Nina kijana mwenye miaka 18 sasa hivi yupo form four, anasoma day yaani kwenda na kurudi nyumbani.
Changamoto yake si mtu wa kueleweka anapoongea. Anaweza ongea vitu viwili vinavyokinzana na bado yeye anaona yuko sawa. Kifupi yaani hawezi hata kuevaluate logic.
Mfano: umeenda shule
Yeye: Sijaenda kwa sababu sina hela ya shule.
Mzazi: Mbona hukuniambia
Yeye: weekend huwa hatuendi!
Yaani mambo ya mfumo huo. Visa ni vingi yaani hadi huwa nahisi labda ana shida fulani.
Huko nyuma alikuwa na tatizo la uongo, nilikuwa namtandika balaa, lakini tangu aingiae form 2 hadi sasa huwa simpigi kabisa.
Ni shida gan hii? Huwa najaribu kukaa nae kwa utulivu kujadili nae aseme kama kuna shida lakini anasema hamna, mbaya zaidi yeye hata ukimrudishia maelezo yake anaona hayana shida!
Je, hii ni kawaida wana saikolojia?