Msaada juu ya tatizo hili la mkopo wa bank


Duka la Dawa Muhimu halihitaji kuwa na pharmacist, ndo point nzima ya mradi huu kuleta maduka yanayoweza kuprovide basic medicine kwa wananchi bila complication ya kufungua Pharmacy ya kweli ulikuwa unapitia kozi fupi tu unafungua.

Sasa sielewi imekuwaje TFDA wameamua kuyafunga baadhi ya maeneo nadhani kuna wakubwa wanaona inawapunguzia biashara kwenye pharmacy zao.

Kwa upande wa deni itabidi ulipe kivyovyote, benki inaweza ikaadjust muda wa mailpo labda lakini kwa vile umeweka nyumba deni limekuwa lako pia sio la biashara tu, hii ndo hatari ya ku cosign loans.
 
Hapo kune Escrow nyingine,watu watakuwa wameishapiga hela kwa wenye maduka makubwa ya Dawa ili nyie vidagaa muhame mji.
Hembu jiungeni na undeni umoja wenu wa muda kisha tafuteni mwanasheri mzuri muwapeleke Mahakamani.
Hakuna sheria hiyo.
Dar ndio jiji kubwa,lakini katikati ya mji kuna maduka kama hayo kibao.

Kwa maelezo hayo hapo ni Dhulma tu,na mkiona mkuu wa mkoa wenu nae anajifanya bingwa wa mipango mjue kaisha kula chake.
Machinga wahamishwe,mamalishe watimuliwe,hadi duka la dawa?kisa matajiri ndio wafanye biashara.
Iteni waandishi wa habari,maana hawa ndio wazee wa kuibia uonevu huu.Kisha tafuteni mwanasheria wenu mfungue kesi.

Maana haya huko mtapohamia wakiona kuna tajiri mwingine anataka kuwekeza kwenye biashara hiyo watawaambieni nendeni vijijini.

Msikubali kirahisi namna hiyo,haki yenu kisheria ipo
 

Ukweli mtupu mkuu,inasemekana zonal pharmacyst ana famasi zake huko pembeni pia hawa mafamasia wa jiji mkoa na wilaya wanafamasi hivo wadelete hizi ndogo ili biashara ibaki upande wao,maana hii issue ya maduka ya dawa muhimu imekua ni sera ya taifa na kila aliekua na duka alihudhuria mafunzo pia akaajili muuzaji mwenye sifa walizotaka lakn wanabadilika tena.
 

Mkuu bank watanipa hata chance ya kujipanga hata 3month ndo anaanza kulipa maana kwa muda huo nitakua na kitu mbadala.
 
Na ndio maana nikasema.Hapo kuna hujma ya wafanyabiashara wakubwa kwa kulishia rushwa
Nyie fanyeni haya
a)Iteni waandishi wa Habari,hakikisheni na ITV wamo
b)Jiungeni umoja wenu wa wenye maduka ya Dawa madogo na ya kati
c)Tafuteni mwanasheria kisha muende mahakamani
Na hapo mnaishtaki wizara ya Afya,maana ilitoa matangazo hadi kwenye TV kwa umuhim wa maduka hayo.
Ili kujua sheria ipi inahusiana na kuhamisha maduka wakati yanavibali.

Hawa matajiri sijui wanatupeleka wapi.Na mkikaa kimya atatokea tajiri mwingine ataanzisha jingine kwa kujua watu wa mwanza sio wazee wa kulianzisha kama Arusha na Dar.
Angalieni mbeya ndio jiji kama Mwanza ila hawapelekeshwi kihivyo,Jiji la Mwanza tu ndio wakimya kila kitu mnaona sawa.
Arusha ndio wamepinda kabisaa,maana matajiri wote wanajua kwamba ukianza vita na raia kwa kuharibu biashara zao basi wanakuhesabia siku
 
Asante mkuu kwa ufafanuzi.
Sasa ndio nasema hapo kuna maduka ya wakubwa ndio yame ESCROW watendaji na kuamua kulianzisha zoezi bubu.
Dawa ni kuita waandishi wa Habari na kuipeleka wizara ya afya mahakamani.Hapo mkuu wa mkoa mwenyewe atawazingua tu.
Chezea pesa wewe
 
Kama mdhamana ilikuwa duka haina tatizo bank watazingatia,but kama ni nyumba duka halihusiki tafuta namna uwalipe pesa zao kwan hapo wanacheza na sheria zaid ya huruma wala ubinadamu.....poleh by the way......

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
This is one of the very useful thread in this forum

TheDealer .... accept my like please
 
Last edited by a moderator:
Nimekumbuka nyingine:

4. Jaribu kwenda kwenye ma benki nyingine uuze huo mkopo wako; then ukope kwao kwa masharti ya kuweka dhamana ya nyumba yako na sio tena biashara ya dawa!

Hope nimekusadia kiasi chake!

Again pole!

Huwezi kukopea nyumba ikiwa huna biashara inayoendelea, pia wale jamaa wa bank wanapenda sana kuuza nyumba za wateja wao
 
Mkopo ni mzuli lakini pia ni mbaya tatizo jingine ni kwamba kwenye biaahara yoyote mkopo ni wa muhimu sana
 
Wakuu mkopo umeisha cha moto nimekiona
Na nimejifunza kitu.
 
Mama yangu! Matatizo ndio yameanzia hapooo! Ndugu, kunusuru nyumba yako tafutaga tu pesa za watu uanze kurudisha taratibu taratibu. La sivyo watauza nyumba wale hawatakagi story... Hakuna kitu kibaya kama kuweka dhamana nyumba bank. Yani watakutesa mpaka upate presha... Mi mwenyewe nilikopa hela nikanunua gari ya biashara na baada ya mda mfupi tu ikapata ajali. Ilibidi nitafute pesa nipunguze deni. Deni ukishalilipa hadi 70% hakuna bank itakuwa na mandate ya kuuza nyumba yako...
 
Kwanza mkopo ulikua bank ya posta.

Kifupi bank hawataki longolongo
Nilikonda kutoka kilo 97 hadi 75 mbaya sana biashara zote zilisimama mpaka kazini sikua na kipato cha maana.

Uzuri wa bank hii ni waungwana kupita bank zote na waelewa sana wanakupa uhuru uwambie mipango yako na unaweka maandishi
Kikubwa hawafuti deni kw
a msamaha labda ufariki.

Ushauri.
Usikope bank bila sababu maalum tena uwe na biashara inarun vizuri bila hivo utapa stroke bure.
 
Ningepedaushauri yafatyo, kwanza huspanik, hayo mambo po, na wewe sio wa kwanza,pili ILIYOfunga ni serikali, napostal bank ni ya rikali, lazi wa na melewano, tau piga picha tukioia, ambatanisha na barua ya kuomba adjustiment yaalipo ya mkop, nakala benk kikuu kito cha malalamiko ya wateja wa mabenk, na wizara ya fedha.

Mwisho kabsa kbra hujfanya haya yoteiulize, duka la limefungwa Kimakosa au la? na je km ni kimakosa ni kosa la nani?? ni lko au la rikali? km ni lako tfta jinsi ya kukaa kitako benki myamalize.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…