Msaada kuhusu mbegu za nyanya

Msaada kuhusu mbegu za nyanya

Assila f1 kuna baadhi ya wakulima wanadai ukianza kuvuna unavuna miezi 6.ukweli ni upi?
Nikweli unavuna miezi hiyo ila ni mpaka uifunge kwa kamba zaidi ya mara mbili na inategemeana na aridhi ya eneo husika na huduma pia uendelee kuihudumia hapo utafikisha hiyo miezi kuivuna
 
Kwanini matuta umeyainua sana na ni membamba? Je kila tuta utapanda mistari mingapi? Utatumia njia gani kumwagilia?
Mkuu ninavyo virusha maji sprinklers...huwa navitumia na muda mwingine namwagilizia mche hadi mche kwa mkono.
 
Yawezekana ni tuta absoluta au kiswahili waitwa kantangaze ambaye ni vigumu sana kumuua na anazoea sumu haraka. Inabidi upige dawa za kuulia wadudu kila mara aina tofauti
Asante mkuu...hivi kuna tofauti gani kati ya mbegu ndefu na mbegu fupi ya nyanya....?
 
Ungefanya hayo matuta upana kuwa sentimeta 30 ungeweza otesha mistari miwili kwa tuta
Mkuu kipindi naandaa shamba sikuwa kabisa na utaalam nilinunua mbegu nyingi kuliko ukubwa wa eneo...eneo lilikuwa dogo sana...ndio maana unaona hivyo ila nadhani muda mwingine nitafanya vizuri zaidi
 
Katika kilimo asilimia 10 ya gharama ni mbegu na asilimia 90 ni huduma ,ukiweka mbegu ya kubahatisha remember 90 percent iko pale pale utakua unaanda hasara so ni bora usifanye bahati nasibu wewe chukua mbegu bora panda na hudumia vyema ,hope umenielewa
Mkuu naomba msaada baadhi ya miche yangu yA nyanya imekumbwa na hali ya majani ya juu kujikunja ama kusinyaa....kuna mmoja nimeukuta umesinyaa kabisa kama umeungua hivi...ili ni tatizo gani¿ nitañitatuaje?
 

Attachments

  • Screenshot_20170510-202225.png
    Screenshot_20170510-202225.png
    287.2 KB · Views: 104
Semi maana yake iko katikati ya nyanya fupi (determinate) na nyanya ndefu (indeterminate) so hizi semi hazizidi urefu wa mita 2 na hatutolei matawi (suckers)
Mkuu kwanini baadhi ya mbegu hutolewa matawi na baadhi hazitolewi?
 
Mkuu kwanini baadhi ya mbegu hutolewa matawi na baadhi hazitolewi?
Zinazotolewa matawi ni nyanya fupi ambazo hurefu hazizidi mita 1.5 sasa kwa matunda huzaliwa kila baada ya cm15 au 20 (std) hivyo ukitoa matawi kwa mche wa kurefuka 1.5m inamaana itakua na vichane 6 tu ,ukiacha matawi inamaana kila tawi likikua vichane 6 ikiwa matawi manne tu unachane roughly 24,kila kichane kikiwa na matunda manne hapo ni matunda 96 (kg 12 roughly per plant)
Kwa nyanya ndefu inakua tu haina mwisho hivyo utavuna mpaka useme basi maana inafika mpaka mita 8 .
Kwahiyo mwenye nyanya fupi akitoa matawi kapunguza mavuno ila mwenye nyanya ndefu anatoa matawi abakiwe na moja au mawili atakayoeza kuyahudumia vyema .

Nyanya fupi inaitwa fupi sababu kuna urefu ikifika inaweka matunda ya mwisho
 
Back
Top Bottom