Msaada: Laini yangu ya Halotel imepata matatizo ya kiintaneti

Msaada: Laini yangu ya Halotel imepata matatizo ya kiintaneti

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,156
Reaction score
10,974
Nimesajili laini ya Halotel mpya, hii ni baada ya kupoteza laini niliyokuwa nikitumia ambayo haikuwa na matatizo yoyote, ni vile tu nilisajiliwa na mtu ambaye niko mbali naye kwa sasa (Ex)

Laini hii niliyosajili leo haina ufanisi kabisa kwenye suala zima la kimtandao. Yaani ipo very slow kulinganisha na konokono. Nasikia kuna kitu inaitwa kuwezesha laini ya Halotel ili kuendana na simu. Kwa anayefahamu, msaada...
 
Huduma kwa wateja wanakupa maelekezo mazuri maana ndoo kazi yao japo uwe mvumilivu maana kuna mda simu itaita hadi utakata tamaa
 
Natamani nimiliki line ya halotel kwa ajili ya matumizi ya internet lakini naambiwa bado hawajawa stable kwa upande huo.

Nitasoma post hapa labda naweza nikakutana na inayofafanua zaidi utendaji wao.
 
Nimesajili laini ya Halotel mpya, hii ni baada ya kupoteza laini niliyokuwa nikitumia ambayo haikuwa na matatizo yoyote, ni vile tu nilisajiliwa na mtu ambaye niko mbali naye kwa sasa (Ex)...
niliwahi kua na line ya mtanadao huo inaitwa Royal,

nikiwa mjini inafanya kazi vizuri sana, nikienda mkoani tu, hususan jimboni haifany kazi kabisa, akati huko jimboni ndio mtandao unaofanya kazi vizuri zaidi na wanainchi wengi wanatumia huo...

niliwapigia na hadi kuwatembelea ofisini pao lakini haikifua dafu....
niliivunja na kusajili nyingine kule jimboni, ambayo inafanaya kazi vizuri mpaka mjini...

kwa msaada zaodi wapigie tu...
 
Nimesajili laini ya Halotel mpya, hii ni baada ya kupoteza laini niliyokuwa nikitumia ambayo haikuwa na matatizo yoyote, ni vile tu nilisajiliwa na mtu ambaye niko mbali naye kwa sasa (Ex)

Laini hii niliyosajili leo haina ufanisi kabisa kwenye suala zima la kimtandao. Yaani ipo very slow kulinganisha na konokono. Nasikia kuna kitu inaitwa kuwezesha laini ya Halotel ili kuendana na simu. Kwa anayefahamu, msaada...
Unatumia simu ya aina gani. ?
Kuna baadhi ya simu hadi ufanye configuration manually hasa Samsung
 
Chief-Mkwawa na wengine naombeni msaada router yangu ya halotel toka juzi inaniletea huu ujumbe wa ISDN/Account nimejaribu kutia user Name na password zote lkn bila bila wakuu
Screenshot_20240618_155112_Captive Portal Login.jpg
 
Back
Top Bottom