MSAADA: Mama mkwe amenifungulia kesi ya uharibifu wa Mali

MSAADA: Mama mkwe amenifungulia kesi ya uharibifu wa Mali

Status
Not open for further replies.
Niliposoma maelezo yako nimegundua yafuatayo:
1- Wewe ni mwanamke mjuaji na mpumbavu unaetaka kua juu ya mume wako.
2- Unamume mjinga ambae hana uwezo wa kusimama na kuongoza familia.
3- Mama wa mume wako ni shangingi la mjini lisilotamani kuona mwanae akipata mke kwa hofu ya kukatiwa mrija wa pesa za mahitaji yake.
4- Huyo sio mume wako kwasababu hakuna ndoa mlioifunga (ingawa sheria inakulinda kwasababu mmeishi pamoja kwa zaidi ya miezi sita.
5- Mwisho nina imani kesi utashinda kwasababu sheria inakulinda ingawa utachelewa kuipata haki yako.
Pia ukishinda kesi jiandae kuishi maisha magumu ya vita shari na ushirikina.
Mimi nakushauri ondoka kwenye hiyo nyumba na ukaanza maisha mapya (kama nilivyo fanyaga mimi) na Mungu atakubariki
Hizo points kali sana
 
For now i am not ready cz am not stable financially, Siogopi kwasabu namwamini Mungu
Umejibu vyema binti Jovetha. Zingatia hili: Ukishaanza mchezo wa kuolewa na kuachika ni kama kula nyama ya Mtu - Hutakaa uache. yaani Umejitia NUKSI mwenyewe.

Jiepushe MNO na ushauri wa namna hiyo kwa maneno ya kejeli "...hey!! ninachofia nn, bado nauzika mwaya; asinibabaishe; nitaolewa kwingine, na miye nna kwetu... ebo..."

Watakaokuambia hayo ndo haohao kesho watakaokusota kidole na kusema - Tulijua tuu.... heheheee...wenzake tunasota hapa yy anapata bahati ya kuolewa halafu analeta za kuleta.

Shenzi kabisa...
 
Hizo points kali sana
Hawa ni ndugu zetu na wameumbwa kwaajili yetu. Sasa tusipo waambia ukweli lazima wataharibikiwa, and huyu mama hawezi pata msaada wa ndoa/mahusiano kwenye mitandao na badalayake tutajitokeza na kujifanya tunamhurumia kisha tunamkula tu...😕
 
Naombeni msaada wa mawazo maana nahisi nitakufa kwa mawazo ila ninajikaza.Mimi ni mama wa miaka 30 Nina mtoto mmoja, nina ndoa ya kimila.Nampenda sana mme wangu lakini tumekuwa hatuna maelewano mazuri mm na yeye kwa sababu ni mtu wakusikiliza ndugu na pia ni mtu ambaye anaona mawazo ya ndugu zake ndo mawazo sahihi especially his mum,mpaka ikafika hatua ya yeye kuhama nyumbani na kwenda kuishi kwa wazazi wake ambao hawako mbali na tunapoishi yapata mwaka sasa tangu aondoke vikao vya kifamilia tumeshakaa lakini hakuna suluhu mpaka Sasa ambayo imefanikiwa.

Sasa hapa ninapoishi tuna nyumba mbili, nyumba Moja ni mpya bado hatujahamia hivyo tumeifanya kama store pia tulikuwa tumeshaweka na vitu vingine kama makabati ili tuweze kuhamia, kutokana na migogoro yetu mpaka sasa hatujahamia.

