Msaada: Mke wangu anataka tuwe tunaishi na mtoto wa dada yake kila wikiendi na likizo

Msaada: Mke wangu anataka tuwe tunaishi na mtoto wa dada yake kila wikiendi na likizo

Mtoto anakuja weekends siku za wiki yuko kwao ubaya uko wapi? Pengine mazingira aliyopo mama yake sio rafiki kwa michezo labda kuna wahuni wengi au uswahilini mno. Wewe jibaba una complain
Target ya dada mtu na mdogo mtu nikama mtoto alelewe na mdogo wake yaan kwangu ili dada mtu aweze kupata nafasi yakufanya ujasiliamali Zaid hata aweze kusafiri
 
Nakubaliana na wewe sana tu,watu wengi wanaliangalia hili suala na 'emotion'zao.Wanaona katoto kanakuja kucheza basi,wanapiga stop hapo.Lakini kuna majukumu ambayo hawayaangalii,hiyo weekend itageuka kuwa 'kila siku' na mtoto na wataanza kusema'mtoto kazoea kuja hapo' mzigo utatuwa kwa jamaa.Kama wazazi wangekuwa hawapo au hawana uwezo basi ni sawa kumchukua mtoto na kukaa nae tena ki roho safi kabisa.Lakini wapo !,aisee no way.Alafu mi huwa
Siwaelewi wazazi wanaozaa alafu kumpa mwengine ulezi,uzuri wa kuzaa mtoto uwe naye karibu,ucheze nae,ujue uzima na ugonjwa wake na mtoto ajue kama ana mzazi anaemjari.Kama haupo tayari kulea, subiri usizae.
Ndo Target ya mke wangu na Dada yake mbeleni kuwa mtoto kamzoea mwenzie akae hapa hapa maana Dada mtu anashindwa toka fanya shuguli za ujasiliamali kusafiri Hana wakumuachia mtoto na hata akitoka shule inabid akachukue wakae nae sokoni.so only solution nikumleta kwa mdogo wake
 
Kama nimekuelewa vizuri nakushauri badala ya mtoto wa shemeji yako kuja kwako siku za weekend na wakati wa likizo, nakushauri kaa na mtoto moja kwa moja. Mama yake yaani shemeji yako atakuwa anakuja kumuona mwanae na kwa financil support mbalimbali kama ni muhimu. Hii itasaidia wewe kumlea mtoto kwa jinsi utakavyoona inafaa kama familia.
Yy hataki kufanya hivyo kwa kuwa Baba mwenye mtoto yupo
 
Bado sijaona kinachomfanya mleta Uzi aonekane ana roho mbaya! Kinachoonekana watu wametanguliza hisia zao.

Mleta uzi ametupatia usuli(history) ya mtoto kuwa kila wiki anakuja na ukiliangalia hilo kwake halionekani ni tatizo kila wiki kuja.

Hata mtoto kugoma kwake si tatizo! Bali tatizo wazazi waliyomzaa mtoto wapo na wanashughuli zao na bado wanawajibika kumlea mtoto wao ila kinachoonekana majukumu hayo anataka kupatiwa yeye. Kwa sababu uono wa mleta Uzi ni kuwa hata kama wametofautiana ila bado huyo mtoto ni mtoto wao na ni wajibu wao kumlea.

Ukiangalia mtoto anagoma kuondoka itafika mahala ndo ataishi hapo mazima! Ni kama tabibu, haaangalii matokeo ya ugonjwa bali anaangalia chanzo ili atibu ugonjwa mazima. Halikadhalika kwa mleta Uzi, Sasa kugoma kuondoka kwa mtoto ina maana gharama za uendeshaji wa familia zitazidi ila ukiangalia kwa aliyeleta Uzi hayo yote kwake si tatizo bali tatizo ni kuwa hizo gharama kwake si stahiki na ndipo mazingira yatakavyokuwa huko mbeleni.

Na jamaa yupo sahihi kuwa kugharamikia si tatizo ila ni kwa nini abebeshwe mzigo hali ya kuwa mbebaji wa huo mzigo yupo na uwezo wa kuubeba wanao?

