Supu ya kokoto
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 4,194
- 7,602
- Thread starter
- #41
Nimekuelewa sana mkuu kwenye michango yako ya huko juu. Japo hapa kwetu wamefikia hapo BOT ndo ikaleta zengwe. So na imani zitaingia tu ngoja tuwapange tu hawa wadeni wetu.Hili lina ugumu wake na nina uhakika kama ni kulipa moja kwa moja itachukua muda kuliko hata ilivyo sasa. Tafuta watumishi wanaolipwa malimbikizo ya mishahara ndipo utaelewa.
Kwa uzoefu wangu kwenye suala la kuwalipa waajiriwa wapya hasa wanaolipwa kwa pesa kutoka serikali kuu hakuna ukiritimba kwenye halmashauri isipokuwa ni taratibu za zilizowekwa na serikali yenyewe ambapo halmashauri haiwezi zikwepa wala kuzipindisha. Akipindisha ndiyo utasikia amekiuka taratibu, n.k.
Wanaolipwa kwa makusanyo ya halmashauri hapo ndipo kuna changamoto na mara nyingi makusanyo kama hayako sawa na si mfuatiliaji utasumbuka sana. Hata huko kwenye mashirika na mamlaka taratibu ni hizo hizo isipokuwa wao chain yao ni fupi sana na uhakika wa fedha upo kwa 100% kama siyo 99%.