Msaada: Kijana wangu anaongea vitu havieleweki, atakuwa na tatizo gani?

Msaada: Kijana wangu anaongea vitu havieleweki, atakuwa na tatizo gani?

Room 28

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2013
Posts
1,077
Reaction score
1,736
Nina kijana mwenye miaka 18 sasa hivi yupo form four, anasoma day yaani kwenda na kurudi nyumbani.

Changamoto yake si mtu wa kueleweka anapoongea. Anaweza ongea vitu viwili vinavyokinzana na bado yeye anaona yuko sawa. Kifupi yaani hawezi hata kuevaluate logic.

Mfano: umeenda shule
Yeye: Sijaenda kwa sababu sina hela ya shule.
Mzazi: Mbona hukuniambia
Yeye: weekend huwa hatuendi!

Yaani mambo ya mfumo huo. Visa ni vingi yaani hadi huwa nahisi labda ana shida fulani.

Huko nyuma alikuwa na tatizo la uongo, nilikuwa namtandika balaa, lakini tangu aingiae form 2 hadi sasa huwa simpigi kabisa.

Ni shida gan hii? Huwa najaribu kukaa nae kwa utulivu kujadili nae aseme kama kuna shida lakini anasema hamna, mbaya zaidi yeye hata ukimrudishia maelezo yake anaona hayana shida!

Je, hii ni kawaida wana saikolojia?
 
Aina nyingi za speech impairment ni psychological. Kwa mfano kama mtoto hajawahi kuwa huru kuongea, kila akifungua mdomo unamkosoa au kumkaripia jua unamsababishia kilema cha maisha. Itahitajika msaada wa mtaalamu wa saikolojia angalau kupunguza tatizo.

Na mbaya zaidi mtoto akigundua ana hilo tatizo na ikatokea wenzake wanantania shuleni basi anaweza hata kuanza kunywa pombe na kuvuta bangi ili ku cope na hayo mazingira magumu anayoishi.

Tupunguze ukoloni na vipigo kwa watoto. Yes usiwalee kizungu lakini ukatili kwenye mambo madogo madogo sio poa kabisa. Kulea mtoto sio chakula, mavazi na malazi pekee.
 
Kajiunga na CCM.maana ccm wanatumia sana watoto mwaka huu
 
Nina kijana mwenye miaka 18 sasa hivi yupo form four, anasoma day yaani kwenda na kurudi nyumbani.

Changamoto yake si mtu wa kueleweka anapoongea. Anaweza ongea vitu viwili vinavyokinzana na bado yeye anaona yuko sawa. Kifupi yaani hawezi hata kuevaluate logic.

Mfano: umeenda shule
Yeye: Sijaenda kwa sababu sina hela ya shule.
Mzazi: Mbona hukuniambia
Yeye: weekend huwa hatuendi!

Yaani mambo ya mfumo huo. Visa ni vingi yaani hadi huwa nahisi labda ana shida fulani.

Huko nyuma alikuwa na tatizo la uongo, nilikuwa namtandika balaa, lakini tangu aingiae form 2 hadi sasa huwa simpigi kabisa.

Ni shida gan hii? Huwa najaribu kukaa nae kwa utulivu kujadili nae aseme kama kuna shida lakini anasema hamna, mbaya zaidi yeye hata ukimrudishia maelezo yake anaona hayana shida!

Je, hii ni kawaida wana saikolojia?
Mwenye matatizo ya akili ni wewe. Hata mimi uje weekend uniulize kama nimeenda shule na unajua ni jpili, nitakujibu hovyo tu..
 
Back
Top Bottom