Na ukiangalia kwa undani zaidi utakuta baba wa mtoto anao uwezo wa kumgharamikia isipokuwa wanawake wana roho mbaya sana tena sana! Inawezekana anamkomoa mshikaji kwa kutomhusisha kabisa na mtoto na kwake anafanya ni kama kisasi kwa jamaa.

Hatukatai ndugu, hatukatai kusaidia! Tunachikitaka ni lazima jamii ifahamu wajibu wake na iwajibike. Tusiweke ngao ya undugu au ukaribu kwa mtu kukimbia majukumu yake. Ikiwa kama jamaa kamkataa mtoto na dada wa mkeo hana uwezo hapo sawa mtaangalia njia gani ya kuweza kumsaidia. Kama uwezo anao mta share gharama.
Mkuu hakika wewe umenielewa vizur Sana..lengo lao mbeleni mtoto ahamie moja kwa moja maana ilishaanza ishara yakuwa watoto wamezoeana Sana so pia dada mtu pia shuguli zake hazifanyi kwa Uhuru sababu yamtoto Hana wakumuachia kumuangalia awapo ktk mihangaiko take analazimika awe nae Hilo ktk mihangaiko yake Hali baba wamtoto yupo nashuguli zake zakumpatia rizki hana habari
 
Hivi bado tuko kwenye primitive communalism? Why tumlazimishe mtu kua na roho ambayo hanayo? Maisha yamebadilika may be kuna risk anaiona mbeleni kwa kukaa na huyo mtoto..sema maisha yetu ya kiswahili kaazi kweli! Unamlazimisha mtu akusaidie[emoji2][emoji2]
 
Umeongea vizuru sana,ila bado kuna mijitu itatokea itarudi na kusema,jamaa ana roho mbaya.
Mkuu ww na bwana hammaz mmenielewa vizur Sana anachokieleza bwana hammazi ndio kinachoonekana kuja kutokea kwangu hapo mbele ya safar maana Kuna dalili naziona wazi
 
Anaefaidika hapa ni mwanao zaidi, watoto waliopekeyao wanakuwa wapweke sana na wanafurahi sana wanapopata watoto wenzio wa kucheza nao.

Mkeo anaakili sana na utu wala hata hutakiwi kuhoji vitu kama hivyo zaidi unapaswa kumjali kama mwanao.

Maisha haya tunapita ukiweza kusaidia mtu mzima acha mtoto fanya tu inakusaidia na kukuongezea riziki maana mtoaji anaona una majukumi mengi zaidi.

Wengine wanahangaika mpaka kuadopt wewe unae tena ndugu bado unajiuliza.
Mkuu unachokiongea upo sahihi Ila lengo lamke liko kwingne kabisa lengo nikumfanya mtoto wangu asiweze kuishi bila mtoto wa Dada maana yake wazoeane Zaid kiasi chakumfanya aweze kuhamia moja kwa moja kumlea kwaminajili ya kuzoeana Sana namtoto wetu
 
Mkuu hakika wewe umenielewa vizur Sana..lengo lao mbeleni mtoto ahamie moja kwa moja maana ilishaanza ishara yakuwa watoto wamezoeana Sana so pia dada mtu pia shuguli zake hazifanyi kwa Uhuru sababu yamtoto Hana wakumuachia kumuangalia awapo ktk mihangaiko take analazimika awe nae Hilo ktk mihangaiko yake Hali baba wamtoto yupo nashuguli zake zakumpatia rizki hana habari
Kuzaa azae yeye malezi na matunzo ya mwanae awabwagie nyie?! Hebu mwambieni na nyie mumkabidhi watoto wenu mwambieni hatuna wa kumuachia tunapokuwa kwenye mihangaiko yetu.

Aongee na bwana wake aliyemzalisha waangalie hiyo changamoto wataitatua vipi! Au achukue ndugu atakaye kuwepo kwake muda wote wa kumuangalia mwanae.

Asitafute uhasama usio na sababu.
 
