chipalila1
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 259
- 32
Ndugu wana JF mada tajwa hapo juu inahusika, mtoto wangu ana zaidi ya mwaka sasa lakini hawezi kutambaa wala kutembea mwenyewe, alipotimiza mwaka mmoja kamili nilimpeleka hospitali ya rufaa, madaktari wakamchumnguza na kudai hana tatizo kwani viungo vyake vipo vizuri, pamoja na majibu hayo ya madaktari lakini mtoto bado hawezi kutembea mwenyewe bila msaada wa baby walker.
Naomba msaada kwenu wataalamu nadhani hapa JF kuna wataalamu wa kila aina wengine wamesomea mambo haya na wengine wamekutana na jambo hili na wakafanikiwa kulitatua hivyo ni imani yangu nitapata ufumbuzi wa tatizo hili.
Natanguliza shukrani