Msaada kuhusu kusafirisha parcel kutoka Marekani

Msaada kuhusu kusafirisha parcel kutoka Marekani

GIRITA

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2016
Posts
4,432
Reaction score
5,864
Salaam wakuu.

Naomba kusaidiwa na yeyote humu ambaye ni mzoefu wa kusafirisha percel kutoka Marekani kuja Tanzania, kwa kutumia makampuni kama DHL na mengineyo hasa napenda kufahamu gharama za kusafirisha simu, ziko mbili kutoka Ohio Cleaveland kuja Tanzania ina gharimu kiasi gani KWA uzoefu wako wa kusafirisha mizigo.

Pili, je unaweza kusafirisha Document bahasha Moja yenye karatasi 10, ukaichanganya na hizo simu 2 zikaja KWA pamoja?

Nauliza hivi maana wiki iliyopita nimetuma document huko huko zimefika jana, gharama tuliyotumia ni sh 138,000 KWA kutumia DHL...sasa nashangaa mtu niliyemtumia anasema eti kutuma hizo simu 2 KWA DHL ni dola 200! Na haiwezekani kutuma document na simu pamoja.

Naomba msaada KWA yeyote anayejua maana hata tulivyotuma document baada ya kuingiza data za mzigo kwenye system ya DHL walituonyesha bei sasa wewe ndio unachagua rahisi kwako...nashangaa hiyo dola 200 ni kweli kwa simu mbili?
 
Iyo mtu yupo sahihi sio chini $100 dhl unaletewa mpk kijijini kwenu
Yupo sahihi kiaje na wewe umesema sio chini ya dola 100?
Nipe bei kamili ya uhakika maana yeye kasema simu 2 gharama ni 200$.
 
Wakuu ufanunuzi Tafadhali.
 
Andaa $105 Alf tegemea network lock kweny hizo simu
Simu nyingi za marekani hazisomi mitandao Africa
USPS should be much less than that, ila ndiyo mzigo unatumwa Posta ya Tanzana.

Mimi nilimtumia mtu box kubwa la vifaa vya muziki nililipa $140.

Box hilo uzito na ukubwa ni angalau mara 20 ya simu mbili.

USPS kila kitu wameweka mtandaoni, kuna mpaka calculator ya gharama za mzigo kwenda Tanzania kwa uzito na dmensions za box.

Soma hapa

Pia, unaweza kwenda Posta ya karibu Marekani (USPS) watakupimia mzigo na kukuambia gharama.
 
Ahsante mkuu,kuhusu muda wa mzigo kukufikia inachukua muda gani?
 
USPS should be much less than that, ila ndiyo mzigo unatumwa Posta ya Tanzana.

Mimi nilimtumia mtu box kubwa la vifaa vya muziki nililipa $140.

Box hilo uzito na ukubwa ni angalau mara 20 ya simu mbili.

USPS kila kitu wameweka mtandaoni, kuna mpaka calculator ya gharama za mzigo kwenda Tanzania kwa uzito na dmensions za box.

Soma hapa

Pia, unaweza kwenda Posta ya karibu Marekani (USPS) watakupimia mzigo na kukuambia gharama.
Ni kweli kwamba simu zote za US ni network locked?
Kama asemavyo jamaa hapo juu?
 
Kama unasafirisha simu tena 2 hiyo gharama ni sawa kabisa, wanapiga uzito plus restrictions za kusafirisha hazardous goods. Simu moja inaweza kuwa na gram 240 mfano 14 pro max, So hapo pamoja na box weka gram 500 tu.
Ukichanganya na hizo karatasi bado itakuwa vile vile tu kwakuwa msafirishaji lazima ataje product anayosafirisha.
 
Back
Top Bottom