Msaada: Jirani yangu ni mbabe na msumbufu

Msaada: Jirani yangu ni mbabe na msumbufu


Pole yalinikuta viongozi wamepewa mgao hapo jiandae kulogwa kama unaweza na ww tafuta fundi akuwekee Sawa vinginevyo hutawaweza
Sifungamani na hayo mambo ndugu
 
Km kiwanja ulikinunua, aliyewauzia ndo anapaswa kuja kumaliza utata huo. Kwanza hii kesi ndogo. Maana, wewe barua yako imeandikwa ni mita ngapi za kiwanja chako, hata mkifika mbele ya Sheria, hizo hati za kununulia kiwanja ndo zitaanika ukweli. Pole sana, mambo ya viwanja ukipakana na mtu mbinafsi, migogoro haiishi.
 
Chukua kuku usimchinje mnyonyoe manyoya yote, mvalishe shanga kisha mtupie kwake.
Baada ya siku 3 chukua paka mnyoe panki, mvalishe kitu kama hirizi mtupie kwake
Siku ya 5 chukua chura mvalishe maguo, mshonee ndani awe kama hirizi kisha tupia kwake,
Siku ya saba nunua drone, iveshe nguo nyeupe irushe juu iwe kama jini linapepea.

Utakuja kunishukuru 😂
Nimecheka sana,hiyo ya kwanza na ya pili amewahi kufanya Pasta Hananja enzi zake za ujana
 
Kabla ya kununua kiwanja jaribu kuangalia jirani zako , wakati wa kuweka mipaka hakikisha wapo wote pamoja na huyo anayekuuzia.
Mimi huko nyumbani kuna eneo nimenunua msituni kabisa mwisho wa makazi ya watu ,nikizeeka nitaishi huko sitaki kero kabsa.
 
Aje na hati yake aonyeshe ukubwa wa eneo lake, lipimwe ili ijulikane nani ameingia nani ametoka
 
Chukua kuku usimchinje mnyonyoe manyoya yote, mvalishe shanga kisha mtupie kwake.
Baada ya siku 3 chukua paka mnyoe panki, mvalishe kitu kama hirizi mtupie kwake
Siku ya 5 chukua chura mvalishe maguo, mshonee ndani awe kama hirizi kisha tupia kwake,
Siku ya saba nunua drone, iveshe nguo nyeupe irushe juu iwe kama jini linapepea.

Utakuja kunishukuru 😂
🤣🤣🤣🤣Matokeo yake ni yapi mkuu kukimbia eneo au inakuwaje ila unavisa sana
 
Hahah naona baada ya hapo The beekeeper unataka ukakichafue kama kwenye movie...
Ushawahi kusikia story mpaka unajiuliza huyu anayesemwa ni mimi au ni mwingine?😂🤸 Leo nimecheka sanaa
 
Pole sana Mkuu kwa changamoto unayopitia. Changamoto hiyo imewahi kunitokea Mjumbe alinunua eneo Dogo kajenga lote akaongeza mpaka kwangu. Niliponunua Nyumba nikaikuta hali hiyo ya mgogoro. Nikamwachia nafasi bado hakutosheka.

Chukua ushauri niliotumia. Mtafute aliyekuuzia Eneo atoe ushahidi, kama Wajumbe na Wenyeviti wako upande wake wala isikusumbue Wewe pandisha ngazi moja baada ya nyingine (Mtendaji, Halmashauri).

Wakishaona uko serious utaona watakavyokufuata kuomba radhi usiwaharibie kwa Viongozi wa juu. Usiketi nao chini kuwasililiza kwa sasa watakuvuruga mpaka uongee peke yako au ufanye uamuzi utakaojutia.
 
Back
Top Bottom