Msaada kuhusu gharama za fundi kujenga nyumba ya vyumba vitatu kuanzia msingi hadi kwenye beam

Usimsikilize huyu, yeye ni kampuni na anao wateja wakeโ€ฆ. sisi huku msingi laki 3, boma laki 5, kuezeka laki 4, plasta laki 3.

Kikubwa uhai tu.
Ni pm bwana ncha Kali tuyajenge
 
Mmi kuna fundi tumekubaliana 3M ujenzi niko Dom. Kanilalia au fair?
Fair kabisa fundi mzuri anye jua kujenga kwa vipimo mara nyingi wapo kwenye makampuni kama Estim n.k ili kumtoa aje akujengee ni gharama maanq wao wana fuata kanuni zote za ujenz nyumba kila mtu ana itamani
 
Kiufupi jitahidi gharama za ufundi zisizidi 15% mpaka 20% ya gharama za material. Ukishapiga hesabu zako za material ktk hatua flani ya ujenzi, tafuta hiyo asilimia ili wakati unabargain na fundi wako ujue unamvutaje ajae kwenye hiyo range. Kuna mafundi wengine ni wazuri sana ila hesabu zinawasumbua, ukimpa ramani anaingalia weeee, lakini akija kutaja bei unakuta amejitoa mwenyewe kwenye range (<15%) na bado hamjabargain
 
Mimi nakumbuka fundi nilimpatia sh 2.5 hivi na maposho posho kimtindo
 
Mkuu nipe namba ya fundi wako

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
NI TANZANIA PEKEE AMBAPO SISI MAFUNDI UJENZI HATUTHAMINIKI.
Sasa mnataka mthaminiwe kwa lipi la maana mnalolifanya?
Mnashindwa hata namna ya kunadi fani zenu? Mngekua na tabia ya kutenga muda kwa ajili kuelimisha watu umuhimu wa kujenga kutumia mafundi ili jamii ihamasike hapo mngethaminika.
Kama hapa, badala ya kutumia fursa ya kutoa elimu na kujitangaza, wewe unaleta malalamiko.
Mkipewa kazi, badala ya kuifanya kwa uaminifu, either mnaanza udokozi au mnajenga chini ya viwango. Mkikutana wala hamuonyana wala kukemeana kwa tabia hizo za hovyo, badala yake mnapeana mbinu zaidi za kufanya wizi.
Kama nyumba zingekua zinafyatuliwa viwandani, hakuna ambaye angehangaika na mafundi.
 
Usimsikilize huyu, yeye ni kampuni na anao wateja wakeโ€ฆ. sisi huku msingi laki 3, boma laki 5, kuezeka laki 4, plasta laki 3.

Kikubwa uhai tu.
๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