Msaada kuhusu mbegu za nyanya

Msaada kuhusu mbegu za nyanya

Booster gani itafaa ndugu
Ndugu bado mpya sana kwenye kilimo ,achana na booster hiyo ni sawa na glucose kwa mwanadamu ,je unaweza ishi kwa kutegemea glucose !!????
Tumia manual ya uzalishaji wa nyanya nimeituma kwenye hii page ina madawa na ina mbolea gani uweke kwa kila shina na kiasi gani ,sasa kuongelea one thing muda wote nashindwa ndugu yangu ,fuata manual then niulize swali toka kwenye manual sababu manual haina sehemu imetaja upige booster .
Sasa kama kufuata manual inakua vigumu hapo nashindwa kukusaidia rafiki yangu
 
706f06dfe5a9561ab96ef3840bce9194.jpg
hapo nimekuta mmea umeishiwa nguvu kabisa....kuushika shina nimelikuta limeoza...dah....
Vipi shina lina harufu kama ya yai viza !? Vipi mizizi imevimba vimba mwanundu manundu !?
 
0b6271727afeb2b6cc8fe8037eac64b4.jpg
mkuu naomba mnisaidie mbegu yangu hii inakuwa kama yanjano sijawahi kuipa mbolea zaidi ya sumu tu je nifanyeje iwe kijani pia yenye afya naikue haraka
 
0b6271727afeb2b6cc8fe8037eac64b4.jpg
mkuu naomba mnisaidie mbegu yangu hii inakuwa kama yanjano sijawahi kuipa mbolea zaidi ya sumu tu je nifanyeje iwe kijani pia yenye afya naikue haraka
Tafuta mbolea ya Can au NPK au weka mbole za wanyama ng'ombe au ya kuku ila hakikiha iwe mbolea kavu ukiweka mbolea mbichi....itakufanyia kitu kibaya hutokisahau
 
Vipi shina lina harufu kama ya yai viza !? Vipi mizizi imevimba vimba mwanundu manundu !?
Harifu inakaribia...ila sio kari sana...then inatoa maji....ni miche miche ila nakuja kushituka ukisha nyauka....nadhani inashambulia haraka sana...sijui ni nini hiko
 
usihofu ndugu yangu...nitakusumbua hadi unichoke....si unajua kwenye kilimo mimi bado mgeni kabisa...

Wanatafiti na kuuza hawana uhakika na mbegu zao(RIjwan),swali la mleta mada limejibiwa na wana nadharia,au wauza mbegu.

Uhalisia ni huu,kama mbegu zilizo shambani ni hybrid majibu yaliyotolewa ni sahihi lakini kama mbegu ulizo nazo ni OPV majibu uliyopewa si ya kweli unaweza kurudia mbegu na zikakupa tija kwa zaidi ya 90%.

Kwa OPV mbegu nzuri zaidi ni mwanga,tengeru(japo wanunuzi wanasumbua kipindi cha uzalishaji mkubwa),Kiboko na Meru.

Mbegu bora zaidi kwa uzalishaji ni hybrid,wengi huzikimbia kwa ukubwa wa gharama zake.Hybrid za nyanya zipo aina nyingi na zinazalishwa na kampuni tofauti.

Kwa uzoefu wangu mbegu bora zaidi kwa sasa (TZ) za hybrid ni Monica,Ashanti na Eden. Zinafuatiwa kwa karibu na kipato,milele na nuru.Kigezo changu cha ubora ni ukubwa na kuvutia walaji kwa tunda husika na ustahimilivu sokoni.

Kwa tija zaidi wasiliana na wakulima usihangaike na wataalam wa nadharia Ofisini au wauzaji wa mbegu,watakupoteza,
 
Asante mkuu..hawa wauzaji wa mbegu ya eden ni kampuni gani...naiona imetajwa sana na wengi
 
Wadau wenzangu nipeni wasifu izi mbegu za nyanya eden-f1.assila-f1.shanty-f1
Kwanza zote ni hybrid

Pili assila inafanya vizuri wakati wa kiangazi

Tatu eden na shanty ziko vizuri kipindi cha mvua!!

Nne zote unaweza lima kwenye open space ... Shambani!
 
Miche inakupa uhakika wa kua nao ya kutosha eneo lote ila mbegu ni fifty fifty kama kuna michache isipoota au ikifa kwa magonjwa ya kwenye kitalu ,inapaswa uwe makini kwenye kutunza miche lakini hakikisha unanunua kwenye source makini
Mkuu nna swali hapa!

Assila f1 ni semi determined au??

Assila naweza lima kipindi cha mvua??
 
db028d5b5dd3bb8b165205e8bd615e51.jpg
ec168da5678cb23591d78839d172decf.jpg
7ba068f238f09cdda9410e3b4fe100da.jpg

Msaada Wadau bamia zangu zimepatwa nanini kutoka namuonekano huo niasaidieni kutatua hali hiyo nifanyeje
 
Ni mbegu ipi inayorefuka hadi mita nane ili iwe chaguo langu, halafu kilimo chagreen house lazima umwagiliaji uwe wa droplets? Maaada jamani
 
Habari zenu wadau mbona mmenyamaza naombenu mnisaidie hapo juu kuhusu greenhouse
 
Ni mbegu ipi inayorefuka hadi mita nane ili iwe chaguo langu, halafu kilimo chagreen house lazima umwagiliaji uwe wa droplets? Maaada jamani
Zipo....mbegu nyingi kama Eden f1 na nyinginezo...unaweza kuonana na wataalam wa mbegu...BALTON... kama upo dar...
Umwagiliaji wa matone ndio uliopendekezwa zaidi kwani hauruhusu kuenea kwa magonjwa yanayosafirishwa kutokana na kutiririka kwa maji...hivyo ukimwagia kwa matone uhakika wa kukuza niche yote kwa 92%
 
Back
Top Bottom