Msaada mtoto wa miezi 6.5 hatambai wala kumove

Msaada mtoto wa miezi 6.5 hatambai wala kumove

Usiwe na mawazo sana kweli ilibidi aanze kutambaa
Ingawa baadhi ya watoto wanapata delayed developmental milestone
Muhimu ni kujua kama ana shida yoyote alizaliwa nayo
Vinginevyo kua na subira sio mara zote ukuaji wa mtoto unaenda sawa na wengine
Amezaliwa Hana shida yoyote Hadi Sasa Hana dalili ya shida yoyote Ile labda akachunguzwe
 
Jaribu huwe unamfanyia mazoezi ya viungo muhimu ni kusimama na kutembea.. mtoto wangu alisimama na kutembea hatua ya kutambaa hakuipitia..
 
Namuwekea kitu anataka haswa ili ajisogeze kukifata? Hii ni afajisukuma na kuwa anapiva mweleka pole pole atafika.

Natumaini anaweza ku move na kujigeuza akiwa umemlaza. Kama sio basi kuna tatizo.

Je, anaweza kujaribu kujinyanyua anyanyuke labda kwa kusikiliza meza au kitu ili asimamie?

Kuhusu kutambaa na ukuaji, kila mtoto ana muda wake ila kuna kitu hisia za Mama sasa hapo ni kufikiria na kuchukua hatua.

Najua kuna watoto wanakuaga fasta hawatambai bali watakuja kusimamia na kutembea.

Mafupi yangu ni hayo.
Hii ndo maana ya jungukuu halikosi ukoko basi uzi ufungwe
 
Acha kufanya ngono hovyo...
Unaharibu mtoto

Unambemenda
 
Inasemekana baadhi ya wajawazito wanakataa kumeza baadhi ya vidonge vya kuongeza madini mwilini kiasi cha kusababisha virutubisho kwa mtoto atakaye zaliwa. Sina ushahidi wa kisayansi....lakini sababu hii inatolewa huko mtaani
 
Habari wakuu nimekuja kwenu kutaka mawazo bint yangu wa Umri miezi 6.5 hatambai ukimuweka hata kujaribu kumove hamna... anakua kama anataka kujivuta hawezi kabisa kumove Wala kutambaa. Nimekuja kwenu kutaka ushauri nini chakunya aweze kutambaa kumove na kusimama.

Naaambiwa kuwa na watu kwa umri wa miezi sita alitakiwa awe ameanza kutambaa, msaada wenu wakuu.
Ukuaji wa watoto hutokea kwa hatua mbalimbali. Hata hivyo kuna tofauti toka mtoto mmoja hadi mwingine, kuna ambao ukuaji huja pole pole na wengine haraka ktk umri fulani.

Kwa mwanao wa miezi 6 ni wazi kwamba bado anahudhuria kiliniki kwa ajili ya kupata chanjo na kuangaliwa hali ya ukuaji wake (uzito, mwonekano kwa ujumla). Kama ana ukuaji hafifu utaonekana tu.

Kwa hiyo ukuaji kwa watoto hutokea kwa mwendo tofauti kwa kila mtoto. Kama mwanao hakupata shida yoyote baada kuzaliwa basi usiwe na shaka.

Utakapompeleka kiliniki yake inayofuata fika pia kwa daktari ili amuone ili akushauri zaidi.
 
Back
Top Bottom