Mkuu kuna watu hata uwe peace [emoji3522] vipi watakutafuta tu shida ianze. Tena kwa hali ya sasa ya kiuchumi ukithubutu hata kubadili gari tu walimwengu wanaanza minong'ono ya kukujadili as if umechukua pesa yao na ndio umetumia kununulia gari.
Me huwa namaintain amani kwa kumind my own business. Kukitokea msiba kama kawa najichanganya, sherehe natimba, vikao vya kitaa natokea, ila normal days me nipo so indoors na nikitaka kuchill viwanja vyangu ni vya mbali na mitaa hiyo. Hii inasaidia sana katika kuheshimiana.
Ni kweli kabisa, IKO HIVI... Shetani yupo kazini masaa 24 kwa siku saba za wiki.
Ufunuo wa Yohana 12:12
"Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu."
(Yeye hana sabato maana alishaasi), yupo kazini ili Kuongeza wafuasi, siku ya hukumu asipewe adhabu peke yake.
SHetani huwatumia, Ndugu, Marafiki, Jamaa na watu mbalimbali wanaotuzunguka. Anafika kwa njia ya Upendo, akisha fanya analotaka anakuacha na majonzi, hapo wewe utataka kulipa kisasi.. ukilipa kisasi basi ndo umeungana nae, wewe ni wake kiuhalali kabisa.
Mfano... Shetani anamtumia rafiki yako kuangamiza biashara yako, kisha anamtumia Mjomba wako akushawishi uende kwa Mganga ukapige ramli na kujikinga, na Wewe bila kumtanguliza Mungu unaenda kwa mganga na kufanyika kuwa mtumwa wa shetani, masharti yanaanza... Kila baada ya miezi mitatu leta mbuzi mweupe pee tutoe kafara, baada ya miaka miwili, shetani hataki tena damu ya mbuzi.. mganga atakuambia mtoe kafara Mama yako au Mwanao umpendaye.. ndio kwaheri hivyo wewe wa shetani.
UFANYE NINI KUJINASUA NA KUJILINDA...
1.Mtangulize Mungu, KUWA MWAMINIFU NA MSAFI HASWA KIROHO (TUBU MARA KWA MARA)
2.ISHI KWA UPENDO
3.PUNGUZA MAHUSIANO YASIYO YA LAZIMA.
Tukumbuke kutubu...