MSAADA KISAIKOLOJIA NINAANGAMIA

MSAADA KISAIKOLOJIA NINAANGAMIA

tafuta cha kufanya hata kama ni kufundisha na amini kuwa kinaweza kukupa kipato ili ukimbie mawazo ya starehe nenda hata kwa wanaouza chips wasaidie kumenya viazi bure wala usijari watakulipa nini au nenda hata kwa wanaolima bustani wasaidie hata kumwagia.
kwa kufanya hivyo utaulisha ubongo wako akili mpya na utawaza vizuri kuliko kuwaza udhaifu acha kujifungia.
 
Ndio mkuu yako fresh
Hakuna haja ya kuwaza kama uko fresh
Fanya yafuatayo

Mrudie muumba wako kwani yeye ndo mmiliki wa nafsi zetu

Isome Dini yako ya udumishe ibada ya swala (Juu ya hili nipo tayari kukufunza mkuu just njoo inbox)
 
Mkuu maliza hiyo dozi kama ulivoandikiwa. Baada ya hapo mkakati wako uwe ni kuacha kabisa punyeto. Kuacha punyeto ni kazi sana lkn nitakupa mbinu kadhaa zitakusaidia:
1.Weka malengo ya muda maalum. Mfano nataka nikae miezi mitatu bila kujaribu jambo hili
2. Usifungue tovuti au forums ambazo masuala ya ngono yanazungumziwa wala usisome hadithi au stori za kusisimua kingono (say no to erotic literatures)
3. Usiangalie picha zozote za uchi ama video. Hata kama sio za uchi lkn zenye vichupi zinazokusudia kusisimua kingono usiangalie.
4. Epuka kukaa upweke mahala pa siri kama chumbani kwasababu kufanya hivyo hupelekea mawazo ya ngono ambayo yatakufanya upige punyeto
5. Usilale sana baada ya kukucha asubuhi kwasababu mida hiyo ni prone kupiga punyeto kwakuwa wanaume asubuhi huwa tunaamka tukiwa na hamasa ya kutaka kusex
6. Tafuta hobby, na bora ya hobby ni Uchamungu. Acha dhimbi ya uzinzi acha nyeto, subiri ndoa mkuu
7. Anza kula vizuri na kufanya mazoezi maana it is likely utadevelop tatizo la premature ejaculation na weak erection. Utakapoona tatizo hili usistuke wala usiende kwa wazee wa dawa za nguvu za kiume, this problem will heal on its own over time. Time is the greatest healer of all time! Time heals everything. Inaweza kuchukua hata miaka 2 kupona tatizo hili kama utakuwa mvumilivu wa kutofanya ngono wala kupiga punyeto katika kipindi hicho.
8. Be honest to your soul. Kila la kheri bro.
Hahahaha miaka 2 bila ngono wala punyeto inahitaji uvumilivu wa kufa paka
 