Kwa tabia za masingle mother hawa, hapo ameshampanga mdogo wake kisaikolojia umsaidie kulea, wao ni kama incubators, kutotolesha watoto malezi sifuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Kabisa, halafu mbaya zaidi amevunja kabisa bond kati ya mtoto na baba yake kisa mama wa kambo. Huyo mtoto kuna kipindi akianza kujitambua ataanza kutaka kujua baba yake yuko wapi? Maana atakuwa anaona na kusikia wenzake wakijivuna na kuwaongelea mama na baba zao. Nachukia sana mijanamke ambayo ugomvi wao na waliozaa nao wanauhamishia kwa watoto. Sitashangaa akizalishwa mtoto wa pili na kumsukumia tena mdogo wake huku yeye anakula bata..

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Mkuu ushazungumzia wangu, wa mwingine kama anakulia katika tabia chafu utakubali awe muda wote na mwanao
Mkuu mimi nakuelewa sana, komaa huyo single mother abebe mzigo wake... Hizo week ends ampeleke mtoto kwa baba yake ili mtoto amzoee baba yake na baba yake awajibike kimatunzo na malezi. Kwa maelezo yako huyo single mother Hana time kimalezi hivyo mtoto anaiga tabia za hovyo huko mtaani kwao na sasa anazileta hapo kwa mtoto wako, jambo hilo ni hatari baadae.

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Wanaume ndo mnaproduce masingle mothers so saidianeni kulea, nini sasa mnalalamika?
Na huyo single mother aendelee kula bata na kutotoa wengine na kumtupia shemeji siyo? Kwa nini weeks ends asimpeleke kwa baba yake mzazi? Huyo mtoto wa miaka 6 kweli hana hamu na baba yake?

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Kulea mtoto ambaye unajua baba yake yupo anazungusha mbupu mjini hapa ni ujinga kabisa,linahitaji moyo sana..labda tu iwe huyo baba ana matatizo yanayofanya ashindwe kuhudumia.

Waafrika especially wabongo tunapenda kubebesha watu mizigo isiyowahusu..no wonder nchi yetu ipo karibia mkiani kwenye list za nchi na furaha duniani
Well said, halafu mtoto ananyimwa haki ya kwenda kwa baba yake mzazi eti kisa anaenda kwa shemeji. Na unaweza kukuta baba ya mtoto amechuna kwa sababu alimwambia mama amlete mtoto hataki au anasingizia mtoto yuko kwa shemeji yangu, hata ukija nyumbani hutamkuta. So jamaa naye kwa hasira kuchuna tuu... Lakini mimi bado nasema mtoto anakoseshwa haki ya kumuona baba yake kwa ujinga tuu wa huyo single mother.

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Kwani walimzalia yeye mambo ya kuzaa kwenu kuje kutusumbua ndugu huo ubwege haukubariki.Mapenzi mfanye nyie miuno mkate nyie akitokea mtoto mniltee alooo tutatafutana ubaya.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Mtoto kuja tu weekend ndio imekuwa nongwa dah wabongo siku hizi bajet imekuwa kali sana.
Kwani hata gemu si huwa tunawaambia naomba niingize kichwa tuu, akikubali anastukia breki ni zile tenesi mbili [emoji23] [emoji23] [emoji23] so anaanza week end baadae analala siku kadhaa mwishowe kahamia jumla.

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Mama mtu nikama anataka jukumu lakumlea mtoto liwe kwake tu yaan mtoto asihusishwe na upande wababa mtoto aendelee kukua kwaupande kwakila kitu Hali baba yuhai na anamke na anashuguli zake zakumuingizia rizki
Anajidanganya tuu huyo single mother, mtoto akifika 15 yrs plus ataanza ku force kwenda kwa baba yake, apende asipende...

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Mambo kama haya hukaribisha umaskini sana ktk familia zetu za kimaskini, hii tabia imenikosti sana.
Kuna watu hapa watasema kwani sh ngapi lkn hawajui chochote kile ni gharama hata kama ni sh 100. Mjue tu bajeti ya familia haiwezi kua ileile

Mkuu nakuelewa sana
Yaani umaskini usababishwe na mtoto wa miaka 6? Kwa kipi hasa?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom