Asante. Vp kuhusu maziwa ya kopo nielekeze kidogo
Yapo maziwa lishe maalumu kwaajiri ya watoto ambao aidha mama amefariki au ana matatizo ya kiafya ambayo yatamfanya ashindwe kunyonyesha.
Sasa mkeo hana shida yoyote ni lishe tu hapo ndio anafeli. Mtoto wa kiume huwa ananyonya sana so sio mchezo mchezo kumkuza hadi atapoacha kunyonya.
Fanya hivi, mtengenezee uji wa lishe mkeo ili aweze kutengeneza maziwa mtoto anyonye hadi akinai. Huo uji uweke nafaka hizi. Mahindi lishe ukikosa hata mahindi ya kawaida yatafaa, ngano, ulezi, mihogo, soya maziwa au soya lishe, mchele, mbegu za maboga, karanga, ufuta na mtama.
Hizi nafaka utaweka kwa ratio tofauti sio kwa kiwango sawa. Yaani kwa mfano huwezi kuweka zote zikawa kilo moja moja bali utazingatia ujazo wa jumla unaotaka kutengeneza kisha utagawa ratio kulingana na kilo za jumla. Mfano utataka kutengeneza kilo 30 za unga kwajiri ya uji then unaweza fanya kilo tano ni za mahindi lishe, kilo 2 ni za mchele, tatu ni za ulezi, kg mbili ni za mbegu za maboga, 3 za ufuta, kuendelea. Mimi nimeweka rough estimate hapo ila upangiliaji wa nafaka na kiwango cha kilo zake unatakiwa kuzingatia kwanza nafaka inalenga nini maana uji wa lishe wa mwanamke anayenyonyesha ni tofauti na uji wa lishe wa mtoto na pia ni tofauti na uji wa lishe wa mwanaume anayejenga mwili wake.
Mtoto anahitaji sana nafaka zenye protein kama karanga, soya lishe, mahindi lishe, ngano, na hizo zingine zinawekwa kubalance tu lishe kumpa mahitaji mengine ya virutubisho na madini muhimu.
Ukija mwanamke anayenyonyesha, atahitaji zaidi ujazo wa nafaka zenye kiwango kikubwa cha material ya chokaa au wanga na vingine vya kuzalisha maziwa kama mchele, mahindi ya kawaida, mihogo, karanga, ufuta, mtama, na hizo nyingine zinamuongezea zaidi nguvu ya mwili katika kuhimili mikiki wakati ananyonyesha. Pia usisahau kumpa gemu la kutosha mwanamke anayenyonyesha akiwa na furaha bila stress maziwa huwa hadi yanachuruzika kama chemchem.
Kwa mwanaume lishe yake kwenye uji mahitaji yatakuwa tofauti sana atahitaji kulingana na ana malengo gani kama ni kutengeneza sana mbegu za kiume na kuongeza nguvu za kufanya mapenzi then lishe yake inataka ratio balance ya tofauti na kama anataka kujenga mwili kwa maana kunenepsha mwili kama yupo chini ya uzito unaotakiwa. Ila pia kama anataka kubalance vyote pia inawezakana.
Ila huu uji unakuwa mtamu zaidi ukipikwa kwa kuweka nazi badala ya maji wakati wa kuuchemsha nazi au maziwa ya ng'ombe ambayo hayajatiwa maji kwa maana kuchakachuliwa. Na ukishaweka mezani unaweza kuweka siagi ya karanga uji unakuwa ni mzito sana , mtamu sana , unashibisha sana na unafanya kazi yake ipasavyo.