Msaada: Mwanangu ana miezi 12 bado hajaanza kutambaa, yeye ni kukaa tu

Msaada: Mwanangu ana miezi 12 bado hajaanza kutambaa, yeye ni kukaa tu

Bado mapema ila kwa tafadhari, uwe unamlazimisha kusimama na kumshika mikono yake miwili unakuwa unamlazimisha kujongea au unabeba miguu yake juu ya yakwako mnatembea wote wewe chini yeye juu, ata kama hajaanza kutambaa lazima ataonesha ushirikiano.

Mwisho mruhusu kucheza na wenzake mara kwa mara asizubae.
 
Miaka ya zamani niliwahi kusikia mtoto kuchelewa kutambaa/kutembea inatokana na either Mzazi mmoja anacheza michezo ya nje hivyo kumuathiri mtoto.

Walienda mbali na kusema ukiona mtoto kiuno hakikazi yaani kina shake shake ujue kesi ni hiyo hiyo kama ya juu.

Ukiwasikia Wanasayansi wao wanasema itakuwa mtoto hapati lishe ya kutosha au ana obesity.

Kama una Wazee nyumbani kwenu, jaribu kuwaulizia.

Pole sana
 
Bado mapema ila kwa tafadhari, uwe unamlazimisha kusimama na kumshika mikononyake miwili unakuwa unamlazimisha kujongea au unabeba miguu yake juu ya yakwako mnatembea wote wewe chini yeye juu, ata kama hajaanza kutambaa lazima ataonesha ushirikiano.

Mwisho mruhusu kucheza na wenzake mara kwa mara asizubae.
Miguu yake hajaweza kuikaza kwa kumnyanyua, na tulimpeleka kwa daktari akasema mbona hanashida ya miguu ila hawezi kuikazisha chini hata ukimnyanyua
 
Miguu yake hajaweza kuikaza kwa kumnyanyua, na tulimpeleka kwa daktari akasema mbona hanashida ya miguu ila hawezi kuikazisha chini hata ukimnyanyua
Ok kama haijakaza vizuri ,unamlaza chali harafu unashika miguu yake na kuwa unainyoosha na kuikunja (kama vile mtu anavyotembea (kushoto unakunja kulia unanyoosha, kulia unakunja kushoto unanyoosha) ....unaanza taratibu akizoea unaongeza speed, iwe kama mchezo siyo karate.😄😄😄
 
Habari ya muda huu.

Mwanangu wa miezi 12 hajanza kutambaa, naombeni ushauri wenu ila alichelewa kulia wakati wakuzaliwa lakini pia degedege huwa inamsumbua.


Naombeni ushauri wenu namna ya kumsaidia inaniuma saana ndugu zangu.😭😭😭
Hii Case kuitatua moja kwa moja hapa itakua changamoto. Chakufanya tembelea hospitali waambie unataka kuonana na Daktari wa watoto (PAEDIATRICIAN) wamuangalie vizuri.

Maana watoto ambao walichelewa kulia huwa wanapatwa na upungufu wa Oxygen katika ubongo hivyo ubongo kutokufanya kazi yake vizuri. Mara nyingi huwa wanapatwa na hiyo shida ya degedege pia kupungua kasi ya ukuaji(delayed milestone).

Lakini anaweza kurejea katika hali yake ya kawaida ikiwa atapata matibabu mapema. Atapata dawa ya degedege ambayo atakua anatumia huku akihidhuria clinic ya watoto na ikiwezekana Tiba ya mazoezi (physiotherapy).

Sijaweza kutaka moja kwa moja shida ya kutembea vizuri kwa sababu natakiwa kuchukua history ya mama tangu ana mimba mpka alijifunguabkwa njia gani, na ukuaji wa mtoto uliendeleaje mpka hapo (medical history taking /clerkship)
 
Back
Top Bottom