Msaada kuhusu toyota Passo

Msaada kuhusu toyota Passo

mutu murefu

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2017
Posts
996
Reaction score
2,636
Habari za muda huu wakuu.
Mimi ni kijana wa miaka 24, katika mishemishe za maisha nimefanikiwa kukusanya kiasi fulani cha pesa.

Nina mpango wa kununua gari ndogo isiokula mafuta(maana mi ni mtu wa mishemishe mjini inakua shida bila usafiri). Nimepata wazo ninunue toyota passo. Kilichonivutia hasa ni CC yake ndogo (ninayodhani inakula mafuta kidogo) hivyo nitaweza kutumia pesa kidogo huku niki save pesa nyingine kwenye ujenzi wa nyumba na mambo mengine. Nataka kwa matumizi madogo tu ya mishemishe za kazini na mjini (sina safari ndefu).

Ninaomba wale wenye uzoefu na ujuzi wa hii gari wanieleweshe zaidi maana ninajua na kutambua kuwa JF ni zaidi ya shule.
Naomba kujuzwa mambo haya
- ulaji mafuta
- kudumu kwake
- comfortability
- upatikanaji wa spea zake

Naomba michango ya kujenga sio kejeli na matusi.

[HASHTAG]#Mutu[/HASHTAG] murefu
 
Ni bora ukachukua Vitz itakufaa zaidi tofauti na Passo si gari imara hasa body pamoja na injini yake
 
Habari za muda huu wakuu.
Mimi ni kijana wa miaka 24, katika mishemishe za maisha nimefanikiwa kukusanya kiasi fulani cha pesa.

Nina mpango wa kununua gari ndogo isiokula mafuta(maana mi ni mtu wa mishemishe mjini inakua shida bila usafiri). Nimepata wazo ninunue toyota passo. Kilichonivutia hasa ni CC yake ndogo (ninayodhani inakula mafuta kidogo) hivyo nitaweza kutumia pesa kidogo huku niki save pesa nyingine kwenye ujenzi wa nyumba na mambo mengine. Nataka kwa matumizi madogo tu ya mishemishe za kazini na mjini (sina safari ndefu).

Ninaomba wale wenye uzoefu na ujuzi wa hii gari wanieleweshe zaidi maana ninajua na kutambua kuwa JF ni zaidi ya shule.
Naomba kujuzwa mambo haya
- ulaji mafuta
- kudumu kwake
- comfortability
- upatikanaji wa spea zake

Naomba michango ya kujenga sio kejeli na matusi.

[HASHTAG]#Mutu[/HASHTAG] murefu
Kwenye swali lako la kwanza na la mwisho sio issue sana ila hayo mawili ya kati unapozungumzia comfortability kwani mjini unataka upambane na nani mpaka uitaji gari nzito ila yote kwa yote tafuta bajaj hutojutia hivyo vigari kila siku utakuja kuomba ushauri ni mimba iliyokosa baba.
 
Hahaha asante sana mkuu kwa ushauri wako
 
Jiandae kisaikolojia mkuu,hako kagari"passo" ukikawasha hua kanatetemeka balaa mpk unasikia mwili wote unawasha ila kakishaanza kuondoka ile kutetemeka inaisha mkuu.
 
Usije kununua passo utakuja kujuta, passo sio gari imara kwenye engine
 
Jiandae kisaikolojia mkuu,hako kagari"passo" ukikawasha hua kanatetemeka balaa mpk unasikia mwili wote unawasha ila kakishaanza kuondoka ile kutetemeka inaisha mkuu.
Ahahahahahahahahah we jamaa
 
Kwenye swali lako la kwanza na la mwisho sio issue sana ila hayo mawili ya kati unapozungumzia comfortability kwani mjini unataka upambane na nani mpaka uitaji gari nzito ila yote kwa yote tafuta bajaj hutojutia hivyo vigari kila siku utakuja kuomba ushauri ni mimba iliyokosa baba.
Du kumbe bajaji nayo ni gari!!
 
Back
Top Bottom