Habari wakuu mke wangu ana dada yake ambaye kazalishwa mtoto mmoja na Dada yake hayuko katika ndoa, hajaolewa na aliyemzalishaalikuja akaoa mwanamke mwingne
Sasa basi mimi na mke wangu tuna mtoto mdogo wa umri sawa na mtoto wa Dada yake..mke wangu amekuwa akimchukua mtoto wa Dada yake kila ijumaa na kumrudisha Jumapili kwa Dada yake
Sasa akiwa anataka kumrudisha mtoto hataki kurudi kwa mama yake anataka kuendelea kuishi nasi wakati huo baba wa mtoto hana muda na mtoto wake kwa mahitaji ya mtoto yaani amuhudumii
Mama wa mtoto hataki hata siku moja kumpelekea mtoto kwa baba yake sababu ana mke mwingine atamtesa Sasa amekuwa akimsukumia kwangu kwa kigezo Cha kuja kucheza na mwenzake
Je, ni sawa baba wa mtoto yupo na mama wa mtoto kukataa mtoto kwenda kwa baba kutembea kwa kisingizio Cha mama wa kambo atamtesa hivyo kuona ni sahihi aende kwa mama yake mdogo hali yakuwa baba yupo na anajichana na maisha?