Yote usemayo ni kweli, uchawi UPO KILA SEHEMU ambako ELIMU NI ZIRO. Wanatafuta short cut kwa waganaga ambao wengi ni matapeli na waongo wa kawaida tu! Hata humo maofisini hali ni hiyo hiyo tu, ulozi kwa kwenda mbele. Sasa wewe mwamini Mungu usiwe vuguvugu na kwa bidii yako na maarifa utatoboa tu. Mimi niko mtaani ila nina interest na hii sekta hivyo naisoma na kuifuatilia sana sana na pia ninao wadogo zangu wako machimboni huko Mbekenyela, Lindi na Tunduru na mmoja alisha kwenda hadi Mozambique kuchimba dhahabu lakini akarudi tupu!
Mimi naamini kuwa sekta ya madini inaweza kuitoa nchi hii kwenye umasikini na ufukara huu, na hii ni kwa kuanzia kwa mtu mmoja mmoja na hatimaye taifa kwani fursa humu ni LIMITLESS, THE SKY IS THE LIMIT! Ila uwe na utaalam na elimu ya sekta hiii(hata kidogo kama chembe ya haradali) na pia kwa vile siku hizi vifaa vya kupimia vipo, hakuna sababu ya kutapeliwa. Wekeza kidogo kwenye modern small scale equips ili ushinde. Achna na chaka chaka chaka bro!