Msaada, mtoto wangu hatembei

Msaada, mtoto wangu hatembei

chipalila1

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
259
Reaction score
32
Ndugu wana JF mada tajwa hapo juu inahusika, mtoto wangu ana zaidi ya mwaka sasa lakini hawezi kutambaa wala kutembea mwenyewe, alipotimiza mwaka mmoja kamili nilimpeleka hospitali ya rufaa, madaktari wakamchumnguza na kudai hana tatizo kwani viungo vyake vipo vizuri, pamoja na majibu hayo ya madaktari lakini mtoto bado hawezi kutembea mwenyewe bila msaada wa baby walker.

Naomba msaada kwenu wataalamu nadhani hapa JF kuna wataalamu wa kila aina wengine wamesomea mambo haya na wengine wamekutana na jambo hili na wakafanikiwa kulitatua hivyo ni imani yangu nitapata ufumbuzi wa tatizo hili.

Natanguliza shukrani
 
Watoto wengine wanachelewa kutembea mpaka mwaka mmoja na nusu au zaidi. Kuwa na amani atatembea muda ukifika.
 
Unataka awahi kutembea Auende wapi!??? Kuwa mpole ndo kwanza mwaka mmoja... Nlijua miwili bhna[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Watoto wengine wanachelewa kutembea mpaka mwaka mmoja na nusu au zaidi. Kuwa na amani atatembea muda ukifika.
Tumesubiri sana mkuu ni nwaka na miezi 6 sasa
 
Nijibu maswali yafuatayo

Mtoto anauzito kiasia gani?
Vyakula gani anapewa?
 
Jaribu kutompa baby walker, inadumaza sana watoto
 
Huwa inatokea, kuna watoto huwa hawatambai inatokea siku anasimama na kutembea,
Huu uzi umenikumbusha ushauri uliotolewa huko fb, "ushauri jaman, mtoto wangu hatembei" jibu likatoka hana pa kwenda.
 
Huna haja ya kuwa na wasi wasi. Japo hujasema mtoto ana umri gani, ila inaonekana bado ni mdogo. Sana sana mpe vyakula kama samaki au dagaa aweze kukomaa mifupa mapema. Usiwe na wasi wasi anaweza kuchelewa kutembea lakini badaye akatembea vizuri.
 
Huna haja ya kuwa na wasi wasi. Japo hujasema mtoto ana umri gani, ila inaonekana bado ni mdogo. Sana sana mpe vyakula kama samaki au dagaa aweze kukomaa mifupa mapema. Usiwe na wasi wasi anaweza kuchelewa kutembea lakini badaye akatembea vizuri.
Mkuu ana umri wa mwaka na miezi 6
 
Lishe inaonekana haiko vzr maana mtoto wa umri huo anatakiwa kuwa na uzito usio kg 12 kazana na lishe
 
Je, anakaa mwenyewe aamkapo au unamkalisha? Kama anakaa mwenyewe usimhangaishe. Atatembea siku si nyingi. Watoto wana vituko vyao. Wapo ambao huketi tu, wakisimama tu huondokea mbele kwa mbele tena mbio, hawatambai. Wapo wengine hutambaa speed ya ajabu na wakisimama hakuna tena kutambaa. Usiogope, muda wake bado.
Swali; Je, umechepuka kidogo?? Wengine wanasema ati kanyonyea maziwa ya mwenzake. Hata ukipimwa na kuonekana una mimba ya mume/babake. Endelea kumnyonyesha mtoto hadi mwezi kabla hujajifungua. Ila, lishe yako iwe nzuri tu
 
gfsonwin I will forever cherish you my sis.

Ulinisaidia sana kipindi watoto wangu walikuwa wachanga.
 
Back
Top Bottom