Msaada mtoto wa miezi 6.5 hatambai wala kumove

Msaada mtoto wa miezi 6.5 hatambai wala kumove

malembeka18

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2018
Posts
3,266
Reaction score
3,698
Habari wakuu nimekuja kwenu kutaka mawazo bint yangu wa Umri miezi 6.5 hatambai ukimuweka hata kujaribu kumove hamna... anakua kama anataka kujivuta hawezi kabisa kumove Wala kutambaa. Nimekuja kwenu kutaka ushauri nini chakunya aweze kutambaa kumove na kusimama.

Naaambiwa kuwa na watu kwa umri wa miezi sita alitakiwa awe ameanza kutambaa, msaada wenu wakuu.
 
Usiwe na mawazo sana kweli ilibidi aanze kutambaa
Ingawa baadhi ya watoto wanapata delayed developmental milestone
Muhimu ni kujua kama ana shida yoyote alizaliwa nayo
Vinginevyo kua na subira sio mara zote ukuaji wa mtoto unaenda sawa na wengine
 
Habar wakuu nimekuja kwenu kutaka mawazo bint yangu wa Umri miez 6.5 hatambai ukimuweka hata kujaribu kumove hamna...anakua kama anataka kujivuta hawezi kabisa kumove Wala kutambaa...nimekuja kwenu kutaka ushauri nin chakunya aweze kutambaa kumove nakusimama ....naaambiwa kuwa nawatu kwa umri wamiez sita alitakiwa awe ameanza kutambaa ...msaada wenu wakuu
Wacha wasiwasi. Siyo lazima watoto wote watambae wakiwa na umri huo. Kna wengine wanaenda mpaka miezi 10. Na wengine hawatambai kabisa, wanajivuta kwa tumbo na wanaingia kwenye stage ya kusimama. Kama ukimwangalia anaonekana hana tatizo lolote basi usiwe na wasiwasi. Kama vipi mpeleke kwa dr amwangalie. Mimi wa kwangu mmoja hakutambaa kabisa bali aliingia kwenye stage ya kusimama moja kwa moja.
 
hatambai ukimuweka hata kujaribu kumove hamna...anakua kama anataka kujivuta hawezi kabisa kumove Wala kutambaa

Unamuwekea kitu anataka haswa ili ajisogeze kukifata? Hii ni afajisukuma na kuwa anapiva mweleka pole pole atafika.

Natumaini anaweza ku move na kujigeuza akiwa umemlaza. Kama sio basi kuna tatizo.

Je, anaweza kujaribu kujinyanyua anyanyuke labda kwa kushikilia meza au kitu ili asimamie?

Kuhusu kutambaa na ukuaji, kila mtoto ana muda wake ila kuna kitu hisia za Mama sasa hapo ni kufikiria na kuchukua hatua.

Najua kuna watoto wanakuaga fasta hawatambai bali watakuja kusimamia na kutembea.

Mafupi yangu ni hayo.
 
Habar wakuu nimekuja kwenu kutaka mawazo bint yangu wa Umri miez 6.5 hatambai ukimuweka hata kujaribu kumove hamna...anakua kama anataka kujivuta hawezi kabisa kumove Wala kutambaa...nimekuja kwenu kutaka ushauri nin chakunya aweze kutambaa kumove nakusimama ....naaambiwa kuwa nawatu kwa umri wamiez sita alitakiwa awe ameanza kutambaa ...msaada wenu wakuu
Mtoto wangu wa Kwanza hakutambaa kabisa.
Alianza kusimamia vitu akatembea.
Hata last Born wetu hakutambaa Kabisa.
 
Namuwekea kitu anataka haswa ili ajisogeze kukifata? Hii ni afajisukuma na kuwa anapiva mweleka pole pole atafika.

Natumaini anaweza ku move na kujigeuza akiwa umemlaza. Kama sio basi kuna tatizo.

Je, anaweza kujaribu kujinyanyua anyanyuke labda kwa kusikiliza meza au kitu ili asimamie?

Kuhusu kutambaa na ukuaji, kila mtoto ana muda wake ila kuna kitu hisia za Mama sasa hapo ni kufikiria na kuchukua hatua.

Najua kuna watoto wanakuaga fasta hawatambai bali watakuja kusimamia na kutembea.

Mafupi yangu ni hayo.
my son na mdogo wetu wa mwisho hawakutambaa kabisa.
 
Mkuu acha wenge,Iwapo miguu ina nguvu,mikono ina nguvu na shingo ina nguvu na ana flexibility na anacheza vizuru basi uache kiherehere.Wewe mwenye Ulitembea ukiwa na 2 Years.Halafu achana na stori za watu wanasema.Hakuna wanachojua zaidi ya maneno ya kukuumiza Moyo.Kama una wasiwasi nenda muone Daktari
 
Mtoto wa miezi sita yupo kweye umri wa kukaa,kulazimisha atambae ni kujipa stress tu,kuwa na subra mtoto tutasema anachangamoto ya kutambaa kama akifikisha miezi 9 na hatambai,hasogei wala kuanzia kusimamia vitu.

Kila mtoto anakuwa tofauti na mtoto mwingine hata kama wamezaliwa siku moja, usiringanishe watoto,pia itategemea na sababu nyingine kama Lishe,magonjwa,pamoja na exposure na overprotective parents, mtoto muda wote mikononi na kwenye kochi [emoji28]

Kuwa na amani

Mtoto anakaza shingo na miezi 3-4
Kukaa 4-7 months
Kutambaa 7-9 months
Kutembea 9-18 months
 
Hiyo Ni dalili mbaya katika mfumo wa ubongo,, anaweza kuchelewa pia kuzungumza au akawa na akili za polepole. Mtoto anapowahi kufanya vitu maana yake ubongo wake Ni very bright. Tafuta ushauri wa wataalam wa watoto
 
Habar wakuu nimekuja kwenu kutaka mawazo bint yangu wa Umri miez 6.5 hatambai ukimuweka hata kujaribu kumove hamna...anakua kama anataka kujivuta hawezi kabisa kumove Wala kutambaa...nimekuja kwenu kutaka ushauri nin chakunya aweze kutambaa kumove nakusimama ....naaambiwa kuwa nawatu kwa umri wamiez sita alitakiwa awe ameanza kutambaa ...msaada wenu wakuu
Hivi ukizaa kichanga siku hiyohiyo kikaanza kusimama na kupiga mbio!!!!😀😀😀😀 Wee mwenyewe utatoka nduki!😁😁
Miezi 6.5 bado mchanga. Kuna wengine upitiliza na kuanza kusimama na kutembea! Stage ya kutambaa wanairuka!
 
Habar wakuu nimekuja kwenu kutaka mawazo bint yangu wa Umri miez 6.5 hatambai ukimuweka hata kujaribu kumove hamna...anakua kama anataka kujivuta hawezi kabisa kumove Wala kutambaa...nimekuja kwenu kutaka ushauri nin chakunya aweze kutambaa kumove nakusimama ....naaambiwa kuwa nawatu kwa umri wamiez sita alitakiwa awe ameanza kutambaa ...msaada wenu wakuu
Kuchelewa hatua ni kawaida sometimes japo sio kwa wote mtoto wangu hakutambaa wala nini ila akaja akaanza kusimamia kwenye vitu mwisho tukaona anatembea mwaka mmoja na nusu😀😀 halafu alivoanza kutembea akawa akianguka anashindwa kuinuka mwisho akaona aaanze kutambaa tu
Ushauri tulipokea mwingi sana ila mwisho tulimuachia mungu tu
 
Hana tatizo lolote huyo mtoto wetu bhana wengine wanachelewa kutambaa na baadhi ya hatua kama kutembea itakua ya haraka kuliko kutambaa..
 
Back
Top Bottom