Msaada kwa wenye kufahamu kuhusu malipo ya Serikali

Nimekuelewa sana mkuu kwenye michango yako ya huko juu. Japo hapa kwetu wamefikia hapo BOT ndo ikaleta zengwe. So na imani zitaingia tu ngoja tuwapange tu hawa wadeni wetu.
 
🤣🤣🤣, sasa kama huna amani unapata wapi nguvu ya kuchakata mbususu!!??
Hizi nguvu huwa zipo naturally mkuu, hata masikini asiye na uhakika wa mlo wa siku huwa anatamani kuchakata mbususu
 
Inawezekana kweli kuna shida BOT Kwa wiki au zaidi kuwa mvumilivu
 
Kwa maoni ya wadau suala hili nimelielewa...ngoja tuvumilie
 
Inawezekana wewe ndiye mtu wa hovyo sana kwa kushindwa kuelewa maelezo!
Maelezo nimeyaelewa sana ila hapa ileje ndugu njoo ujionee...wenyeji wakishakujua wewe ni mgeni hakuna rangi utaacha kuona. Vitu na mahitaji bei inapanda Mara dufu. Niko chilemba humu ndani ndani. Labda huko itumba na isongole kuna kauafadhali.
 
Maelezo nimeyaelewa sana ila hapa ileje ndugu njoo ujionee...wenyeji wakishakujua wewe ni mgeni hakuna rangi utaacha kuona. Vitu na mahitaji bei inapanda Mara dufu. Niko chilemba humu ndani ndani. Labda huko itumba na isongole kuna kauafadhali.
Hali hiyo si Ileje peke yake, ni po pote Tanzania! Watanzania tumekuwa watu wa kupenda utapeli na kuvuna usichopanda.
 
Ila mbona halmashauri kama ya tunduma wameshapewa. Hii huwa imekaaje? Sisi walikuwa wanatwambia tutapewa then wakaanza kuleta habari kuwa malipo yetu yako tayari shida sasa iko BOT.
Wewe bado mgeni sana halmashauri aisee! Ngoja nikuongezee mfano mwingine..

Kuna ziara ya rais au waziri anakuja kitembelea kituo cha afya, na ujenzi hauja kamilika kwasababu pesa hakuna ila ded anaona kuna kifungu cha malipo yenu kina 10milion na zinatakiwa 10mil ili kukamilisha ujenzi!

Je wewe ungekua ded ungelipa watumishi posho alafu rais akija utumbuliwe au utapeleka kwenye kituo cha afya ili usitumbuliwe?

NB: jiweke nafasi ya ded ndio ujibu.
 
🥲Haki za wanyonge haziendi bure kwa hakika kuna haja ya kuwa na siku ya hukumu ili kila mtu apate haki yake


Viongozi mnaopewa madaraka msidhulumu haki za watu hii ni mbaya inatengeza jamii yenye chuki na viongozi
 

Malipo ya kielektroniki ni changamoto, mfumo umeshatengemaa sasa kuruhusu malipo ya hawa watu?
 
Malipo ya kielektroniki ni changamoto, mfumo umeshatengemaa sasa kuruhusu malipo ya hawa watu?
Kwa kuwa mishahara imeanza kutoka naamin wakifuatilia within two weeks watakuwa wamelipwa specifically watu wa afya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…