Msaada: Kaka Yangu Kahukumiwa Miaka 30 Leo

Msaada: Kaka Yangu Kahukumiwa Miaka 30 Leo

Umesoma na kumuelewa alivyoandika
Simu huwa zinanunuliwa madukani, iweje yeye anunue kwa mtu mitaani? Pili miaka 30 kwa simu tu haiingii akilini, lazima kuna makosa mengine kama ya ujambazi au wizi huyo kaka yako kayafanya. Refer kifungo cha Sabaya kwa miaka kama hiyo.
 
Pole sana sana mkuu, lakini kupitia kaka yako tunapata somo kua si vizuri kununua simu kwa mtu haijalishi ni nani.

Mkuu je ukipewa ushauri ambao utahitaji tena pesa itakuaje?? Ndio utakwama tena??
 
Pole sana ndugu
Ila nina swali kwamba aliemuuzia simu na yupo ndani au ndo huyo katoka??
Na je kaka yako aliuziwa simu akijua ni simu ya wizi??
Aliemuuzia ni mtu aliekua anapenda kutembelea mazingira ya pale alipokua akifanyia umachinga hakujua kama ni ya wizi, pia aliemuuzia simu hakuonekana tena mpaka leo

Kuhusu kujua kama ni ya wizi sjui maana walinunua vifaa kama simu2 mwingne alinunua laptop kwa bei chee
 
Kwa ufupi kesi ya kaka angu yeye ni machinga, aliuziwa simu na mtu baada ya kuitumia hiyo simu kama wiki mbili alikamatwa

Kosa ile simu aliyonunua ilipolwa kwa nguvu kutumia siraha na kupora vitu baadhi ikiwemo pkpk, na katka sakata hilo walikamatwa watu watatu akiwemo na yeye

Wakapelekwa polisi kwa upelelezi badae kesi ikaenda mahakamani wamekaa miezi tisa mmoja wao alitoka wiki mbili zilizopita wakabaki wawili,

Leo ilikua siku ya hukumu naimetokea kama nilivyoeleza hapo juu,

Nmeongea na kaka amelia sana anasema wamefungwa kwa kukosa hela ambapo mwenzao kesi ya pamoja ametoka kwa kutumia pesa

Kwaupande wetu pesa hatuna familia ya kimasikini naomba msaada kama kunautaratibu upi tuutumie kama familia, imeniuma sana kuona kaka anafungwa miaka yoote hiyo.

yuda exalioth
Jamiiforms
geita
Kiimsingi katika sheria, baada ya maamuzi kutolewa juu ya kesi yoyote nafasi inayobaki ikiwa kunaupande haujaridhika na maamuzi nikukata rufaa.

Naomba nitumie nakala ya hukumu DM then tuone tunafanyaje.
 
Rahisi ni ghali. Ndicho kilichomtokea kaka yako.

Huko huko GEREZANI kuna askari magereza ambao shughuli zao ni kusaidia wafungwa kukata rufaa. Hivyo na wewe mshauri aongee na askari hao wa kitengo cha sheria akate rufaa mahakama kuu.
Asante mkuu

yaani wamelalamika kwamba inakueje shahidi anakua ni askari wale wale waliowakamata ndio waliotoa ushahidi
 
Simu huwa zinanunuliwa madukani, iweje yeye anunue kwa mtu mitaani? Pili miaka 30 kwa simu tu haiingii akilini, lazima kuna makosa mengine kama ya ujambazi au wizi huyo kaka yako kayafanya. Refer kifungo cha Sabaya kwa miaka kama hiyo.
Je sheria inasemaje kama hiyo simu ilipolwa kwa kutumia siraha na ukutwe nayo?
 
Hizo ni story za upande mmoja unataka kutochota tukuonee huruma.
Ukute yeye ndiye jambaz wanaotembea na boda boda na panga usiku wakikukuta wanakuibia kibabe.
Binafsi sina huruma na mwizi wala mnunuaji wa Mali ya wizi
Unasema kweli rakini mkuu niamini mimi kwamba kaka sio mwizi na sio jambazi
 
Back
Top Bottom