Msaada: Kusafirisha vitu toka U.s.a

Msaada: Kusafirisha vitu toka U.s.a

Kapuku83

Senior Member
Joined
Sep 8, 2012
Posts
146
Reaction score
35
Wadau naombeni msaada kwa wale watu wanaojua kampuni zinazosafirisha vifurushi toka USA kuja Tanzania mbali ya USPS,FEDEX na DHL anisaidie kujua ikiwezekana na mawasiliano yao!asanteni
 
Za kwako mzee! Kama unahitaji kusafiriaha kwa meli kuna jamaa mmoja Yuko poa sana anakaa North Carolina anaitwa Haji ukihitaji info ntakupatia. From what I know ana container linaondoka April 25 kama sijakosea
 
Mkuu naomba nipatie info/contacts zake mkuu!
 
Wala huitaji kujua mtu wala kutafuta contact za mtu..kama mzigo una kilo zisizopungua 35 mwambie aende posta..kuna posta kila mtaa na bei ni ndogo sana ndani ya siku 15 mzigo utakuwa tanzania..nimetumia njia hii kwa zaidi ya miaka 8 ni nzuri sana..kama mzigo ni mkubwa sana weka wazi
 
USPS posta ni kujitupa kwenye mikono ya ukiritimba. Pili air cargo is very expensive always.
 
Mm kuna m2 yupo Sweden anataka kunitumia tv flat screen 32inch,kupitia posta je ushuru inaweza fika bei gan.??
 
Kwa system ya posta ushuru utatakiwa kulipia huku kule utalipia sending charges tu..uzuri ni kwamba kila mtaa kuna huduma ya posta..kwa kilo kumi wawezatumia ata dhl japo huitaki..siku hizi posta mambo yote yapo wazi mtumaji atakupatia namba itayokuwezesha ku trace mzigo wako kama ilivyo dhl..ata ulipaji wa kodi si mkubwa
 
Poa poa vp je ushuru wa tv flat screen inch32 ni mkubwa au!?
 
Mi natuma saana flat screen toka hapa dubai..juzi nilituma mbili ushuru walianza laki na nusu baadaye nikawapa elfu 95 kwa mbili..ila ukituma kwa bandarini utakuwa juu kidogo
 
Nisaidie flat screen yako ulituma kwa njia ya post pia kweli?
 
Kama ujuavyo flat screen ni uzito mdogo tu 10kg..inakwenda vizuri sana kwa posta hasa ikiwa mpya ni salama zaidi maana inakuwa kwenye box lenye usalama mzuri...itafika vizuri sana bila matatizo na tax yake ni ndogo
 
Poa kaka na shukuru kwa ushauri wako mana nilikuwa na hofia nilishawai kutumiwa vifaa vya c2dio walini sumbua sana pale posta.
 
Asante Kapuku83 kwa kuleta post hii na wakuu wengine,maana nami nimepata mwanga juu ya mambo yaliyokua yakinitatiza
 
Karibuni..siku za nyuma posta walikuwa wame base sana kwenye kuuza stamps..mapato ya simu..nafikiri unakumbuka kipindi kile unapotaka kupiga simu lazima uombe kwa operator na usubiri saa nzima kuunganishwa..pamoja na bank yao ndio yalikuwa mapato yao makubwa..lakini siku hizi baada ya hizo biashara kushuka wameboresha sana huduma ya kusafirisha na kupokea mizigo (parcel)binafsi ni mwaka wa 8 naitumia kutoka hapa dubai kutuma Tz..hakuna tatizo..mwambie anayekutumia aandike pia namba yako ya simu pia akupe tracking number ambayo itakusaidia...wana njia ya express toka dubai to tanzania siku 3 pia wana njia ya kawaida wiki 2..karibuni sana..posta wapo duniani kote
 
Ndugu asante,ila naomba kujua jambo moja,hv hawa ems wapo dunia nzima au?na je wana link na posta?
 
Kama ujuavyo flat screen ni uzito mdogo tu 10kg..inakwenda vizuri sana kwa posta hasa ikiwa mpya ni salama zaidi maana inakuwa kwenye box lenye usalama mzuri...itafika vizuri sana bila matatizo na tax yake ni ndogo

Mkuu.. waongeje kuhusu bei na kodi ya eclectronics zingine kama home theaters..refrigerators ..still and moving Cameras.. high specs computers.. handheld gps n.k?
 
Mkuu.. waongeje kuhusu bei na kodi ya eclectronics zingine kama home theaters..refrigerators ..still and moving Cameras.. high specs computers.. handheld gps n.k?
Kwa vitu vizito kama hivyo meli ndio njia nzuri zaidi maana ni cheap na hata kodi yake haitakusumbua..japo sijajua ukubwa wa hizo frigdes na ni ngapi mpya au used zina lita ngapi nk..moving camers na home theatre zinatumika vizuri ata kwa posta(binafsi nimekwishatuma)ushuru ulikuwa laki 1.2 kwa vyote viwili...njia nyingine ni kwa ndege lakini ni expensive ktk kutuma na ata mzigo ukifika pale airport TRA watajua una pesa..nadhani kitachendelea unajua ni nini
 
Ndugu asante,ila naomba kujua jambo moja,hv hawa ems wapo dunia nzima au?na je wana link na posta?

Wapo dunia nzima ila hii ni kitengo cha vifurushi au docs zinazosafirishwa haraka zaidi...Express mail Service (EMS)ni kitengo pale posta
 
Back
Top Bottom