Msaada: Mbwa wangu amebakiza saa machache afe

Msaada: Mbwa wangu amebakiza saa machache afe

Mpe mafuta ya kupikia chakula au maziwa mkuu, imewahi kutoa kwa mbwa wetu after food poisoning. Mpe pole huyo mbwa
 
Hapana mkuu mbwa wangu huwa nawafungulia jioni kula ila asubuhi huwa nawawekea chakula humo humo kabla sijaondoka..
Huyu jirani yangu tulitofautiana kipindi fulani, mwanae alikuwa anamtongoza mfanyakazi wangu..
Jirani yako mshenzi hana utu, why aweke sumu kwa mbwa, kuweni makini na hata huyo dada wenu wa kazi anaweza kutumika
 
Kwa hakika hapo ni sumu imehusika zaidi. Hakuna ugonjwa unaoweza kuingia mara moja kwa mbwa wote watatu na kuanza kufa ghafla.
 
Amina.

Hutakiwi kuishi kwa kuwakwaza wengine kiasi cha kupelekea wakuchukie namna hii.

Tubu dhambi zako, Na uwapende jirani zako kama unavyojipenda.
Mkuu kuna watu hata uwe peace [emoji3522] vipi watakutafuta tu shida ianze. Tena kwa hali ya sasa ya kiuchumi ukithubutu hata kubadili gari tu walimwengu wanaanza minong'ono ya kukujadili as if umechukua pesa yao na ndio umetumia kununulia gari.

Me huwa namaintain amani kwa kumind my own business. Kukitokea msiba kama kawa najichanganya, sherehe natimba, vikao vya kitaa natokea, ila normal days me nipo so indoors na nikitaka kuchill viwanja vyangu ni vya mbali na mitaa hiyo. Hii inasaidia sana katika kuheshimiana.
 
Mkuu huyo mbwa ana dalili moja tuu ya kuhema kwa shida? Vipi haarishi wala kutapika?
Ndio alikuwa anaharisha na kuhema kwa shida sana. Na hana nguvu kabisa, pia kula alishindwa
Je alikuwa na shida gani
 
Jirani yako mshenzi hana utu, why aweke sumu kwa mbwa, kuweni makini na hata huyo dada wenu wa kazi anaweza kutumika
Sielewagi nilimkoseaga nini yaani kwa kweli.
Lakini sidhani kama yeye ndio kampa sumu siwezi jua mkuu wangu.
 
Kwa hakika hapo ni sumu imehusika zaidi. Hakuna ugonjwa unaoweza kuingia mara moja kwa mbwa wote watatu na kuanza kufa ghafla.
Ni kweli mkuu hawawezi kufa wote pamoja hata kama wanaumwa. Walikufa wote kwa masaa tu.
Huyu mmoja leo kamalizikia.
 
Kuna majirani huwa hawapendeki hata ukiwa mkimya ni wa evil in nature na hawapendeki
Zaburi 119:62
Katikati ya usiku nitaamka nikushukuru,
Kwa sababu ya hukumu zako za haki.

Mungu wetu ni HAKIMU, Anahukumu, na Hukumu zake ni za Haki (Hana upendeleo)... Ukipeleka MASHITAKA KWAKE, Huyapima na kutoa hukumu kwa Haki... PELEKA WATESI/MAADUI ZAKO WOTE KWA MUNGU (SIO KWA WAGANGA WA KIENYEJI) Mungu kwa UAMINIFU wake atapima mashtaka yako na kukupa haki yako bila upendeleo... Unapopeleka mashitaka hakikisha MOYO WAKO NI SAFI JUU YA HUYO UNAYEMSHITAKI, Vinginevyo Hukumu itakupata wewe mwenyewe kwani MUNGU WETU UHUKUMU KWA HAKI.

UTAKUAJE NA MOYO SAFI... FANYA TOBA, TUBU HASWA, YANI TUBU KWELI KWELI KIASI CHA KWAMBA UKITENDA UOVU TU MOYO WAKO UNA KUSUTA.

Narudia, HAKIKISHA MOYO WAKO NA MIKONO YAKO NI SAFI NDIO UPELEKE MASHITAKA. TUBU
 
Mkuu kuna watu hata uwe peace [emoji3522] vipi watakutafuta tu shida ianze. Tena kwa hali ya sasa ya kiuchumi ukithubutu hata kubadili gari tu walimwengu wanaanza minong'ono ya kukujadili as if umechukua pesa yao na ndio umetumia kununulia gari.

Me huwa namaintain amani kwa kumind my own business. Kukitokea msiba kama kawa najichanganya, sherehe natimba, vikao vya kitaa natokea, ila normal days me nipo so indoors na nikitaka kuchill viwanja vyangu ni vya mbali na mitaa hiyo. Hii inasaidia sana katika kuheshimiana.
Ni kweli kabisa, IKO HIVI... Shetani yupo kazini masaa 24 kwa siku saba za wiki.

Ufunuo wa Yohana 12:12
"Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu."
(Yeye hana sabato maana alishaasi), yupo kazini ili Kuongeza wafuasi, siku ya hukumu asipewe adhabu peke yake.

SHetani huwatumia, Ndugu, Marafiki, Jamaa na watu mbalimbali wanaotuzunguka. Anafika kwa njia ya Upendo, akisha fanya analotaka anakuacha na majonzi, hapo wewe utataka kulipa kisasi.. ukilipa kisasi basi ndo umeungana nae, wewe ni wake kiuhalali kabisa.

Mfano... Shetani anamtumia rafiki yako kuangamiza biashara yako, kisha anamtumia Mjomba wako akushawishi uende kwa Mganga ukapige ramli na kujikinga, na Wewe bila kumtanguliza Mungu unaenda kwa mganga na kufanyika kuwa mtumwa wa shetani, masharti yanaanza... Kila baada ya miezi mitatu leta mbuzi mweupe pee tutoe kafara, baada ya miaka miwili, shetani hataki tena damu ya mbuzi.. mganga atakuambia mtoe kafara Mama yako au Mwanao umpendaye.. ndio kwaheri hivyo wewe wa shetani.

UFANYE NINI KUJINASUA NA KUJILINDA...
1.Mtangulize Mungu, KUWA MWAMINIFU NA MSAFI HASWA KIROHO (TUBU MARA KWA MARA)
2.ISHI KWA UPENDO
3.PUNGUZA MAHUSIANO YASIYO YA LAZIMA.

Tukumbuke kutubu...
 
Back
Top Bottom