliko yeye.
No sawa apime eneo tu Kisha kama ni lake kweli adai haki yake, hata hiyo njia anaweza toa kwa wapitaji na yeye kulipia sehemu ya ardhi iliyotolewa, suala ya njia ya kupita ni haki ya msingi katika Sheria ya Ardhi ila haipatikani bure awauzie tu, kiungwana
 
Fuga nyoka wengiii,na kila siku hakikisha anakutana na nyoka mlangoni kwake,huyo lazima atakupisha na utaishi kwa raha bila jirani mkorofi🤸‍♂️🤸‍♂️🤸‍♂️🤸‍♂️
 
Kwani eneo lako halina mpaka? Na kama lipo hadi serikali z mitaa c wanajua mipaka yako kama kweli upo sahihi iweje wote waseme umekosea wew kama una hati ya kiwanja c inaonyesha mipaka?
 
Ukiona kwenye sheria anakuwahi kwa mbele basi uchague moja ya kua mpole au ufunge safari ya kusini au magharibi mwisho wa reli
Mtu anayekuwahi kwa mbele kwenye sheria hii huwa balaa sana, na mwisho wake huwa mgumu sana.
 
Swala lako mbona ni rahisi kabisa Mkuu.

Kwakuwa maeneo yana ukubwa fulani basi ni wazi eneo lako litakuwa limepungua.ukubwa baada ya wewe kutoa sehemu ya bara bara. Sasa wewe chukua mkataba wako waoneshe ukubwa alafu mpime eneo kisha mtapata ukubwa uliosalia. Ugomvi unahamia kwake.

Mfano eneo lako ni 30M*30M sasa wewe umemega 1.5M moja kwa moja eneo lako litabaki 30M*28.5M. Vile vile lipimwe na eneo lake ujulikane ukubwa wake ni ngapi, namba hazidanganyi ukweli utakuwa wazi.

Usihangaike sana na wajinga wacha wajihangaikie wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…