Msaada mtoto wa miezi 6.5 hatambai wala kumove

Usiwe na mawazo sana kweli ilibidi aanze kutambaa
Ingawa baadhi ya watoto wanapata delayed developmental milestone
Muhimu ni kujua kama ana shida yoyote alizaliwa nayo
Vinginevyo kua na subira sio mara zote ukuaji wa mtoto unaenda sawa na wengine
Amezaliwa Hana shida yoyote Hadi Sasa Hana dalili ya shida yoyote Ile labda akachunguzwe
 
Jaribu huwe unamfanyia mazoezi ya viungo muhimu ni kusimama na kutembea.. mtoto wangu alisimama na kutembea hatua ya kutambaa hakuipitia..
 
Hii ndo maana ya jungukuu halikosi ukoko basi uzi ufungwe
 
Acha kufanya ngono hovyo...
Unaharibu mtoto

Unambemenda
 
Amezaliwa Hana shida yoyote Hadi Sasa Hana dalili ya shida yoyote Ile labda akachunguzwe
Basi relax ni kawaida hio nmeona watoto wengi wenye delayed developmental milestone na wakaja ku catch vizuri
 
Inasemekana baadhi ya wajawazito wanakataa kumeza baadhi ya vidonge vya kuongeza madini mwilini kiasi cha kusababisha virutubisho kwa mtoto atakaye zaliwa. Sina ushahidi wa kisayansi....lakini sababu hii inatolewa huko mtaani
 
Ukuaji wa watoto hutokea kwa hatua mbalimbali. Hata hivyo kuna tofauti toka mtoto mmoja hadi mwingine, kuna ambao ukuaji huja pole pole na wengine haraka ktk umri fulani.

Kwa mwanao wa miezi 6 ni wazi kwamba bado anahudhuria kiliniki kwa ajili ya kupata chanjo na kuangaliwa hali ya ukuaji wake (uzito, mwonekano kwa ujumla). Kama ana ukuaji hafifu utaonekana tu.

Kwa hiyo ukuaji kwa watoto hutokea kwa mwendo tofauti kwa kila mtoto. Kama mwanao hakupata shida yoyote baada kuzaliwa basi usiwe na shaka.

Utakapompeleka kiliniki yake inayofuata fika pia kwa daktari ili amuone ili akushauri zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…