Msaada: Mnaopenda kula mboga za majani, mlifanyaje, mbona mimi nateseka?

Iko wapi hiyo dinner mbona mi sioni chakula apo naona mboga tu? Hilo jani nalo ni sehemu ya chakula au ni urembo tuu? Au ugali upo kwa pembeni?
Huto tuvitu nimekula tunne ndiyo dinner hiyo. Hilo jani ni chakula na ugali siruhusiwi kula 😭
Nikisema nateseka, namaanisha
 
Siri ipo kwenye uungaji kama unaunga kivivu zitakuwa kama dawa hutazila.

Mboga za majani weka nyanya, kitunguu, karanga kama una nazi tia kidogo.

Usiweke mafuta kama itabidi weka kidogo ya alizeti.
Binafsi napenda sukumawiki zile za kenya, chainizi, mgagani, majani ya kunde, mlenda & bamia, sipendi tembele na kisamvu navichukia kiufupi 🙁
 
Kwa ukubwa wa ilo jani lilivo ukifanikiwa kulila na ukianza kuzowea siku ukiamua kwenda sehemu zinazolishwa wanyama itabidi uende na msimamizi wako maana unaweza kupewa majani umlishe mnyama ukajikuta unayafakamia wewe.
Ujuwe nilijua upo zenji kulisha kobe
 
Mpwa wangu mie, asante 😍 ngoja niviweke kwenye list nitajaribu!
 
Kama utakula majani tu kama wanyama (sorry)
Basi hutafaidi mboga mboga na salad hata siku moja

Uzuri leo bila kuuliza mtu unaweza kutengeneza mwenyewe vyakula vya aina 70 vya vegetarian kwa kupitia mitandao

Unaweza kutengeneza hata supu za aina tofauti kila siku na uka enjoy tu
Hebu angalia milo hiyo simple ya veg tupu
 
Huku kucheka nilikocheka lazima kuna hata kilo moja imepungua 🤣 🤣 🤣 , acha kesho nijipongeze hata na nusu chapati daaaaahhhhh.
 
Hiyo njia ya kula protein ( ketogenic diet) ni njia ya kishamba ( unapunguza uzito haraka ila sio ya uhakika , rapid but not sure)

Punguza uzito kwa kupunguza ulaji wa vyakula vya wanga na mafuta sio kuacha kabisa

Unaweza ukaacha kula wanga maisha yako yote? Hapo ukila wanga kidogo tu uzito unarudi
 

Asante kwa recommendation, huwa naangalia recipe online. Changamoto ni kuenjoy hivi vyakula.
Ila nitaongeza kwenye list yangu na kuvijaribu pia hivi ulivyoshare.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…