Msaada: Mke wangu anataka tuwe tunaishi na mtoto wa dada yake kila wikiendi na likizo

Mkuu jaribu kuangalia tu maslahi ya huyo mtoto asiye na hatia. Kama mama'ke ana hali ngumu na wewe una nafuu ya maisha mbebe tu huyo mtoto. Ila kama mama yake ana nafuu ya maisha basi amlee mwanaye mwenyewe. Mtoto kwenda kwa baba na mama wa kambo ni very risk
 
Mkuu ushazungumzia wangu wamwingne Kama anakulia ktk tabia chafu utakubali awe mda wote na mwanao
Kuwa baba kwa watoto wote bila kujali ni wa kwako au la, inaelekea humpendi kabisa huyo mtoto mwingine..acha ubaguzi.
 
Sio tabia mbaya mkuu mtoto kashashika michezo yakike tu kwake
Acha kujitetea, wewe una roho Mbaya, huyo Mtoto Mdogo tu anakumalizia nini !?
Je ! Angekua ni Mtu mzima Ndugu ya Mkeo anataka kuishi Kwako si ungemfukuza na Mapanga !!!

Hizo unazosema kuwa Mtoto wako anacheza michezo ya Kike isiwe sababu ya kujitetea....

Acha uchoyo na roho mbaya.
 
Wanaume tujipange maana tunazidi kupungua, yani tumebaki watu wa ajabu ajabu, mtu mzima ana familia lakini hana akili ya kuamua masuala madogo kama haya?
Hili nalo jambo la kuomba msaada JF?
Nashukuru umegundua hilo. Wa kulaumiwa ni wazazi..watoto wa kiume wanalelewa kiajabu sana siku hizi
 
Kama nimekuelewa vizuri nakushauri badala ya mtoto wa shemeji yako kuja kwako siku za weekend na wakati wa likizo, nakushauri kaa na mtoto moja kwa moja. Mama yake yaani shemeji yako atakuwa anakuja kumuona mwanae na kwa financil support mbalimbali kama ni muhimu. Hii itasaidia wewe kumlea mtoto kwa jinsi utakavyoona inafaa kama familia.
 
we huhitaji ushauri Bali maombi.hao watoto ni ndugu kuliko ww na mwanao mtoto wa mdogo ake mkeo ni mwanao kabisa .hata huyo mtoto alikuwa atakupenda balaa mi kwa baba zangu wadogo hunambii kitu na xmas hii mtoto wa mdogo wake wife nimetuma laki aje aspendi kwangu
 
Kaka nyumba ni yako asikupangie mtu masharti kila mzazi awajibike kwa watoto wake sio unazaa unategemea wengine wakulelee afu ukiambiwa ukweli unasema watu wachoyo

Sent from my SM-N960U using JamiiForums mobile app
Wenye roho mbaya utawajua huenda na ww umekulia kwa mjomba wako lakn sasa hivi unajidai kila mtu apambane na familia yake sio poa
 
Mtoto mmoja tu wa shemeji yako unakuwa na hofu na je ingekuwa ni mtu mzima ametia timu hana mishe ingekuaje? mtoto ameletwa azoeane na mtoto mwenzake na ndio maana anamleta weekend angalau asiwe mpweke. Komaa tu upate thawabu na mtoto wako apate kampani ya mtoto mwenzake ili akili ichangamke kuliko kukaa mwenyewe tu pamoja na nyie wazazi wake tu
 
Huoni kama mkeo hicho kitoto kinamliwaza pambana kitandan nawe upate wako
 
Analysis nzuri, mbona sie wa analojia tumecheza rede, kuruka kamba, mdako na wakati mwingine hata kuosha vyombo tulifanya lakini mwisho wa siku ilivyofika muda wa kujielewa tukaacha mdogo mdogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…