Msaada: Mnaopenda kula mboga za majani, mlifanyaje, mbona mimi nateseka?

Msaada: Mnaopenda kula mboga za majani, mlifanyaje, mbona mimi nateseka?

Zingatia: Hii ni nyuzi serious, haihitaji utani wala dhihaka. Kama huna ushauri, endelea kuperuzi kwenye majukwaa mengine.

Mwezi uliopita niliandika uzi wa kuomba ushauri na msaada wa kupunguza uzito.

Nimefuata ushauri na kumpata mtaalamu wa lishe, amenitengenezea mpango wa chakula na inabidi nisile vyakula vya wanga, nile protein na mbogamboga kwa wingi.

Changamoto: Hivi vyakula vya majani majani vinanikosesha raha maana nilizoea chapati, wali, ugali, viazi wala vyakula vya ngano. Mnaopenda mboga za majani au ambaye alipitia hii process ya kujilazimisha kuzila, ulifanyaje?

Hiyo hapo chini ni dinner yangu ya leo (nakula hivyo vidude vinne) ila najionea tabu tu. Nisaidieni mawazo na mapishi / recipe nzuri kwa ambao mnafahamu.

View attachment 3274305

Cc:
Mwachiluwi kwa recipe ideas

na

makutupora
realMamy
Nomadix
Mallerina
bonjov
For emotional support 😌 mje mnifariji napitia magumu 😂😂
Mimi nilishauriwa hivyo hivyo,mwanzo inakuwa ngumu lakini pole pole utazoea.
Chemsha ndizi weka hizo mboga za majani na nyanya na vitunguu maji/swaumu,usiweke mafuta kabisa chumvi kwa mbali. Uwe unabadili mboga ktk huo mchanganyiko wa ndizi za kuchemsha na mboga ziwe nyingi utaona matokeo mazuri.
Kwangu imenisaidia sana na nimepunguza nyama nyekundu. Uzito unaumiza sana miguu.
 
Nikiitengeneza hii ndio inakuwa msosi wa usiku
 

Attachments

  • Screenshot_20250118_120312_Facebook.jpg
    Screenshot_20250118_120312_Facebook.jpg
    372.5 KB · Views: 10
Ooh
Kuzipenda mboga za majani inategemea na chanzo chake imean zinatoka wapi na unazila na Nini kuzipa radha ya kuvutia

Anza kuzilima mwenyewe kwenye eneo lako,hata kama ni kwenye makopo,chinese zinastawi, unamwagia maji safi na unakua Imaninazo sana kuzila unapozipika kwa kupasha joto tu ukichanganya na viungo vingine

Imagine unauziwa mboga kumbe zimetoka kunyeshewa maji ya mtaroni Au bonde la msimbazi.

Pakiti ya hizi mbegu za ni bei ndogo haizidi elfu 10, na utatumia Mwaka mzima. Unaweza una na sukuma wiki,pia

Hapa chini ni majani ya kunde nimepanda na yamwagilia kwa maji ya bomba so nakula nikiwa na uhakika yametoka wapi
Asante sana 🙏
 
Back
Top Bottom