Msaada kwa Godzilla, ana hali mbaya

Msaada kwa Godzilla, ana hali mbaya

Daaaaaaa kweli mkuuu
Binadam mkijuana huwa kuna mawili kati ya haya hutokea kushuka thamani sana au kupanda thamani kutokana na utakayoyakuta kwa mwenzako hapo ndio upendo wa kweli unadhihilika wengi huwa wanashindwa pale unapojua mwanaume uliyemtamani siku zote ni 5mns au mwanamke uliyempenda sana kumbe ni mwenye roho ya hatari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TAARIFA RASMI ZA MSIBA WA GODZILLA (Golden Jacob Mbunda) KIFO: (Kutoka kwa Familia) Godzilla aliugua ghafla majuzi kwa kulalamika anaumwa tumbo na kutapika. Alienda kwenye Zahanati ya jirani na kwao, akagundulika ana Malaria. Wakati ameanza matibabu aliendelea kutapika, na kutokula vizuri, hii ikachangia Sukari kupanda na BP kushuka. Mnamo juzi usiku hali ilibadilika ghafla na wanafamilia wakamkimbiza hospitali ya Lugalo, ambapo ndio alifariki. MSIBA: Msiba upo nyumbani kwao na marehemu, Salasala, karibu na Shule ya Sekondari ya Green Acres. Sio mbali kutoka kituo cha Mbezi Africana. UTARATIBU WA MAZISHI: Wanasubiriwa Ndugu kutoka Mwanza (Kaka wa Marehemu) na ndugu wengine kutoka Songea, na pia kukamilisha Mipango ya kuendesha msiba. Matarajio ni kwa Mazishi kufanyika Siku ya Jumamosi katika Makaburi ya Kinondoni, Dar Es Salaam. Utaratibu wa kuaga Mwili na Misa utatolewa muda muafaka ukiwadia baada ya taratibu husika kutimia. RAMBI RAMBI: . . Michango yote ya Wasanii kutoka kwenye ma-group ya Wasanii inapokelewa na @soggydoggyanter 0754772220 (Anselm Ngaiza), ambayo inajumuisha Hip Hop Community, Umoja Wa Wasanii, Tanzania Urban Music Association (TUMA), nk. Marafiki wa Zillah katika Social Media (Twitter, Instagram, Facebook) wanaweza kutuma mchango kwa namba hizi TIGOPESA 0659421111 Mansour Rashid @papichulo_chuly 0717367673 Webiro Wasira @wakazimusic MPESA . . 0745368485 Webiro Wasira 0769991190 Prince Kessy @esilovey1 Ila kama kuna mtu anataka kutuma mchango peke yake, basi anaruhusiwa kufanya hivyo kupitia Namba ya Mama Mzazi Wa Marehemu. MARY CHARLES MBUNDA 0652810084 KING ZILLAH ALIISHI KAMA MFALME... HEBU TUMPE HESHIMA YA MWISHO NA KUMLAZA KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE KAMA MFALME PIA "Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe" #RIP #ZiZi #KingZillah UKITUMA HELA TUMA NA MSG
 
Sijapost R.I.P Zilla kwa sababu sijawahi kupost ngoma yake, sijawahi kumuwish birthday, hakuwa rafiki yangu ingawa alikuwa msanii mwenzangu, kwanini leo itokee amefariki ndio nipost R.I. P !? Roho inanisuta”. - Ameyasema hayo Christian Bella.
 
MSTAAFU RAISI JAKAYA KIKWETE : >>>Nimestushwa na taarifa za kifo cha msanii wa kizazi kipya GodZila. Alikuwa kijana mdogo mwenye ndoto kubwa na ameondoka wakati ambapo bado mchango wake ulihitajika. Nawapa pole familia ya Marehemu na wasanii wote kwa msiba huu. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema.
 
Sijapost R.I.P Zilla kwa sababu sijawahi kupost ngoma yake, sijawahi kumuwish birthday, hakuwa rafiki yangu ingawa alikuwa msanii mwenzangu, kwanini leo itokee amefariki ndio nipost R.I. P !? Roho inanisuta”. - Ameyasema hayo Christian Bella.
Achana na Akili za Wacongo, akili zao Alizikwa nazo Patrice Lumumba. Watanzania tutabaki na ukarimu wetu daima
 
Back
Top Bottom