Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Za kwako mzee! Kama unahitaji kusafiriaha kwa meli kuna jamaa mmoja Yuko poa sana anakaa North Carolina anaitwa Haji ukihitaji info ntakupatia. From what I know ana container linaondoka April 25 kama sijakosea
Karibuni..siku za nyuma posta walikuwa wame base sana kwenye kuuza stamps..mapato ya simu..nafikiri unakumbuka kipindi kile unapotaka kupiga simu lazima uombe kwa operator na usubiri saa nzima kuunganishwa..pamoja na bank yao ndio yalikuwa mapato yao makubwa..lakini siku hizi baada ya hizo biashara kushuka wameboresha sana huduma ya kusafirisha na kupokea mizigo (parcel)binafsi ni mwaka wa 8 naitumia kutoka hapa dubai kutuma Tz..hakuna tatizo..mwambie anayekutumia aandike pia namba yako ya simu pia akupe tracking number ambayo itakusaidia...wana njia ya express toka dubai to tanzania siku 3 pia wana njia ya kawaida wiki 2..karibuni sana..posta wapo duniani kote
Kama ujuavyo flat screen ni uzito mdogo tu 10kg..inakwenda vizuri sana kwa posta hasa ikiwa mpya ni salama zaidi maana inakuwa kwenye box lenye usalama mzuri...itafika vizuri sana bila matatizo na tax yake ni ndogo
Kwa vitu vizito kama hivyo meli ndio njia nzuri zaidi maana ni cheap na hata kodi yake haitakusumbua..japo sijajua ukubwa wa hizo frigdes na ni ngapi mpya au used zina lita ngapi nk..moving camers na home theatre zinatumika vizuri ata kwa posta(binafsi nimekwishatuma)ushuru ulikuwa laki 1.2 kwa vyote viwili...njia nyingine ni kwa ndege lakini ni expensive ktk kutuma na ata mzigo ukifika pale airport TRA watajua una pesa..nadhani kitachendelea unajua ni niniMkuu.. waongeje kuhusu bei na kodi ya eclectronics zingine kama home theaters..refrigerators ..still and moving Cameras.. high specs computers.. handheld gps n.k?
Ndugu asante,ila naomba kujua jambo moja,hv hawa ems wapo dunia nzima au?na je wana link na posta?
Wadau naombeni msaada kwa wale watu wanaojua kampuni zinazosafirisha vifurushi toka USA kuja Tanzania mbali ya USPS,FEDEX na DHL anisaidie kujua ikiwezekana na mawasiliano yao!asanteni