MSAADA KISAIKOLOJIA NINAANGAMIA
Habari wakuu poleni na majukumu ya hapa na pale. Sijui hata nianzie wapi muweze kunielewa. Mimi ni kijana umri 26 muhitimu wa chuo kikuu kwa sasa nipo tu nyumbani sina ishu ya kufanya zaidi ya kulala tu ndani na kuishia kujilaumu sana kwa yaliyopita. Mnamo mwaka 2015 nilibahatika kupata mwenza kipind bado nasoma chuo ila kwa upande mwengine niliweza kuweka rehani maisha yangu kwani huyu mwenza wangu alikuwa anasumbulia na maradh ya ini pamoja na HIV. Sikupenda kumtenga nilijotoa kwa kila hari lakin mwisho wa siku niliambulia kibuti baada ya kuachana mwaka 2017 December ndipo nlipoingia kwenye matatizo makubwa sana kwani mitandao pia ilichangia kwa kiasi kikubwa sana kuniweka kwenye mawazo pale nilipokuja kugundua kwamba ugonjwa wa ini unaambukizwa hata kwa njia ya mate ndipo nlipokuwa na wasiwasi kila siku kwa kuhisi nimepata maambukizi lakini nilipopima mara mbili January na April sikuweza kukutwa na hayo maambukizi kwakweli bado nilikua na wasiwasi zaidi kwan kwa huu mwaka pekeyake nimepima HIV zaidi ya mara 10 lakini sikupata maambukizi. Kwa upande mwengine wa maisha yangu nkajikuta nimeingia kwenye mchezo mbaya sana ambao nimejitahidi sana kuacha lakin nashindwa mchezo wa PUNYETO kwani nimekuwa teja aliyekubuu. Hivi karibuni nilipata mwenzangu mwengine mnamo March 2018 turishiriki ngono kwa mara ya kwanza tangu nizaliwe nilijikuta nafanya oral sex na huyu binti mnamo April 2018 ntaanza kuona kama kuna mabadiriko kwenye kinywa changu pamoja na kuchoka mara kwa mara, tumbo kujaa gesi maumivu ya tumbo upande wa kulia karibu na mbavu, choo cheusi, tumbo kuunguruma, shingo kuuma kwa mbali katika hiyo hari nimefanya vipimo kama mkojo, choo kikubwa na full blood count lakini kwenye full blood count nimeenda hospital mbili tofauti wote wakidai nina bacteria infection na kuanza kutumia dawa za antibiotics lakn dariri ziko palepale huku nikiendelea na mchezo huu wa PUNYETO. Nikijaribu kugoogle nakutana na vitu ambavyo vinatisha mno nashindwa ambavyo ndivyo vimenipelekea mm kuwa mtu wa mawazo yasiyokuwa na mwisho. Ukigoogle utaambiwa cancer, ulcers, hepatitis, figo na magonjwa mengine makubwa makubwa kwakwel nateseka na msongo najihisi naumwa magonjwa yote haya kwani sina raha kabisa nimekuwa mtu wa kujifungia ndani na kujilaumu sana kwa niliyopitia. Naombeni ushauri wenu wa kuu kwan najiona kama nakufa kesho hivi
Pole sana kwa unayoyapitia na uliyoyapitia naweza kukushauri vitu vichache sana endapo utaviweza basi kuna uwezekano mkubwa sana wa kubadili mtazamo, kwanza acha kabisa kukaa peke yako usijifungie ndani peke yako hii itakusaidia kuacha kuwaza ngono muda wote, unapohisi kujisikia kufanya hivo jitahidi ubadili mazingira au tafuta shughuli ya haraka ya kufanya usiangalie picha zenye ushawishi mkubwa wa kupiga punyeto, unachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kujiweka bize na mambo ya msingi ya maisha only na kuamua sasa punyeto basi hata kama utaenda kwa wanasaikolojia usipoamua sasa basi huwezi kufanikiwa chochote kile, kuhusu maradhi hayo maradhi ni makubwa mno unayo yawaza mfano ugonjwa wa ini HEPATITIS B SURFACE ANTIGEN(HBsAG) ni ugonjwa unaoambukizwa kwa mate ndio na njia zote zinazoambukiza HIV ila HBsAG ina faida moja tuu kama una kinga zake za asili ambazo ni HEPATITIS B SURFACE ANTIBODY(HBsAB) ambazo ni kuanzia optical density 100milU/mL hapa sio rahisi kupata ugonjwa huo wa ini kumbuka kupima pia antibody ujue sababu za kutopata ugonjwa wa ini,
Madhara ya punyeto, haya yanafahamika ikiwemo kutopata hamu ya kusex na mwanamke, uume kusinyaa, kukosa nguvu za kufanya tendo, kuua cells za ku stimulate uzalishaji wa nguvu, kuvuruga saikolojia yako kila muda inawaza punyeto, kuhatarisha afya yako kwa ujumla na kuja kujutia maisha yako yote hata hupelekea mtu kujiua sababu ya kukwepa aibu utakapogundulika na matatizo ya uzazi nakushauri kwa sasa anza na kuamua SEMA NO KWA PUNYETO halafu lazimisha mawazo yako yasifikirie punyeto muda mwingi kwa sasa anza kufanya mazoezi muda mrefu na kula matunda na chakula ili kurudisha afya yako ikae sawa acha kuangalia picha za ngono ushauri wangu mdogo ni huo tuu kwa issue za vipimo niulize chochote kuhusu hepatits hiv n.k nitakufafanulia napokua na muda mzuri wa kutosha pia hata kupima kabisa
 
tumbo kujaa gesi maumivu ya tumbo upande wa kulia karibu na mbavu, choo cheusi, tumbo kuunguruma..

hizi ni dalili mojawapo za ulcers, nenda kafanye vipimo vya vidonda vya tumbo kisha ulete mrejesho hapa
 
Mtu wangu i want you to know that " YOU HAVE A REASON TO LIVE" ..ndio Just believe me!! Unasababu ya kuishi nalazima uishi.

