Msaada makadirio kwa ramani hii

kiukweli nyumba kubwa ina utamu wake
mwanzoni wakati naanza kujenga niliweka ramani yangu humu watu wakanitisha ila namshukuru Mungu kwa sasa nipo kwenye finishing, wewe nenda mdogo mdogo kama huna haraka sana [emoji106]
 
Asante Sana Kiongozi.Yaani umeongea right on point.Sina haraka nayo Sana so I will take my time kwa phases.Kikubwa mwisho nipate kilicho Bora na Tamanio la Moyo.Napenda Sana nyumba iliyo na eneo la kutosha.
kuna watu walisema hiyo ni nyumba au hekalu japo sio kubwa kiivyo sema ukisikiliza sana watu waweza kughairi ujenzi
 
Big up Mkuu,umeelezea vizuri hadi raha.Wewe ni Engineer?.
 
Bora finishing unauwezo wa kuifanya taratibu ,ila sio kupaua ni habari nyingine.

Mimi hapo nipo dilema kuchagua kati ya ANDO na ALAF,nimefanya uchunguzi bei zao hazitofautiani sana sema Alaf mkoa ninaokaa inabidi kuwatumia mawakala ambao siwaamini
Chukua ALAF mkuu
 
Kha!kha!, Acha kutisha watu bhana.
Sema uhalisia sasa! Na vyovyote atakavyofanya, iwe kujenga kwa kuunga unga au mwanzo-mwisho, 110m haiepukiki!

Kila siku mnasema watu wanatisha wengine kujenga, kusema huo ukweli wa gharama nafui au hata kuweka makadirio hayo ya bei nafuu hamuweki.
 
kiukweli nyumba kubwa ina utamu wake
mwanzoni wakati naanza kujenga niliweka ramani yangu humu watu wakanitisha ila namshukuru Mungu kwa sasa nipo kwenye finishing, wewe nenda mdogo mdogo kama huna haraka sana [emoji106]
Hongera Sana Mkuu nakumbuka kweli Uzi wako wa ile nyumba.Big up sana
 
Hiyo nyumba 16M hatoboi kumaliza boma labda kama anatumia tofali za kuchoma na anajengea udongo baadala ya saruji. Hiyo nyumba msingi peke yake kwa ujenzi standard wa DSM au Dom itakula 10M. Kupandisha pia not less than 10M. So aandae 20M. Otherwise aondoe beam
 
Ni kweli kiongozi hapo kwa msingi tu imefikia 12M
 
unatumia za kuchoma au block?

by the way weka madrsha makubwakubwa kusave tofali.
Ondoa hilo wazo kuanzia leo moendwa, dirisha kubwa halisave gharama, unapoongeza ukubwa wa dirisha(madirisha makubwa), maana yako unapunguza tofali si ndio, basi ujue unaongeza na gharama za dirisha lenyewe, liwe la mbao ama la kuchomelea ama aluminium, vipimo vikizidi na mpunga unazidi.

Madirisha makubwa ni mazuri hasa kwa kuingiza hewa swaafi, ila hayapunguzi gharama
 
.kuu hiyo nyumba ina makona na vi chunba vingine visivyo na umuhimu ongea na fundi apunguze hayo ili anagalao upunguze ukubwa. Hizo nyumba si kwa sisi wabongo labda uijenge kama 2 in one ili upande mmoja uipangishe lakini kwa hiyo mkuu mmh
 
.kuu hiyo nyumba ina makona na vi chunba vingine visivyo na umuhimu ongea na fundi apunguze hayo ili anagalao upunguze ukubwa. Hizo nyumba si kwa sisi wabongo labda uijenge kama 2 in one ili upande mmoja uipangishe lakini kwa hiyo mkuu mmh
Mkuu ingefaa iwe vyumba vingapi ili iwe na standard nzuri na ya kawaida?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…