SuperHb
JF-Expert Member
- Mar 21, 2016
- 911
- 751
Rejea hapo juu....naomba niende kwenye mada husika..
Nina mdogo wangu alimtambulisha binti nyumbani kwa wazazi wetu, wazazi wakambariki baada ya hapo binti aliendelea kuishi kwao
Kwa bahati mbaya au nzuri binti alipata Ujauzito ,ikabidi binti atoroke aje kwa mwanaume ili Nyumbani wasigundue kama kapata mimba
Basi mwanamke alihamia kwa mwanaume na taratibu za kwenda kuongea nyumbani kwa binti zikafuata. Nyumbani kwa binti wakasema wasubiri watapewa majibu, kwa ngoja wawasiliane na wazazi wao husika walioko mkoa mwingine, maana binti alilelewa na Bibi yake.
SASA TATIZO LILIPO...
Sasa Baada ya mwanaume ambaye ni mdogo wangu baada ya kukaa na binti kwa miezi miwili anataka amfukuze Hamtaki tena, na isitoshe binti mwenyewe ana mimba, anasema hana mapenzi nae, yupo anayempenda rohoni kwamba huyu ilikuwa bahati mbaya...
Kwahyo huyu mdogo wangu ameenda kwa wazazi akawaambia hamtaki anataka amfukuze binti hana mapenzi nae tena. Sasa kesho nimeitwa kwenye kikao Mimi, mdogo wangu ambaye ni mhusika pamoja na Wazazi kwa ajili ya kulijadili hili.
KWA KUKUMBUSHIA...
Huyu dogo anaye binti ambaye yuko naye katika mahusiano tangu nyuma sema wametengana kama miaka miwili hivi binti alienda kimasomo, ila bado wanawasiliana vizuri mpaka sasa hivi. HUYO NDO ANAYEMPENDA KUTOKA MOYONI MWAKE NDO ANATAKA AMUOE
NAOMBENI USHAURI NINI CHA KUFANYA NDUGU ZANGU