Msaada kwa Godzilla, ana hali mbaya

Msaada kwa Godzilla, ana hali mbaya

TAARIFA RASMI ZA MSIBA WA GODZILLA (Golden Jacob Mbunda) KIFO: (Kutoka kwa Familia) Godzilla aliugua ghafla majuzi kwa kulalamika anaumwa tumbo na kutapika. Alienda kwenye Zahanati ya jirani na kwao, akagundulika ana Malaria. Wakati ameanza matibabu aliendelea kutapika, na kutokula vizuri, hii ikachangia Sukari kupanda na BP kushuka. Mnamo juzi usiku hali ilibadilika ghafla na wanafamilia wakamkimbiza hospitali ya Lugalo, ambapo ndio alifariki

Kwenye Bold mnazidi kutuchanganya...kwa mujibu wa dada yake Zilla anasema jamaa kafia nyumbani tena mikononi mwa huyo dada yake...."Mama akaniambia mdogo ako anakuita kabla sijaenda chumbani kwake yeye akawahi kutoka akaja kwangu nikamuuliza vipi akasema naomba tu nilale pembeni yako,naona kuna watu wengi sana wanaizunguka nyumba wanataka kunichukua,ghafla Zilla akawa anataka kutoka nje,mimi na Mama tukamshika tukimwambia lala hapa kwanza upumzike,basi akalala kama mtu alieishiwa nguvu ndo ikawa moja kwa moja hakuamka tena alifia mikononi mwangu tukampeleka lugalo akiwa tayari ashakufa'' mwisho wa Kunukuu
 
Mkuu amini nukuu yako na kile unachokiamini vingine potezea

Sijapost R.I.P Zilla kwa sababu sijawahi kupost ngoma yake, sijawahi kumuwish birthday, hakuwa rafiki yangu ingawa alikuwa msanii mwenzangu, kwanini leo itokee amefariki ndio nipost R.I. P !? Roho inanisuta”. - Ameyasema hayo Christian Bella.

Kumtakia mtu heri katika safari yake ya mwisho sio lazima uwe unamjua
Hapana unaweza kuta maiti barabaran ukasema tu Mungu mlaze mahali pema peponi haijalishi uhusiano mlokua nao

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mwili wa mwanamuziki, Golden Jacob ‘Godzilla’ kesho unagwa katika uwanja wa RTD Salasala kabla ya kuzikwa kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Baba mlezi wa Godzilla, Antoni Kato amesema hapo awali wasanii waliomba aagwe Leaders msanii huyo, lakini jana walikaa ndugu na wasanii na kukubaliana Godzilla ataagwa Salasala na sio Leders.

Kato alisema mazishi ya Godzilla yataanzia nyumbani kwao Salasala na baadae kanisa la Mtakatifu Agustino lililopo Salasala, halafu watarudi katika Uwanja wa RTD Salasala kwa ajili ya kuagwa na watu wote wanakaofanikiwa kufika na baadaye kwenda kuzikwa Makaburi ya Kinondoni saa tisa na nusu

"Tunashukuru tulikaa kikao na kuelewana Godzilla aagwe katika viwanja vya RTD Salasala,baada ya kutoka nyumba na Kanisani,na baadae kwenda kuzikwa Makaburi ya Kinondoni”

Kato alisema sababu ya kuchelewa kuzika ni kutokana na ndugu kumsubiria kaka mkubwa wa Godzilla, Kelvin aliyekuwa anatokea Mwanza.

Godzilla amefariki dunia usiku wa kuamkia Jumatano ya Februari 13 majira ya saa 10 alfajiri nyumbani kwao salasala jijini Dar Es Salaam, baada ya kusumbuliwa na Malaria pamoja na presha.
 
Back
Top Bottom