Kwann unajaribu kujipa nyakati ngumu za kudhuru pumzi zako ilihali hukuwah kuchangia kuitengeneza hiyo Pumzi ???

SASA mie bana, huwa napenda kutoa maelekezo ....

Umewahi kaa na kuzungumza na Subconscious mind Yako??? Unailisha nini?? Umewah kaa na kufikiria juu ya fikira unazoilisha hii chemba??? ...

Sasa kuna kitu tunakiita " Power of Affirmation " , hii ninguvu yakuuambia Subconscious mind yako, kua unataka uweje na iweje ,chochote kile na kikawa vile unavyotaka.

Watu wanaofanikiwa kutumia hii nguvu, Huwa wanamaisha ya Furaha sana , kama mimi nilivyo , Ninafuraha mnoo kwakua mambo yangu yanaenda vile ambavyo nimeiambia chemba yangu yawe.

Sasa ufanye nin? .. Ongea na ubongo wako.

Kaaa chumban pakiwa kimya , fumba macho, kusanya hisia zako zaidi kisha sema maneno chanya tuuu unayotaka, sema " mimi ni mwenye afyaaaaa tele,, mimi nitaishi maisha marefuuu, mimi sitakua na matatizooo , mimi ni boraaa sanaaaa n.k n.k n.k , sasa nn faida yake??? Kufanya ivo mara kwa mara kuna uzoesha ubongo wako nahatimaye mawazo mbalimbali huja kukuonyesha nin , ufanye ili uwe unavyotaka.

, Ni usiku sana, Nachohimiza , kuhusiana nahizi dalili unazopata, Rudi hospital ,Nenda Hospital ya kueleweka kabisa , Haya mengine yote yalobaki nimepesi sanaa wala hayatokusumbua tena sio punyeto sio nn ...

NitakuPM
Ni moja ya comments nzuri sana kwa wenye kuelewa
 
Pole sana kwa unayoyapitia na uliyoyapitia naweza kukushauri vitu vichache sana endapo utaviweza basi kuna uwezekano mkubwa sana wa kubadili mtazamo, kwanza acha kabisa kukaa peke yako usijifungie ndani peke yako hii itakusaidia kuacha kuwaza ngono muda wote, unapohisi kujisikia kufanya hivo jitahidi ubadili mazingira au tafuta shughuli ya haraka ya kufanya usiangalie picha zenye ushawishi mkubwa wa kupiga punyeto, unachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kujiweka bize na mambo ya msingi ya maisha only na kuamua sasa punyeto basi hata kama utaenda kwa wanasaikolojia usipoamua sasa basi huwezi kufanikiwa chochote kile, kuhusu maradhi hayo maradhi ni makubwa mno unayo yawaza mfano ugonjwa wa ini HEPATITIS B SURFACE ANTIGEN(HBsAG) ni ugonjwa unaoambukizwa kwa mate ndio na njia zote zinazoambukiza HIV ila HBsAG ina faida moja tuu kama una kinga zake za asili ambazo ni HEPATITIS B SURFACE ANTIBODY(HBsAB) ambazo ni kuanzia optical density 100milU/mL hapa sio rahisi kupata ugonjwa huo wa ini kumbuka kupima pia antibody ujue sababu za kutopata ugonjwa wa ini,
Madhara ya punyeto, haya yanafahamika ikiwemo kutopata hamu ya kusex na mwanamke, uume kusinyaa, kukosa nguvu za kufanya tendo, kuua cells za ku stimulate uzalishaji wa nguvu, kuvuruga saikolojia yako kila muda inawaza punyeto, kuhatarisha afya yako kwa ujumla na kuja kujutia maisha yako yote hata hupelekea mtu kujiua sababu ya kukwepa aibu utakapogundulika na matatizo ya uzazi nakushauri kwa sasa anza na kuamua SEMA NO KWA PUNYETO halafu lazimisha mawazo yako yasifikirie punyeto muda mwingi kwa sasa anza kufanya mazoezi muda mrefu na kula matunda na chakula ili kurudisha afya yako ikae sawa acha kuangalia picha za ngono ushauri wangu mdogo ni huo tuu kwa issue za vipimo niulize chochote kuhusu hepatits hiv n.k nitakufafanulia napokua na muda mzuri wa kutosha pia hata kupima kabisa
Assante mkuu kwa ushauri wako ubarikiwe sana. Je uchukua muda gani kugundua virus vya hepatitis B? Kuna pia hepatitis A na C je hizi haziambukizwi kwa njia ya mate?
 
