Msaada: Mke wa mtu anataka kuhamia kwangu

Only human after all don't put a blame on me!!!wimbo huwa naupenda sana.
 
Kwakuwa wewe, huyo mwanamke na mumewe ni watu wazima, kisheria nyote mnawajibika na maamuzi yenu. Wewe ulikutana na mwanamke na baada ya kukwambia yeye ni mke wa mtu tena mwenye watoto uliridhia kuanzisha mahusiano nae bila kuwa na doubt yoyote. Mwanamke kwa ridhaa yake na utashi aliamua kuanzisha mahusiano na wewe akijua wazi yeye ni mke wa mtu ila akataka kuwa na wewe pembeni ya mume wake. Jamaa amegundua unatafuna mkewe kaamua kukuachia ingawa kishingo upande lakini akaona ni bora akuachie ili asiendelee kuishi kwa mashaka.

Sasa sioni shida ipo wapi upande wako kwasababu wewe ulimtaka mwanamke na mwanamke amekutaka nyote mlilidhiana na kuwa tayari kupendana ingawa hamkuwa mkiishi pamoja. Kitendo hadi huyo mwanamke alianza na wewe mahusiano halafu baadae akashtukiwa na mumewe but still akaendelea na wewe it means alitaka wewe uwe mbadala wa mume wake.

Sasa mwanaume kutumia hekima, hajamdhuru mkewe ameamua tu kukuachia umchukue ili muwe huru. Sasa mbona unaanza kulalamika na kujitetea kwa hofu?

Kwani wewe si ndicho ulichotaka hicho kuwa na huyo mwanamke, why unaogopa kuweka ndani mali hiyo ufanye nayo maisha au unaogopa na wewe itakupiga matukio kama ya mwenzako? [emoji23][emoji23][emoji23]

Chukua mke huyo anza nae maisha, sometimes mke mwema anatoka kwa bwana.
 
Issue sio kuoa ndugu yangu. Issue huyu ni Mke wa mtu. Namuoaje duh! Mi sijui hata kesho yangu... Inauma sana
Jamaa amekuachia na ameshavuta mke mpya, unasemaje mke wa mtu tena na umeshapewa umalizane nae mwenyewe?

Muelekeze makazi mapya huyo mwanamke aje alale. We unataka mwenzako akalale wapi ebo? [emoji848]
 
Mmmhhhh
 
Jamaa amekuachia na ameshavuta mke mpya, unasemaje mke wa mtu tena na umeshapewa umalizane nae mwenyewe?

Muelekeze makazi mapya huyo mwanamke aje alale. We unataka mwenzako akalale wapi ebo? [emoji848]
Ety mwenzio
 
Kwa kweli inashangaza sana. Kipindi mwanamke yuko kwenye ndoa mleta mada alikuwa anampenda sana. Eti now kawavunjia ndoa yao eti nae hantaki tena huyo mwanamke na anampa majina mabaya eti singo maza wakati yeye ndo kamshawishi mpaka kupelekea huo using maza.
 
Sio majina mabaya bali ni khali khalisi
 
Kivyovyote vile huyo jamaa hatokuacha salama.. kiufupi jiandae kuliwa jicho
Ajiandae na ukilema wa Kudumu mimi namfaham jamaa nitamsaidia kumpeleka kwa sangoma ili iwe fundisho kwa wengine ulikuwa unajidai na mkewe yeye anahangaika kutafuta wewe unamlia mkewe na hela zake juu ktk hili mimi lazima nimsaidie rafiki yangu. Wewe na huyo mwanamke lazima mnyooshwe na dunia ili iwe fundisho.
Afadhali ungekuwa hujui kuwa ni mke wa mtu lakini hata ulipojua ulizidi kumuumiza mwanaume mwenzio. Kibaya zaidi hata mlipogundua kuwa amejua bado mlishirikiana na huyo mwanamke kumuumiza rafiki yangu. Hakuna namna lazima na nyinyi muumie tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…