Msaada: Mpenzi wangu sio mwaminifu ila kila nikimwambia tuachane analia

Msaada: Mpenzi wangu sio mwaminifu ila kila nikimwambia tuachane analia

pascal luoga

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2019
Posts
233
Reaction score
264
Habari wakuu wote ndani ya jukwaa hili la mahusiano na kwingineko pia, naimani wote mu wazima wa afya. Bila kuchelewa naomba niende moja kwa moja kwenye maada

Iko hivi, nina mpenzi wangu ambaye niko naye kwenye mahusiano mwaka wa 3 sasa. Yeye anaishi kwao mimi pia naishi kwetu ila najikuta kuna vtu vinanifanya nisimwamini hata siku moja na mpaka sasa bado simwamwini mwaka wa tatu sasa.

Shida alizonazo ni kwamba kwa miaka yote hii mitatu mwaka jana mwanzoni nilikuja kugundua kwamba anatoka na marafiki zangu wawili kwa wakati mmoja na alikuwa anafanya siri, baada ya kuchunguza na kufahamu sikumwambia nikakaa kimya kilichokuwa kinanitatiza ni kwamba mbona anaonesha kunisaliti lkn nikimtizama naona ananipenda kwa upendo wa dhati kabisa, ninachomwmbia anafuata, ananiheshimu, yani ana ishara zote zile za mapenzi ya dhati kwangu.

Nikapotezea ila kilichokuwa kinaniumiza ni kwamba ndiyo ana mapenz ya dhat kwangu ila kwann ana mahusiano pia nje? ... Baadae nikaja kumwambia naomba tuachane... Alilia huku anaomba msamaha kwamba hatorudia. Nikaja nikamsamehe (wale rafk zangu aliachana nao sasa sifahamu kwamba aliacha ama aliachwa? Maana rafiki zangu hao pia walisema kwamba hawamwelewi)

BALAA LINAPOANZIA
KUNA Vitu vinanitatiza sana Pia kwake.
  1. Kwa kipindi chote hiki cha mahusiano kinachonitatiza ni kwamba siku zote ambazo tumewai kutoka ama tunazokuwa tuko out, SIMU yake huwa haitoi kwenye pochi hata siku moja yaani unaweza kutana naye sehemu ya appoinment mnakaa mnaongea mpka mnaondoka simu yake haitoi.
  2. Appointment mpaka upange wewe yeye hajawai kuniambia hata siku moja, siku nyngne unapanga ila kwake excuse zinakuwa nyingi.
  3. Huwaga namtumia kifurushi cha sms cha mwezi cha sms 1000 , lkn cha ajabu ukichat naye dk 2 tu anakwmbia yuko BUSY, na kwa siku mnaweza kuta mnachat sms 10 tu kisingizio chake yuko busy na usiku anasema analala mapema sabb ya uchovu. KINACHONIUMIZA ndani ya wiki 2 anasema sms zimeisha zote 1000 wakati huwa hatuchat sana kwa kisingizio cha UBUSY, sasa je hizo sms 1000 zinaishije?

LICHA YA VYOTE HIVYO
SIKU UKIMWAMBIA TUACHANE ANALIA NA KUOMBA MSAADA KWA RAFIKI ZANGU WAMSAIDIE KUOMBA MSAMAA KWANGU

SASA JE! KUNA MPENZI HAPA!

Naombeni mnisaidie mbinu za kumuacha huyu msichana sabb nikisema kwa sasa kwmba ananisaliti ushahidi sina sabb smu yke sishiki na huwa haitoagi mbele yangu.

MSAADA WAPENDWA NIWEZE KUONDOKANA NA HII LAWAMA...

NAHITAJI KUMUACHA, JE NITUMIE MBINU GANI?
 
Pole sana mtoa mada..

nakushauri achana na huyo mwanamke na pia
usikubali kumpa chance ya pili hata akitoa machozi kwani hata wezi wanalia

afu wanawake ni wepesi kusoma saikolojia ya mtu. kwamba amejua mapungufu/udhaifu wako na ndio anamo pitia mule mule..!

pia kapime kujua afya yako
 
Nipe number yake ni mkanye, karipio moja kali ataacha
 
Naombeni mnisaidie mbinu za kumuacha huyu msichana sabb nikisema kwa sasa kwmba ananisaliti ushahidi sina sabb smu yke sishiki na huwa haitoagi mbele yangu.
Nimekoma ubishi wangu, na hatimae leo nakiri hadharani kwamba uchawi kwenye mapenzi upo!!!

Yaani mtu anatafuta namna ya kuacha girlfriend with evidence pamoja na kuamini anagongwa na washikaji?!

We bhana sikiliza! In short huna ubavu wa kuacha demu, kwahiyo we endelea tu kugongewa manake hata ukijifanya kuacha, in two weeks utaenda kuomba msamaha as if we ndo mkosaji!

Halafu juzi niliuliza hapa jamvini lakini sikupata jibu! Hivi kwanini hapa JF ni wanaume ndo tunaongoza kulia lia habari za mapenzi?!
 
Unahitaji Ushauri wakati kwa maelezo yako ni kwamba hakutaki? Hiyo kuonyesha wanatupenda ni anafanya danganya toto tu. Ukiendelea naye yapo mambo makuu mawili 1. Hasara ikukamate umuue au 2. Wewe Ujiue. Wanawake wako wengi ambao Mungu atakupa ubavu unao fit. Huyu atakuua kwa stress. Yaani enzi ZANGU nijue tu mtu anatia shaka. Yaani in no time nakufutilia mbali.
 
Back
Top Bottom