Hakuna haja ya kuwaza kama uko fresh
Fanya yafuatayo

Mrudie muumba wako kwani yeye ndo mmiliki wa nafsi zetu

Isome Dini yako ya udumishe ibada ya swala (Juu ya hili nipo tayari kukufunza mkuu just njoo inbox)
Sawa mkuu ntafanya hivyo
 
epuka kukaa peke yako muda mrefu maana wanasema Idle mind is the Devil's workshop mwisho wa siku utaishia kupiga punyeto tuu.

pia umesema umemaliza chuo na upo nyumbani tu, je hufikirii kutafuta kitu cha kufanya kujiingizia kipato? japo ni kweli sasa kuna changamoto mno za ajira, ila ukikaa tu ajira hazikufati nyumbani ndugu unatakiwa utoke kuzitafuta.
Assante sana kwa ushauri wako ubarikiwe
 
Hapo ndiyo ujue madhara ya dhambi jinsi inavyotesa japo mwanzo unapoitenda unasikia raha hata ukiambiwa usifanye unaona unaingiliwa maisha yako

Mshukuru Mungu kwa kukulinda dhidi ya maambukizi na uamue kutulia sasa maana inawezekana ukirudia tena ndiyo ikawa kwa heri

Usijipe stress na majibu ya google ambayo vipimo vimethibitisha hauna na iruhusu akili yako iamini u mzima maana kinachokusumbua ni kuamini majibu ya google na akili yako kuamini hivyo na inaweza kukufanya ukaumwa maana unaamini.

Nakutakia maisha mapya
Assante sana Mungu akubariki
 
Assante mkuu kwa ushauri wako ubarikiwe sana. Je uchukua muda gani kugundua virus vya hepatitis B? Kuna pia hepatitis A na C je hizi haziambukizwi kwa njia ya mate?
Hepatitis A (HAVAbIgM) hii huambukizwa kwa kula chakula chenye kinyesi toka kwa mtu mwenye maradhi hayo hii haiambukizwi kwa njia nyingine zaidi ya hiyo fecal oral route kwa kiswahili ni kula mavi kama ilivyo kipindupindu au amoeba na huu ni ugonjwa wa ini pia ila njia ya uambukizo ndio huo niliousema tuu.
Hepatitis C (HCV) huu ni ugonjwa wa zinaa unaambukizwa kwa njia zote zinazoambukiza ukimwi huu kwa kweli hauna tiba wala chanjo japo ni ugonjwa ambao upo kwa kiasi kidogo sana.
Hepatitis B (HBsAG) dalili zake huanza kuonekana kati ya siku 60 mpk 150 kwa average ya siku 90 tuu tangu uupate lakini ni vema ukaenda kupimwa ugonjwa hu una kinga ambayo ukichomwa unaweza usipatwe na ugonjwa huu kwa hiyo kwa muda ulioeleza ni sahihi hauna ugonjwa huu ila ulikua kwenye risk ya kuweza kuupata
 
Assante sana mkuu ubarikiwe zaidi Mungu akusimamie kazi zako
 
Mkuu kwani wewe ni mkaazi wa mikoa ya shinyanga, mwanza, geita n.k? Samahani lakini
 
Assante sana mkuu ubarikiwe zaidi Mungu akusimamie kazi zako
Kuhusu choo, kuumwa tumbo, kujaa gesi na kuunguruma wewe una mawazo mengi inaonekana yanakusumbua kama unawaza mpk ukahisi maumivu ya tumbo na hupati chakula vizuri kwa muda na hauli kabisa unaweza kupata vidonda vya tumbo nakushauri nenda hospital omba upimwe vidonda vya tumbo(h.pylor) waambie wakupime H.PYLOR STOOL ANTIGEN hapa watatumia choo kupima usitumie damu(H.PYLOR SERUM ANTIBODY) tumia ya choo ndio utapata majibu ya uhakika kwamba una ulcers au hauna ya damu huweza kuonesha hata kama ulishawahi kuumwa zaman inaweza sema unae bado ok do it change now
 
Sawa mkuu nashukuru sana
 
Mkuu kweli unamoyo wa ukweli sana,ulijua kabisa girl wako anaukimwi still ulikuwepo,dah
 
Mkuu kweli unamoyo wa ukweli sana,ulijua kabisa girl wako anaukimwi still ulikuwepo,dah
That was a big mistake I made, that is why najutuia kila wakati but kumbuka pia no one knows tomorrow so tusiwatenge
 
Back
Top Bottom