Tatizo watu wanatuhumu watumishi wa halmashauri bila kujua kwamba si kila aliyepo halmashauri anahusika na masuala ya malipo na bila kujua ni kipi kinafanyika mpaka malipo yakamilike hasa kwa hawa wanaoajiriwa na hela yao kutumwa halmashauri. Kutumwa kwa hela siyo kwamba ikifika leo kesho mhusika anapata. Haiko hivyo na wala huwezi mlaumu mtu wa halmashauri kwa vyovyote vile.
Marytina Prince Mhando Supu ya kokoto Kwa ufupi iko hivi, pesa inatumwa na kuingizwa kwenye akaunti ya halmashauri (naongelea hawa walioajiriwa elimu na afya), halmashauri wanaomba TAMISEMI wawape kifungu cha kulipia hiyo hela kupitia kwa katibu tawala mkoa. Hapa ni kwamba hela hiyo inapokelewa ikiwa bajeti za halmashauri zimeshapitishwa na bunge. TAMISEMI nao wanafanya taratibu zao na Wizara ya fedha, wanarudisha majibu kwa halmashauri kupitia mkoa kwa kuwapa kifungu wao wanaita ceiling (hapa wanaelewa watu wa uchumi na maafisa mipango huko halmshauri kuna taratibu wanafanya na kwasasa naambiwa wanatumia mifumo).
Wakipata kifungu wanaanda bajeti ya kuwalipa hao watu na wanasubiri wizara ya tamisemi waidhinishe na hicho kifungu kisomeke kwenye mfumo wa malipo walipe. Kifungu kikishasoma watu wa uhasibu ndiyo wanaweza kulipa. Hapa sasa ndiyo huwa kuna changamoto sababu halmashauri wao wanaweza kukamilisha taratibu zote mapema mara tu pesa inapoingia lakini wizara wakatumia muda mrefu kuwapa mkoa na halmashauri mwanya wa kukamilisha hatua za mwisho za malipo. Hapo ndipo unakuta wanakaa kwa muda mrefu. Kama mkoa na wizara wanakamilisha taratibu zao mapema kwa halmashauri kunakuwa hakuna kukaa na ni suala la muda hata wiki haipiti labda watumie muda kwenye kukokotoa kila mtu analipwa kiasi gani na kuzungusha hati za malipo kama wanaopitisha hawapo.
Pia kwa halmashauri ambayo inakuwa na uwezo au ina kifungu cha kulipia hiyo hela wanaweza kuwalipa wahusika ili taratibu za hapo juu zikikamilika inakuwa ni kufidia.
Kinachowafanya wakae sana kwa baadhi ya halmashauri ni kukwepa hoja za ukaguzi kwa maana wanaweza kutumia mfano kifungu cha mafuta au likizo kulipia malipo ya kujikimu kwa ajira mpya na mkaguzi akija wanakuwa na hoja za ukaguzi za wrong coding kwamba walitumia vifungu kinyume na matakwa ya kikanuni (hapa wahasibu wanaelewa). Kwamba kwenye nyaraka inasomeka kuwalipa hela ya kujikimu lakini kifungu kinasomeka ununuzi wa mafuta na hapo mkaguzi anakuwa na mashaka (hati yenye mashaka ingawa zipo sababu nyingi).
Kuepuka hili wanasubiri mpaka kifungu husika kiwepo. Ukiambiwa kimeburst ni sawa na wewe ukiishiwa salio kwenye simu ina maana huwezi piga simu.
SUALA la mfumo wa BOT ni sahihi kabisa sababu mimi natoa huduma kwenye halmashauri moja na hilo nimekuwa nikikumbana nalo mara kadhaa wakati wa malipo lakini ukifunguka nalipwa. Tusiwabebeshe lawama nao wanafanya kadri mifumo inavyowaruhusu
KUHUSU pesa ya call allowance ninachojua fedha hiyo inatoka serikali kuu na kwa uzoefu wangu huwa inatolewa kidogo kidogo na kwa vipindi. Sasa huwezi mlaumu mtu wa halmashauri kwamba hajalipa wakati amepokea kidogo au hajapokea kabisa. Mara nyingi nilichokuwa nakiona ni kwamba wakipokea kidogo wanaanza kulipa madai ya nyuma kuja ya mbele kadri wanavyopokea pesa. Hii ni sawa na walimu ambao nao hela yao ya likizo inatoka serikali kuu na si halmashauri.
Tatizo la watumishi mlioko halmashauri hasa nje ya makao makuu na wale mlioko kwenye mashirika ya serikali ni mnapenda yale maneno ya kuambiwa badala ya kujua taratibu zikoje. Unakuta mtu anasema anadai hela ya likizo lakini hajawahi kuandika barua ya kuomba hiyo hela zaidi ya kujaza fomu ya likizo tu. Mwingine unakuta anaomba kulipwa nauli ya kwenda kigoma kutokea mtwara tuseme 200K wakati kwenye taarifa zake alisema makazi yake ni lindi na anapswa kulipwa 20K. Sasa huyo utakuta analalamika kwamba niliomba hela ya likizo 200K nikalipwa 20K na hajalipwa yote.
Ushauri wangu ni kwamba, kama upo kijijini pendeni kuwatumia wale walioko makao makuu wawajuze taratibu za malipo zilivyo na mtaishi kwa amani ukiachana na changamoto za majungu na kusumbuliwa na kila mtu kisa upo halmashauri. Hawa watu wanastahili kutiwa nguvu sana na kuboreshewa mishahara yao.
Mimi niliajiriwa 2008 kama afisa biashara na niliacha kazi 2011 kutokana na niliyoyakuta huko ya kutuhumiwa mwizi achilia mbali kimtaji kidogo nilichopata kwa kujibana sababu sikuwa na majukumu mengi. Imejengeka kwamba watumishi wa halmashari ni wezi ili kuhalalisha wizi kwenye wizara na mashirika huko sababu wao hawana mtetezi na ni watoto wa mkulima.
Hivi unapeleka milioni 20 halmashauri ya kigoma na halmashauri ya temeke ujenge darasa lenye tiles, miundombinu ya umeme na uweke meza na viti unategemea nini!! Mtu wa temeke atajenga lakini mtu wa mafia hataweza kukamilisha vyote hivyo na mwisho mtu atasimama jukwaani anasema wa kigoma ameiba ila wa temeke amekamilisha kwa milioni 20.