Msaada: Mwanamke niliyezaa naye alienda kwao baada tu ya kujifungua, hataki nimuone mtoto

Msaada: Mwanamke niliyezaa naye alienda kwao baada tu ya kujifungua, hataki nimuone mtoto

kikiboxer

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2017
Posts
3,668
Reaction score
9,809
Wakuu Salaam,

Moja kwa moja kwenye mada. Mwaka juzi nilipata mtoto na mwanamke mmoja nilikuwa nikiishi naye wakati huo.

Kipindi chote cha ujauzito alikuwa akiishi kwangu mara baada ya kujifungua akaenda nyumbani kwao kupata msaada wa karibu. Alijifungua vizuri mtoto wa kike na baada ya miezi 2 alikuja na mtoto na kukaa siku kadhaa akarudi tena kwao.

To cut story short ni kwamba ilipita muda haji kwangu na kuomba tu matumizi ya mtoto kupitia simu baada ya muda kupita nikamwambia nataka nimuone mtoto mana nimemmiss muda sasa akawa analeta story tu mtoto hamleti.

Nikaamua kukata kutuma hela hadi mtoto aje/aletwe nimuone basi ikawa shida hakumleta mtoto tangu muda huo. Umepita muda sasa mwaka sijamuona mtoto nahitaji kumuona nimeenda kwao lakini nazungushwa kwamba hayupo kasafiri wakati marafiki zake wanasema yupo.

Sasa wakuu naomba tusaidiane nianzie wapi ili kushinikiza kumuona huyu mtoto niende serikali za mtaa au police kabisa? Na kama kuna njia nyingine ya kufanya kumuona tu mtoto mana najua sitaruhusiwa kumchukua kwani bado mdogo.

N:B huyu mwanamke sikumtolea mahari tuliishi pamoja tu tukapata mtoto.
 
Mkuu habari,,Hilo swala lako ni dogo Sana,,,

Kwanza inaonekana hiyo mimba si yako ni ya mwanaume mwingine ndio maana baada ya kujifungua hataki kuishi na wew ili kuzuia mtoto asibemendwe na sperm za mwanaume mwingine ambaye ndio wew.
 
Mkuu nyumbani kwao ndio hao wanaonizungusha nimeenda mara 2 sasa sipati jibu la kueleweka.
Basi washajua mtoto sio wako ukienda ukiondoka itakua wanakucheka sana unavyohangaika wewe barizi jaza mwingine tu upate wa kwako
 
Baba yake yupo nae wewe geresha tu mkuu wanawake wanajua hizo mbinu "zugaring approach"
Mkuu nashukuru kwa ushauri huu lakini nachotaka nimalize kabisa hili suala. Nifunge kurasa kama nina mtoto nae au sina isije badae nikajutia kwamba mtoto ni wangu na nilimwacha kwa muda mrefu.

Hata kama sio wangu nijue tu sitadai gharama wala sita laumu mtu ila niwe free sina kwamba sina mtoto nae. Kwa sasa wakati mwingine roho inaniuma nikikumbuka nina mtoto na sifanyi lolote juu yake.

Nikithibitisha sio wangu nitakuwa free zaidi kwani hata sasa ninaishi na mwanamke mwingine.
 
Acha naye jogoo hatunzi vifaranga ....hawawezi kukusingizia eti umekataa majukumu...maana umeenda hadi kwao wanakuficha sepa
Nina taka kufanya hivo ila sasa upande wa nyumbani kwetu huwa wanamuulizia huyu mtoto nami nakosa cha kuwajibu.
 
Inaonekana uyo dada anaujua ukwel mzima iweje amfiche mtoto kuna nn katikati hapo lazm kutakuwa kuna jambo aidha mtoto sio wako ila uyo dada anamjua mwenye mtoto
 
Kuna uwezekano mkubwa mama mtoto wako hakua na uhakika juu ya mmilik wa ujauzito ndo maana mlikaa wote katika kipind cha ujauzito.Inaonekana baada ya kujifungua amegundua mtoto sio wako na ndo maana halalamiki kuhusu matunzo.
 
Mbegu bado zipo za kutosha mkuu hapa nilipo naishi na mdada tayari anatema mate.

Shida ni kuwa nawaza nina mtoto mwingine ambaye sina hakika kama atakuja au hatokuja.
Kama hataki Umuone anakuzungusha huyo sio mwanao lakini na wewe Uliishi nae miezi yote ya mwanzo ile KUMUANGALI TU MTOTO hukuona kama umepigwa???? Au ndo hujui kufananisha.. ndugu zako nao pia hawajui??? Anyway cha muhimu huyo mwanamke mtafute mkaee usikute kamgawa mwanao kisa kuna mwanaume anatoa pesa zaidi yakoo yani PELEKA KESI POLISI Kama sio ustawi wa jamiii ili jambo liishe kisheria sio kwa maneno mkuu..! Pole sana ila Simamia hili jambo mapema bora upoteze muda na hela hata kwa kupima DNA ili nafsi yako iwe Huru pole sana.
 
Mkuu nashukuru kwa ushauri huu lakini nachotaka nimalize kabisa hili suala. Nifunge kurasa kama nina mtoto nae au sina isije badae nikajutia kwamba mtoto ni wangu na nilimwacha kwa muda mrefu.

Hata kama sio wangu nijue tu sitadai gharama wala sita laumu mtu ila niwe free sina kwamba sina mtoto nae. Kwa sasa wakati mwingine roho inaniuma nikikumbuka nina mtoto na sifanyi lolote juu yake.

Nikithibitisha sio wangu nitakuwa free zaidi kwani hata sasa ninaishi na mwanamke mwingine.
Mkuu ukitaka kudhibitisha ni DNA peke yake.
 
Kama hataki Umuone anakuzungusha huyo sio mwanao lakini na wewe Uliishi nae miezi yote ya mwanzo ile KUMUANGALI TU MTOTO hukuona kama umepigwa???? Au ndo hujui kufananisha.. ndugu zako nao pia hawajui??? Anyway cha muhimu huyo mwanamke mtafute mkaee usikute kamgawa mwanao kisa kuna mwanaume anatoa pesa zaidi yakoo yani PELEKA KESI POLISI Kama sio ustawi wa jamiii ili jambo liishe kisheria sio kwa maneno mkuu..! Pole sana ila Simamia hili jambo mapema bora upoteze muda na hela hata kwa kupima DNA ili nafsi yako iwe Huru pole sana.
Mkuu hichi ndio ninachotaka.
Kumaliza kabisa hili suala ili badae lisije kuibuka tena. Kama sio wangu mimi sina tatizo kwani watoto nitapata zaidi wala sitadai gharama za kumtunza nachotaka ni kuweka record sawa kama wangu aendelee kukaa huko akikuwa nimchukue au kama si wangu basi tufunge kurasa kabisa. Mana juzi kati alipiga simu kuhusu mtoto nikatuma hela kiasi.

Asante sana mkuu nadhani nianzie serikali za mtaa nipande mpaka police tujue kipi ni kipi.
 
Back
Top Bottom