Msaada: Mtoto ananyonya sana

Msaada: Mtoto ananyonya sana

Kiongozi
Inaelekea mama hana maziwa ya kutosha. Jitahidi mama ale vitu vya kumuongezea maziwa.
Kama bajeti haiko vizuri kununua hayo maziwa ya formula, Mwanzishie maziwa ya ngombe (una weka nusu maziwa na nusu maji) mf: unachanganya kikombe kimoja maziwa na kikombe kimoja maji ili yawe mepesi kabisa. Na ikiwezekana upate mtu mwenye ngombe kabisa ili akupe maziwa ya ngombe mmoja (asibadilishe badilishe ngombe) wafugaji wanajua ukimwambia maziwa ya mtoto
Akinywa hayo maziwa yaliyo changanywa na maji akiteremshia na ya mama atakuwa poa kabisa.....
Miezi mitatu inaweza kumsababishia matatizo mtoto, Maziwa ya ng'ombe kabla ya umri wa miezi 12 inaweza kumuweka mtoto hatarini mf.-kutokwa na damu ndani ya utumbo . Pia ina protini nyingi na madini ambayo ni ngumu kwa figo za mtoto mchanga kuchuja kwa urahisi na haina kiasi sahihi cha virutubisho kwa mtoto. At least miezi 9 kwa kufosi lakini sio salama risk ni kubwa
 
Habar

Ndugu zangu nina mtoto wa kiume wa miezi 3 ananyonya sana mpaka mama yake anachoka na hashibi, ukimtoa analia.

Na clinic wameshaur mtoto anyonye tu maziwa ya mama hadi afikishe miezi 6

Nini naweza kufanya kumsaidia mtoto na mamake?
Yaani unataka asinyonye sana ili mama yake aende wapi,kudanga?

Yaani suala la mwanaume kula kiume mwanaume wa Dar Es salaam unataka ushauri wa kitabibu?

Nakushauri umwambie mkeo asimnyonyeshe huyo mtoto ili asichoke.
 
Bila Shaka huyo mtoto ni wa kiume, huwa wananyonya hao....halafu Baba Kama una wivu vile kila saa kidume kinaning'inia kwenye nyonyo ya nkeo🤣🤣🤣
Yaani nimeona huyu hahitaji ushauri bali makanyo.

Kwa nini wana zaa kabla ya kupevuka?

Yaani hajui ulaji wa mtoto wa kiume na sisi wanaume kiujumla?

Au kwakuwa yeye anaishia kula chips basi anadhani ndo ulaji wa mwanaume?

Bahati yake siyo kijana wangu,ningempiga makofi mbele ya mke wake.
 
Habar

Ndugu zangu nina mtoto wa kiume wa miezi 3 ananyonya sana mpaka mama yake anachoka na hashibi, ukimtoa analia.

Na clinic wameshaur mtoto anyonye tu maziwa ya mama hadi afikishe miezi 6

Nini naweza kufanya kumsaidia mtoto na mamake?

Ndio mama yake ale sana pia ili asichoke

Mtoto anyonye maziwa ya mama tuu miezi6
 
Aptamil 70,000 2weeks

Mama ale vyakula bora apate maziwa mtoto anyonye

Apate pia maji ya madafu, oats na nazi isikose kwenye chakula chake

Awe na matunda au snacks baada ya mlo
Kwa life la kawaida mtu kutoa 70k kila baada ya 2weeks sio mchezo wakuu. Bora hizo lactogen 20+k, au hata sma 45k ila dawa ni mama kula healthy maziwa yatoke. Hizo formula iwe kwa kuongezea kidogo tu.
 
Vp kuhusu maziwa ya ngombe au hayafai pia
Kwani huyo ni mtoto wa ng'ombe hadi anyonye maziwa ya ng'ombe?!

Huyu maziwa yana hormones ndani yake sasa unataka mtoto wako awe na tabia za ng'ombe katika Gene zake?
 
Kiongozi
Inaelekea mama hana maziwa ya kutosha. Jitahidi mama ale vitu vya kumuongezea maziwa.
Kama bajeti haiko vizuri kununua hayo maziwa ya formula, Mwanzishie maziwa ya ngombe (una weka nusu maziwa na nusu maji) mf: unachanganya kikombe kimoja maziwa na kikombe kimoja maji ili yawe mepesi kabisa. Na ikiwezekana upate mtu mwenye ngombe kabisa ili akupe maziwa ya ngombe mmoja (asibadilishe badilishe ngombe) wafugaji wanajua ukimwambia maziwa ya mtoto
Akinywa hayo maziwa yaliyo changanywa na maji akiteremshia na ya mama atakuwa poa kabisa.....

Simshauri
Siku hizi ng’ombe wanakula sindano na mtu Kesho anakamua anakuuzia
 
Asante. Vp kuhusu maziwa ya kopo nielekeze kidogo
Yapo maziwa lishe maalumu kwaajiri ya watoto ambao aidha mama amefariki au ana matatizo ya kiafya ambayo yatamfanya ashindwe kunyonyesha.

