Msaada: Mke wangu anataka tuwe tunaishi na mtoto wa dada yake kila wikiendi na likizo

Msaada: Mke wangu anataka tuwe tunaishi na mtoto wa dada yake kila wikiendi na likizo

Mkuu jaribu kuangalia tu maslahi ya huyo mtoto asiye na hatia. Kama mama'ke ana hali ngumu na wewe una nafuu ya maisha mbebe tu huyo mtoto. Ila kama mama yake ana nafuu ya maisha basi amlee mwanaye mwenyewe. Mtoto kwenda kwa baba na mama wa kambo ni very risk
 
Mkuu ushazungumzia wangu wamwingne Kama anakulia ktk tabia chafu utakubali awe mda wote na mwanao
Kuwa baba kwa watoto wote bila kujali ni wa kwako au la, inaelekea humpendi kabisa huyo mtoto mwingine..acha ubaguzi.
 
Sio tabia mbaya mkuu mtoto kashashika michezo yakike tu kwake
Acha kujitetea, wewe una roho Mbaya, huyo Mtoto Mdogo tu anakumalizia nini !?
Je ! Angekua ni Mtu mzima Ndugu ya Mkeo anataka kuishi Kwako si ungemfukuza na Mapanga !!!

Hizo unazosema kuwa Mtoto wako anacheza michezo ya Kike isiwe sababu ya kujitetea....

Acha uchoyo na roho mbaya.
 
Wanaume tujipange maana tunazidi kupungua, yani tumebaki watu wa ajabu ajabu, mtu mzima ana familia lakini hana akili ya kuamua masuala madogo kama haya?
Hili nalo jambo la kuomba msaada JF?
Nashukuru umegundua hilo. Wa kulaumiwa ni wazazi..watoto wa kiume wanalelewa kiajabu sana siku hizi
 
Kama nimekuelewa vizuri nakushauri badala ya mtoto wa shemeji yako kuja kwako siku za weekend na wakati wa likizo, nakushauri kaa na mtoto moja kwa moja. Mama yake yaani shemeji yako atakuwa anakuja kumuona mwanae na kwa financil support mbalimbali kama ni muhimu. Hii itasaidia wewe kumlea mtoto kwa jinsi utakavyoona inafaa kama familia.
 
we huhitaji ushauri Bali maombi.hao watoto ni ndugu kuliko ww na mwanao mtoto wa mdogo ake mkeo ni mwanao kabisa .hata huyo mtoto alikuwa atakupenda balaa mi kwa baba zangu wadogo hunambii kitu na xmas hii mtoto wa mdogo wake wife nimetuma laki aje aspendi kwangu
 
Kaka nyumba ni yako asikupangie mtu masharti kila mzazi awajibike kwa watoto wake sio unazaa unategemea wengine wakulelee afu ukiambiwa ukweli unasema watu wachoyo

Sent from my SM-N960U using JamiiForums mobile app
Wenye roho mbaya utawajua huenda na ww umekulia kwa mjomba wako lakn sasa hivi unajidai kila mtu apambane na familia yake sio poa
 
Mtoto mmoja tu wa shemeji yako unakuwa na hofu na je ingekuwa ni mtu mzima ametia timu hana mishe ingekuaje? mtoto ameletwa azoeane na mtoto mwenzake na ndio maana anamleta weekend angalau asiwe mpweke. Komaa tu upate thawabu na mtoto wako apate kampani ya mtoto mwenzake ili akili ichangamke kuliko kukaa mwenyewe tu pamoja na nyie wazazi wake tu
 
Mkuu mimi mwenyewe naswala km lako linanisumbua sana isipokiwa mi na mke wangu bado hatujapata mtoto lakini huyu dada wa mke wangu kamleta mwanae hapa na anaweza kata hata week asionekane wala kupiga simu kazi anayofanya huwa anaingia mchana sometimes usiku. Nilimwambia sometimes ukipata mda njoo umchukue mwanao then unamrudisha asubuhi ukiwa unaenda kazini duuh nilichoabulia ni matusi paka Leo hatusemeshani na huyu shemeji yangu anadai mi Nina roho mbaya na mtoto anakaa wangu. Baba wa mtoto yupo kaoa mke mwingine na anasisitiza mama wa mtoto asikae na mwanae kwasababu hapikagi na ni mtembezi. So mtoto inabidi akae kwa mama mdogo wake otherwise apelekwe kwa shangazi yake upande wa baba. Huyu mama wa mtoto hataki anadai kule anateswa sasa inabidi akae hapa. Mke wangu ana mda now tangu alipo simama kazi. Hata sielewi nifanyeje imebidi nikae tu kimya kinachoniumiza ni dharau za huyu shemeji yangu na nikikumbuka visa alivyokuwa anamfanyia mdogo wake mke wangu paka kumtimua kipindi anakaa nae kwake
Huoni kama mkeo hicho kitoto kinamliwaza pambana kitandan nawe upate wako
 
Mmmhhh hebu twende taratibu...
1. Mtoto wako/ wenu na mkeo ni wakiume

2. Mtoto wa shemeji yako ni wa kike

3. Watoto hao wanakutana siku 3 kwa wiki / kati ya siku 7

4. Muda mwingi unaombadilisha mtoto wa kiume kuiga michezo ya kike ni siku 3/7 badala ya 4/7 ambazo anakuwa nanyi baba na mama yake...!!!!?

5. Kati ya hizo siku 4 mnazokuwa nae nyie wawili, pamoja na hizo 3 anazokuwa na mtoto wa shemeji yako, ulishajaribu kukaa nao na kuwaonesha michezo ya jumla ambayo haishawishi kufata jinsia isiyo yake?

6. Ingekuwa umepata mapacha mmoja wa kike na mwingine wa kiume au una watoto 2 waliopishana mwaka ungewatenganisha michezo yao wasiigane kulingana na jinsia zao ...!!?

Mimi ni wa kike pekee kati ya watoto 7, nimecheza michezo yote ya kiume unayoijua ya utotoni kiasi mama alinichapa hadi akaacha. Alichofanya ni kunibadilishia mavazi yakawa ni vikaptura na suriali ili nisikae uchi. Na aliniambia kila kovu moja mwilini mwangu litalotokana na michezo ya kiume basi nijiandae kufinywa.

Pamoja na hayo tabia za kike nilikiwa nazo, nilijua kazi zote za kike ilipofika wakati. Mama alikuwa nami kila hatua ila kwenye michezo aliniacha na kaka zangu chamuhimu hakuruhusu tutoke nje ya geti.

Kila la kheri kwenye malezi.
Analysis nzuri, mbona sie wa analojia tumecheza rede, kuruka kamba, mdako na wakati mwingine hata kuosha vyombo tulifanya lakini mwisho wa siku ilivyofika muda wa kujielewa tukaacha mdogo mdogo
 
Back
Top Bottom