samahani nimechelewa kuuona huu uzi, ila kwa sababu mimi nimepitia hii shida nimeona nikupe ushauri kidogo. Kwa maelezo yako kuwa unapata hedhi ni uthibitisho kuwa mayai unayo. Aliyetakiwa kupima wa kwanza ni Mwanaume. Kipimo cha mwanaume ni rahisi sana tena hakichukui muda umrefu, mwambie mmeo akapime sperm count (Uwingi wa mbegu kwenye manii yake) kama zitakutwa ok basi ndio waje kucheki mirija yako kama haijaziba kwa x-ray. nakuhakikishia hivyo vipimo viwili vikifanyika mwezi unaofuata unashika mimba. nimefanya mimi mwenyewe na kuwashauri jamaa zangu wawili nao wakapata mimba mwezi unaofuata. Tatizo naloliona ni kuwa wanaume wengi wabishi kwenda kupima, wanafikiri kwa kuwa wanatoa manii basi hawana shida, kiuhalisia hata ukiwauliza wataalamu wa afya ya uzazi, saa hizi tatizo la low sperm count ni kubwa sana hata wenyewe hawajui kwa nini ni kubwa hivi. Uzuri wake lina tiba ya asilimia 100.