Sasa mkeo hana shida yoyote ni lishe tu hapo ndio anafeli. Mtoto wa kiume huwa ananyonya sana so sio mchezo mchezo kumkuza hadi atapoacha kunyonya.

Fanya hivi, mtengenezee uji wa lishe mkeo ili aweze kutengeneza maziwa mtoto anyonye hadi akinai. Huo uji uweke nafaka hizi. Mahindi lishe ukikosa hata mahindi ya kawaida yatafaa, ngano, ulezi, mihogo, soya maziwa au soya lishe, mchele, mbegu za maboga, karanga, ufuta na mtama.

Hizi nafaka utaweka kwa ratio tofauti sio kwa kiwango sawa. Yaani kwa mfano huwezi kuweka zote zikawa kilo moja moja bali utazingatia ujazo wa jumla unaotaka kutengeneza kisha utagawa ratio kulingana na kilo za jumla. Mfano utataka kutengeneza kilo 30 za unga kwajiri ya uji then unaweza fanya kilo tano ni za mahindi lishe, kilo 2 ni za mchele, tatu ni za ulezi, kg mbili ni za mbegu za maboga, 3 za ufuta, kuendelea. Mimi nimeweka rough estimate hapo ila upangiliaji wa nafaka na kiwango cha kilo zake unatakiwa kuzingatia kwanza nafaka inalenga nini maana uji wa lishe wa mwanamke anayenyonyesha ni tofauti na uji wa lishe wa mtoto na pia ni tofauti na uji wa lishe wa mwanaume anayejenga mwili wake.

Mtoto anahitaji sana nafaka zenye protein kama karanga, soya lishe, mahindi lishe, ngano, na hizo zingine zinawekwa kubalance tu lishe kumpa mahitaji mengine ya virutubisho na madini muhimu.

Ukija mwanamke anayenyonyesha, atahitaji zaidi ujazo wa nafaka zenye kiwango kikubwa cha material ya chokaa au wanga na vingine vya kuzalisha maziwa kama mchele, mahindi ya kawaida, mihogo, karanga, ufuta, mtama, na hizo nyingine zinamuongezea zaidi nguvu ya mwili katika kuhimili mikiki wakati ananyonyesha. Pia usisahau kumpa gemu la kutosha mwanamke anayenyonyesha akiwa na furaha bila stress maziwa huwa hadi yanachuruzika kama chemchem.

Kwa mwanaume lishe yake kwenye uji mahitaji yatakuwa tofauti sana atahitaji kulingana na ana malengo gani kama ni kutengeneza sana mbegu za kiume na kuongeza nguvu za kufanya mapenzi then lishe yake inataka ratio balance ya tofauti na kama anataka kujenga mwili kwa maana kunenepsha mwili kama yupo chini ya uzito unaotakiwa. Ila pia kama anataka kubalance vyote pia inawezakana.

Ila huu uji unakuwa mtamu zaidi ukipikwa kwa kuweka nazi badala ya maji wakati wa kuuchemsha nazi au maziwa ya ng'ombe ambayo hayajatiwa maji kwa maana kuchakachuliwa. Na ukishaweka mezani unaweza kuweka siagi ya karanga uji unakuwa ni mzito sana , mtamu sana , unashibisha sana na unafanya kazi yake ipasavyo.
 
Yaani nimeona huyu hahitaji ushauri bali makanyo.

Kwa nini wana zaa kabla ya kupevuka?

Yaani hajui ulaji wa mtoto wa kiume na sisi wanaume kiujumla?

Au kwakuwa yeye anaishia kula chips basi anadhani ndo ulaji wa mwanaume?

Bahati yake siyo kijana wangu,ningempiga makofi mbele ya mke wake.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] vijana na mabinti wa siku hizi ni hopeless kabisa especially eneo la uzazi. Kuna siku namsikia mdogo wangu (mtoto wa kike wa mama yangu mdogo) anaongea na mwenzake kwenye simu anamuomba ushauri huyo mwenzake juu ya mtoto kuwa na kwikwi na kucheua maziwa kama anatapika. Huyo mwenzake kwenye simu anamwambia achukue majani gani sijui amuogeshee mtoto kisha hiyo hali itaisha.

Ninasubiria wamalize kuongea nikaanza kumsema kwa uzembe wake wa kutokujifunza kuwa mtoto huwa anacheuwa na kupatwa na kwikwi kama matokeo ya uzembe wa mama yake kufeli kumuweka begani abeuwe baada ya kunyonyeshwa.
 
Kama hela ipo nunua lactogen ya wachanga wa umri wake au uji mwepesi sana wa mhogo. Shibe kwa mtoto muhimu sana
 
Back
Top Bottom