Hivi karibini nilipoteza ufunguo wa hiyo nyumba mpya hivyo ikanibidi nimuite Fundi ili aweke kitasa kipya ili niweze kufanyia nyumba usafi maana hapa tunapoishi Kuna mchwa wengi hivyo nilazima kufanya usafi vitu visiharibiwe na mchwa. Baada ya kubadilisha kitasa nikamwambie dada apafanyie usafi,wakati dada akiendelea na usafi,

Mara shemeji akaja amkamfukuza yule mdada na kuchukua zile funguo za nyumba na baadae mama mkwe alifika nyumbani na rafiki yake akinigombeza kwanini nimevunja mlango wa nyumba,nikamwambie sijavinja nimebadikisha kitasa,akaniambia kwanini nabadilisha kitasa Cha nyumba bila kumpa taarifa,nikamwambie,nyumba si yangu na mme wangu ndo maana sijawapa taarifa kama nimebadilisha kitasa na baada kama ya siku 10 kupita nikapigiwa simu nahitajika kituo Cha police kufika pale nikaambiwa nimeshitakiwa na mama mkwe kwa uharibifu wa Mali na kesi ikapelekwa mahamani mind you kwenye kiwanja tulichojenga tulipewa na baba mkwe.Naombeni msaada wa kisheria juu ya hii case
Watu mna moyo
 
Direct nataka nikwambia fanya upatane na familia ya mumeo..wewe una tatizo ususani kwenye majibu na kumbuka hilo ni kosa kuvunja mlango kwa sababu ulizo ziandika,kuna kati ya miezi sita au mwaka jela na faini juu.
Kisaikoloji utetezu wako hauna mashiko bali utakukandamiza mbele ya pilato...Hili bomu lililo andaliwa juu ya mke,mwanamke kuwa juu ya kila kitu mpaka mnajisahau ujue msipo jielewa mtaelewa......
umeomba ushauri na huo ndio wangu ukipenda chukua ukiona haufai waachie JF.
Ulishawahi kuwa kwenye situation ya kutaka amani na mtu/watu wao wakawa hawataki kabisa? Acha kucomment kitoto elewa kuwa situation zinatofautiana ya huyu mwadada haifanani na yako acha kumkandamiza mwanamke mwenzetu sababu ya past experience yako.

Kama huyu mwanadada ana makosa wamshtaki kwa kosa alilofanya kama linashitakika kusheria, waache kufabricate case eti ohh amefanya uharibifu wa mali, toka lini kuvunja kitasa cha nyumba yako mwenyewe likawa kosa? Hii tabia ya kutengenezeana vikesi si nzuri.
 
Umejibu vyema binti Jovetha. Zingatia hili: Ukishaanza mchezo wa kuolewa na kuachika ni kama kula nyama ya Mtu - Hutakaa uache. yaani Umejitia NUKSI mwenyewe. Jiepushe MNO na ushauri wa namna hiyo kwa maneno ya kejeli "...hey!! ninachofia nn, bado nauzika mwaya; asinibabaishe; nitaolewa kwingine, na miye nna kwetu... ebo..."
Watakaokuambia hayo ndo haohao kesho watakaokusota kidole na kusema - Tulijua tuu.... heheheee...wenzake tunasota hapa yy anapata bahati ya kuolewa halafu analeta za kuleta. Shenzi kabisa...
Kibaya zaidi ni kuwa na watoto wa baba tofauti
 
Hawa ni ndugu zetu na wameumbwa kwaajili yetu. Sasa tusipo waambia ukweli lazima wataharibikiwa, and huyu mama hawezi pata msaada wa ndoa/mahusiano kwenye mitandao na badalayake tutajitokeza na kujifanya tunamhurumia kisha tunamkula tu...😕
Sasa mnyambo walivyonyambuka unamwachaje kwa mfano, masipota jovetha!
 
Direct nataka nikwambia fanya upatane na familia ya mumeo..wewe una tatizo ususani kwenye majibu na kumbuka hilo ni kosa kuvunja mlango kwa sababu ulizo ziandika,kuna kati ya miezi sita au mwaka jela na faini juu.
Kisaikoloji utetezu wako hauna mashiko bali utakukandamiza mbele ya pilato...Hili bomu lililo andaliwa juu ya mke,mwanamke kuwa juu ya kila kitu mpaka mnajisahau ujue msipo jielewa mtaelewa......
umeomba ushauri na huo ndio wangu ukipenda chukua ukiona haufai waachie JF.
Bitter truth

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom