Msaada: Mke wa mtu anataka kuhamia kwangu

Msaada: Mke wa mtu anataka kuhamia kwangu

Akili za kitoto mbaya sana. Umeharibu ndoa ya mtu then kudadeki. Jiandae kuliwa jicho.
 
Uyu dogo kanikera hata kama hii ni chai. The way men tunahaso kwa ajili ya wake zetu na maisha yetu ya baadae alaf mtu analeta ujinga kama huu. Nakukula jicho kudadeki zako dogo.
 
Uyu dogo kanikera hata kama hii ni chai. The way men tunahaso kwa ajili ya wake zetu na maisha yetu ya baadae alaf mtu analeta ujinga kama huu. Nakukula jicho kudadeki zako dogo.
Punguza matusi mkuu
 
Uyu dogo kanikera hata kama hii ni chai. The way men tunahaso kwa ajili ya wake zetu na maisha yetu ya baadae alaf mtu analeta ujinga kama huu. Nakukula jicho kudadeki zako dogo.
Sidhani kama ni chai maana kisa kama hicho kimewahi kutokea daresalaam maeneo ya bunju usalama. Jamaa alikuwa mtu wa safari za mara kwa mara, siku moja alivorudi nyumbani alimfumania mkewe nyumbani kwake kwenye kitanda chake mwenyewe. Aliachana nae Kwa amani na nyumba wakauza. Mpaka sasa jamaa ameshaoa mwanamke mwingine na ameshajenga nyumba nyingine maisha yanaenda flesh. Kwa hiyo mambo kama hayo yapo na yanatokeaga.
 
Sasa nifanye nini ndugu? Nipe wazo basi mwanaume mwenzio... Haya mambo hayana mwenye
Njoo tuyazungumze nipe jicho nilibize siku 15 yaani nusu mwezi at least bao 65 ntakusamehe na mke wangu namrudia naomba ufanye haraka uje na makopo mawili
 
Njoo tuyazungumze nipe jicho nilibize siku 15 yaani nusu mwezi at least bao 65 ntakusamehe na mke wangu namrudia naomba ufanye haraka uje na makopo mawili
Punguza dharau mkuu
 
Mchuma janga ula peke yake . Mke wa mtu ni mtamu sana coz unakuta amenona ila sasa ukishakabidhiwa ndo shughuli inaanza .
 
Khabarini wana jukwaa.

Mwaka 2021 nilikutana na dada mmoja mzuri sana, mrembo, mwenye kuvutia na mpole sana ambaye mwanaume yeyote mwenye akili timamu lazima tu angempenda. Basi nikafanya mchakato nikapata mawasiliano yake. Baada ya kuwasiliana na kumueleza shida yangu hakuwa na hiyana hivyo tukaingia katika mahusiano japo alinambia kuwa yeye ni mke wa mtu na ana Watoto wawili.

Kusema kweli tulipendana, mpaka sasa nampenda sana. Mme wake ni mtu wa mishemishe, mara nyingi hayupo. Hivyo nilikuwa naenda usiku kulala kwake na siku nisipoenda basi nilikuwa nampigia simu huyo mpenzi wangu tunazungumza hadi usiku wa manane. Au chatting kwa WhatsApp au sms za kawaida. Japo tulifanya kwa siri sana na mtu asingeweza kugundua, hata rafiki zangu wa karibu hawakujua na rafiki zake pia hawakujua lolote.

Penzi letu lilinoga mno, ilifikia hatua nikawa namiliki CREDIT CARD ya mme wake, na haikuwa issue kufanya miamala midogo midogo. (sio kwamba nilikuwa nalelewa sema tu alinipenda na kuniamini kiufupi tunapendana) pia nilimpenda mno mtoto wake mdogo, nilikuwa nampelekea vizawadi zawadi nikienda kulala, nacheza nako in short ni kacheshi mno kale katoto na kalinipenda pia.

Wakuu, hakuna marefu yasiyo na ncha, hatimaye mwenyemke akajua kwamba mke wake anachepuka, (hapo ndipo chanzo cha tatizo langu) akajaribu kutafuta ajue anachepuka na nani, akatafuta mpaka akapata namba yangu, mke wake akanambia kuhusu hili hivyo tukakubaliana tusitumiane sms na atakuwa ananitafuta yeye. Na mimi niliamua kuchukua extra precaution ikiwa ni Pamoja na kutopokea namba ngeni, pia mke wake alikuwa akinipigia nikipokea nasubiri aanze yeye kuongea ndo na mimi niongee. Baada ya jamaa kuona sipokei namba ngeni wala kujibu sms za namba ngeni aliamua kutafuta jina nililosajiria laini, nashukuru mungu laini yangu hiyo nilisajiri kwa jina la mtu mwingine na mtu huyo alikuwa mkoani hivyo asingeweza kunifahamu.

Baada ya harakati za kunitafuta kugonga mwamba, jamaa aliamua Kwenda mkoani kuendelea na mishe zake. Mimi na mpenzi wangu tukarudisha mapenzi na tukaendelea kuchati na kupeana mambo kama kawaida. Siku ya jumamosi mwezi wa nne tarehe 13 jamaa alirudi, na mke wake alinijuza juu ya ujio wake. Usiku mida ya saa 4 kuna message moja illingia WhatsApp kutoka namba ngeni nanukuu

“NIMEAMUA KUKUACHIA HUYO MWANAMKE, KESHO ATAKUJA MUANZE NAE MAISHA, MIMI NTABAKI NA WANANGU. ASANTE SANA MWANAUME MWENZANGU”

Ujumbe huu ulinishitua sana na ukizingatia ulikuwa umeeandikwa kwa maandishi makubwa kuonesha msisitizo, kusema kweli niliamua kuhama ghetto nikaenda logde kulala ili kulinda usalama wangu maana nilihisi kama naweza patwa na jambo baya. Pia simu nilizima ili isije kuwa tracked nikapatikana kiboya. Usiku sikupata usingizi hata kidogo yaani hata kufumba tu macho hakuna. (acheni jamani watu tunapitia shida sana hapa Tanzania duh) kuna mda natamani hata niwe mkimbizi Afghanistan kuliko kuishi hapa Bongo.

Kuna jambo moja ambalo mke wake hakunambia na alinambia ikiwa ni too late. Kumbe jamaa alimpa zawadi ya simu kabla hajarudi mkoani kwenye mishe zake, simu hiyo alikuwa ameihack achilia mbali normal sms and calls, hata chatting za WhatsApp alikuwa anaziona na kuzisoma. Jambo hili lilinishitua sana maana nilijua atakuwa amenasa pia picture zangu tunazotumiana na mkewe hivyo kudakwa ni suala la muda tu.

Kwa ufupi ni kwamba.

Jana Asubuhi na mapema nilihama huo mtaa, nikaenda mtaa mwingine mbali kabisaa maana nilihisi jamaa anaweza niletea huyo mke wake hadi kwangu. hivyo asubuhi na mapema niliita Kirikuu ikabeba vitu vyangu nikasepa. Leo saa 4 usiku nikapokea simu ya huyu mwanamke (mpenzi wangu) akanambia kwamba

baba jay (code) amekuja na mwanamke mwingine, mimi amenifukuza amekatalia watoto wake nimekuja hapo kwako wamesema umehama, kwanini umehama bila kunambia? Uko wapi nahitaji tuzungumze.

Ujumbe huu umefanya nikatetemeka kuanzia unyayo mpaka utosi, sikutarajia jambo kama hili, huyu mwanamke anasema anataka aje tuishi, pia nimsaidie afungue shauri mahakamani ili apewe talaka, mgawo wa mali na Watoto pia. Yaani niko njia panda nawaza nimuelekeze nilipo? Dah! Hata sielewi… na mimi sina mpango wa kuoa saa hizi. Yaani kimsingi sitaki kabisaa mambo ya kuoa iwe leo au kesho. Hata nikitaka kuoa siwezi oa single mother, nyumbani watanielewaje? Wakiskia story kuhusu huyu mpenzi wangu je itakuwaje? Duh.

Mambo ni mengi sema siwezi Andika yote ntapoteza muda wenu bure.

Ndugu zangu naombeni Mnishauri nina shida sana. Yaani dunia imekuwa chungu sana kwangu, naishi kwa kujificha kama mnyama duh! Nimechoka na maisha ya utumwa. (better die free than living as a slave)

Endelea 👇 👇

Msaada: Mke wa mtu anataka kuhamia Kwangu
Kuna watu watakuonea huruma na kukushauri.

Mkuu, hata ukitolewa marinda hatuna hasara na wewe mkuu.

Baada ya kumvunjia ndoa huyo mpumbavu mwenzako, nenda na kwingine ukaanze mahusiano motomoto kama ilivyokuwa ada yako
 
Kuna watu watakuonea huruma na kukushauri.

Mkuu, hata ukitolewa marinda hatuna hasara na wewe mkuu.

Baada ya kumvunjia ndoa huyo mpumbavu mwenzako, nenda na kwingine ukaanze mahusiano motomoto kama ilivyokuwa ada yako
Punguza matusi mkuu. Kuwa na ubinadam
 
Ndugu zangu kabla sijaendelea kuna mambo machache nilitamani kuyasema:

Kwanza, unapomuona mtu amekuja kuomba ushauri JF unapaswa umshauri na sio kumtukana, kumkejeli na kashfa nyingine nyingi. Kila mtu anakosea, usijione wewe ni mkamilifu sana kiasi cha kuwa na haki ya kutukana wenzio.

Pili, kuna wazee wa kudai muendelezo hawa watu wanakera sana, unaomba ushauri, wao wanaomba muendelezo inamaana hata ukifa ni sawa tu kikubwa wao wapate muendelezo.

Tatu, napenda kuwashukuru wanajf wafuatao kwa ushauri wao Nuzulati DR HAYA LAND Wakilimkuu , laskaboza Lubebenamawe Excel na wengine wote walionipa ushauri ambao kwa namna moja au nyingine umeniwezesha mimi kuwa hapa nilipo leo.

Nyie wenye akili, msiokosea, Malaika watakatifu njooni tena mnitukane. Haiwezekani mtu anakutukana kama vile anakulisha… tuache mambo ya ajabu… kila mtu anakosea… kukosea kwangu kidogo kusifanye nionekane kama mimi ndo mkuu wa wenyedhambi….

…….. ……….. ……….

Tuendelee…

jana nilikamilisha mchakato wa kuuza vitu vyangu vyote, (usiombe uuze kitu ukiwa na shida mtu ananunua kama vile hataki, tena kwa bei anayotaka yeye…) niliuza mpaka simu yangu ya mkononi nikanunua nyingine, laini pia nimesajiri nyingine. Mara ya mwisho nimewasiliana na huyo mwanamke jana asubuhi, nikaahidi Kwenda kumuona, japo sikuthubutu Kwenda. Sasa niko kwenye gari, nimeamua kurudi kwanza nyumbani ili nijipange nianze mapambano ya kutafuta Maisha upya… sina mawasiliano na huyo mwanamke kwa sasa, japo namba zake ziko kichwani na sijui zitatokaje. Ila nimepanga niwe napeleleza taratiru na nikigundua kuwa mme wake amemuacha ki ukweli ukweli ntaenda tu nimtafute ili tuweze kuendeleza Maisha yetu Pamoja. Kusema kweli kuna chemistry Fulani nzuri sana kati yetu na naamini tutafika mbali… (japo namuomba Mungu amsaidie wayamalize haya mambo na mmewe and finally waishi vyema)

Samahani kwa wote ambao story yangu itakuwa imewakera kwa namna moja au nyingine ila ndo Maisha haya… pia NAOMBA MSAMAHA kwa mme wa mwanamke huyo iwapo atauona ujumbe wangu naomba anisamehe sana I know it hurt… (sometimes life lose its purpose and everything become a mess)

kwa mama jay (kipenzi changu) I chose to be your friend but falling in love with you was out of my control…


Rag’n’Bone Man -
Human
Acha kujiliza liza wakati wewe umeelezea kwa kina umalaya wenu mliokuwa mnaufanya.
Kwa taarifa yako, mwanamke akishatoka nje ya ndoa na akaja kuolewa na huyo mchepuko, muoaji ajiandae kisaikolojia maana atokaye nje haachi hadi akutane na vumbi.

Yaani jiandae na hiyo chemistry menu, utakuja kustuka too late
 
Back
Top Bottom